Chemsha Bongo: Mwenye duka alipata hasara ya shilling ngapi?

KijijiForums

Official Account
KF Moderator
Joined
Jun 5, 2023
Messages
26
Reaction score
57
Points
0
Binti Kidawa alikwenda dukani kununua mkate na noti ya 1000. Akakuta mkate unauzwa 700, akatoa elfu 1 na kumpa muuzaji. Muuzaji hakuwa na chenji ikabidi akaombe chenji dukani kwa Manka. Baada ya muda kidogo Binti Kidawa akarudi kwa muuza duka na kumwambia noti ya elfu 1 aliyompa ni feki. Muuza duka sababu alikuwa bado hajapata chenji ikabidi ampe elfu 1 nyingine.

Je, muuza duka alipata hasara ya kiasi gani?​
 
Kumbe ni kidawa alikuja kurudisha elfu? Nikajua ni manka!
Sasa hapo hasara haiwezi kujulikana maana pengine muuza duka ni tapeli anahela feki nyingi anafanya mchezo wa kuzisafisha..😎😳
Kwa nini elfu 2?
Kwa sababu hawajazema kuwa hela feki kapewa na Kidawa

Inaonekana hela feki alikuwa nayo mda mrefu. So hasara 1000

Though nakubali kukosolewa sina uhakika
 
Kumbe ni kidawa alikuja kurudisha elfu? Nikajua ni manka!
Sasa hapo hasara haiwezi kujulikana maana pengine muuza duka ni tapeli anahela feki nyingi anafanya mchezo wa kuzisafisha..😎😳
Haha 😆
 
Muuza duka ndio ametoa hela mara mbili soma vzri
ndo mafumbo yalivyo yanaandikwa kwa lugha ya utata....

hapo kuna maana mbili, kidawa kampa mwenye duka buku nyingine, au mwenye duka ndo kampa kidawa buku

kwa vile mwenye duka hana sababu ya kumpa kidawa buku, basi tutaegemea kwenye maana ya kwanza....

afu pia kwa vile kidawa kamuambia mwenye duka buku ya mwanzo ni feki, basi tutachukulia hiyo ya pili kaitoa yeye kwasababu mwanzoni alitoa hela feki
 
Mimi mwanzo sikuona hvo, nlizani manka ndio alirudisha hela,, kwa hoja zako hapo kiswahili ndio kimeleta utata
 
Similar threads

Mwanamke mmoja aliingia Dukani na kuiba Sh.100 bila mwenye Duka kujua. Baada ya dk5 akarudi na kununua kitu chenye thamani ya Sh.70 kwa kutumia ile hela aliyoiba. Mwenye duka akamrudishia chenji ya Sh.30 Mwenye Duka Kapoteza Sh. Ngapi? A: 30 B: 70 C: 100 D: 130 E: 170 F: 200
Replies
1
Views
170
Kijana aliyekuwa karibu na dereva aliulizwa ni nani kwako anayeendesha? akajibu "kaka mkubwa wa mjomba wake na dereva ni mjomba wangu" Je dereva ni nani kwa kijana yule?
Replies
1
Views
194
Baba mmoja alikuwa na mabinti Sita na kila binti alikuwa na kaka mmoja. Je, baba huyu alikuwa na watoto wangapi?
Replies
3
Views
269
Chidola na Chilemba ni watoto mapacha. Kesho Chidola atasherekea siku yake ya 5 ya kuzaliwa. Chilemba yeye itabidi asubiri mpaka mwaka ujao pale atakapofikisha umri wa miaka mitano ndio asherekee siku yake ya kuzaliwa. Je, Leo ni tarehe ngapi?
Replies
3
Views
587
Nina mayai sita Nimevunja mawili Nimekaanga mawili Nimekula mawili Je, nimebakiwa na mayai mangapi?
Replies
2
Views
180

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top