Interlocking blocks - Ujenzi tofali za kisasa

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Muhindi Wa Kuchoma

Well-known member
Platinum Villager
Joined
Jul 9, 2023
Messages
3,821
Reaction score
3,805
Points
113
Ujenzi wa nyumba kwa kutumia matofali ya kufungamana ni mojawapo ya aina ya ujenzi wa gharama nafuu ambao huondoa matumizi ya udongo mwashi kama kiunganishi kati ya tofali na tofali ingawa mambo yote ya msingi na kanuni za ujenzi lazima vizingatiwe.

Kabla ya kuanza ujenzi ni lazima kuwe na msingi imara uliojengwa kwa vifaa imara ambao upo kwenye vipimo sahihi, ili kuweza kutumia tofali hizi. Sehemu ya msingi wa nyumba (substructure) itakuwa na-:
  • Kitako cha msingi: zege/mawe
  • Ukuta wa msingi: Matofali ya saruji na mchanga, udongo na saruji yanayofungamana, mawe au matofali ya kuchoma.
Endapo tofali za udongo-saruji za kufungamana zitatumika ni lazima unene wa ukuta wa msingi usipungue sm 30 (urefu wa tofali). Ili kukabiliana na hali ya unyevunyevu ni vyema kuimarisha zaidi tofali kwa kuongeza kiwango cha saruji kwenye udongo wakati wa ufyatuaji.
Ujenzi kwa kutumia matofali ya udongo au udongo ulioimarishwa umeonekana kuwa wa gharama nafuu zaidi kutokana na upatikanaji wa udongo katika sehemu kubwa nchini.

Katika ujenzi huu tofali linalotumika huwa na vipimo vifuatvyo: Urefu 300mm, Upana 150mm na Unene 100mm. Vilevile kuna vipande vya nusu na robo tatu tofali.
1690843829424.png
Tofali Zima​

Kabla ya kuanza ujenzi ni lazima kupitia ramani iliyopo ili kuona kama inakubaliana na vipimo vya urefu wa ukuta ambapo ni lazima vigawanyike kwa tofali zima au nusu (yaani 300 au 150mm).
1690843939945.png
Tofali Nusu​

Mfano ukuta wenye urefu wa mita 3, hujengwa kwa tofali nzima 10, katika mstari mmoja wenye urefu huo. Ikumbukwe kuwa katika ujenzi huu hatukati vipande vyenye urefu mbalimbali kama ambavyo hufanyika katika ujenzi wa matofali yasiyofungamana, badala yake vipande vya nusu na robo tatu hutumika.
1690844007950.png
Tofali Robotatu​

Nyumba imegawanyika katika sehemu kuu mbili:-
  • Msingi: Sehemu ya chini ya nyumba (substructure)
  • Boma: sehemu ya juu ya msingi
Msingi: Msingi wa nyumba hujengwa kwa:
zege, mawe, matofali ya saruji na mchanga, na matofali ya udongo na saruji.
1690844333437.png
Namna ya kuset matofali ya kufungamana kwenye msingi uliojengwa kwa matofali ya saruji na mchanga.

Kwa kuwa msingi ndio sehemu inayobeba mzigo wa jengo zima ni muhimu vifaa vinavyotumika kuujenga viwe bora na imara. Kwa maeneo yaliyo mengi nchini zege, mawe na tofali za saruji mchanga ndio hutumika kujenga msingi wa nyumba. Hata hivyo matumizi ya udongo na saruji hutumika kujenga misingi kwa maeneo yenye udongo imara. Lakini mchanganyiko wake ni lazima uboreshwe zaidi ili kupata tofali imara lenye uwezo wa kubeba uzito na kuhimili hali ya unyevunyevu.

Boma: Sehemu hii ya nyumba hujengwa kwa kutumia zege, mawe, matofali ya mchanga na saruji, matofali ya udongo na saruji, matofali ya udongo na chokaa au matofali ya udongo. Ujenzi kwa kutumia matofali ya udongo au udongo ulioimarishwa umeonekana kuwa wa gharama nafuu zaidi ukilingnisha na ujenzi wa matofali ya saruji na mchanga. (itaendelea toleo lijalo)
1690844243619.png

Source
 

Katkit

Well-known member
Platinum Villager
Joined
Jun 8, 2023
Messages
693
Reaction score
2,144
Points
93
Bomba sana hii, lakini mimi sitakuja kujenga.
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Nyumba ikikamilila inapihwa vanish inakuwa nzuri sana
Nilishawahi waza iko siku nitafarua matofali yangu mwenyewe kujenga nyumba hii.
 

Similar threads

Picha mbalimbali za muonekano wa daraja la JPM lenye urefu wa kilomita 4.6 linalojengwa katika eneo la Kigongo - Busisi, jijini Mwanza. Leo Juni 14, 2023 Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alifanya ukaguzi maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo linalogharimu shilingi bilioni 716, ambapo ujenzi wake...
Replies
3
Views
118

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom