- Jul 9, 2023
- 3,821
- 3,805
- 113
Kipindi ambacho dunia imekuwa sawa na kijiji kidogo, mawasiliano ni rahisi mno. Mpaka leo hayajatolewa majibu; kwa nini ilikuwa vile. Ilitokeaje? Ukweli ni upi?
Taarifa zikaanza kutolewa mitandaoni kuwa Rais Magufuli alikuwa na hali mbaya kiafya. Ikaelezwa alifikishwa mpaka Kenya. Wapo waliodai alipelekwa India.
Serikali yake ilitangaza kuwa Magufuli alifariki Jumatano Machi 17 wakati alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja Dar. Hata hivyo inaripotiwa kuwa Magufuli huenda alifariki Machi 11 lakini serikali ikadinda kuweka hilo wazi. Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu ni miongoni mwa wanamtandao ambao wanaamini ukweli kuhusu kifo hicho ulifichwa.
Magufuli alifariki Mzena? Tanzania
Kuna mtu anaitwa Evarist Chahali, yeye hujitambulisha kama mtumishi wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa na alishapata kufanya kazi ya uchambuzi wa masuala ya siasa na jamii kwenye magazeti kadhaa nchini. Chahali ndiye alikuwa wa kwanza kusema Rais Magufuli alishafariki dunia. Chahali akaeleza kuwa taarifa za Rais Magufuli kupelekwa India hazikuwa za kweli, bali alifia Hospitali ya Viongozi, Mzena, Kijitonyama, Kinondoni, Dar es Salaam.
(Soma: https://www.mwananchi.co.tz/mw/haba...agufuli-kilivyotoa-funzo-usiri-mifumo-3638688)
Magufuli alifariki nchini Kenya? (imeripotiwa na TUKO - Kenya)
"Duru ziliniarifu kuwa Magufuli alifariki Kenya Alhamisi na mwili wake kusafirishwa Tanzania kusubiri masuala ya mageuzi serikalini kupangwa," Lissu alisema.
Kulingana na duru katika hospitali moja jijini Nairobi, Magifuli alifika humu akiwa katika hali mbaya na madaktari kujaribu kuyaokoa maisha yake. Hata hivyo hali ilionekana ngumu na hospitali hiyo ikashauri watafute matibabu kwingine ya dharura zaidi. Hayo hayakuwezekana na madaktari wakasema hakuna linaloweza kufanyika kwa kiongozi huyo.
(Soma: https://kiswahili.tuko.co.ke/406273...uenda-alifariki-lakini-serikali-ikaficha.html)
Magufuli alifariki nchini India?
Kiongozi mkuu wa upinzani Tanzania, Tundu Lissu, amesema Alhamisi kuwa rais John Magufuli, ambaye hajaonekana hadharani kwa karibu wiki mbili, yuko India akitibiwa virusi vya corona na kwamba yuko katika hali mbaya.
(Soma: https://www.dw.com/sw/lissu-asema-magufuli-amehamishiwa-india-akiugua-covid-19/a-56841246)