Tajiri wa Nigeria, Aliko Dangote, sasa ndiye mtu wa pili kwa utajiri barani Afrika kulingana na orodha ya hivi punde ya Forbes .
Dangote aliachwa nyuma ya bilionea wa Afrika Kusini Johann Rupert, ambaye ni mwenyekiti wa kampuni ya bidhaa za kifahari ya Uswizi Compagnie Financière Richemont...