Je, walimu wavae sare mashuleni?

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,617
Reaction score
26,430
Points
113
Kwa nini wanafunzi wanavaa sare?
Hili swali limekuwa likiulizwa mara nyingi na wanafunzi dunia nzima. Wengi wakitaka kujua nini hasa lengo la kuvaa sare za shule. Baadhi ya shule zimeenda mbali zaidi na kuruhusu wanafunzi kuvaa nguo zao za nyumbani. Lengo hasa la kuweka sare ni kuhakikisha usawa na utambulisho wa wanafunzi.

Lengo la mijadala hii ni kujua hasa nini mantikii ya kuvaa sare shuleni ikiwa sare zinavaliwa na wanafunzi pekee. Kuvaa sare kwa walimu kungeleta maana zaidi kwa wanafunzi kuvaa sare masjhulenj. Kuna makundi kibao yanavaa sare ikiwemo maaskari, wahudumu wa afya, wafanyakazi wa taasisi binafsi nk.


Karibuni kwenye malumbano kwa hoja, wanaokubali hoja na wanaopinga hoja. Hoja inauliza Je walimu wavae sare mashuleni?
 
ili maskini awe sawa na tajiri😅
Masikini na tajiri
Tunatofautina kwa mengi mfano, mweupe na mweusi, mrefu na mfupi, makabila yanatofautiana, akili na uongozi.

Sasa polisi wakivaa sare mkubwa utamjua kwa cheo. Mwalimu mkuu anaweza vaa nguo mbovu wakati walimu wake wana nguo nzuri huoni hii haileti picha nzuri
 
Hapana sio kweli
 
Ningeshauri wavae sare ya damu ya mzee(usiulize kwann...
 
Naunga mkono hoja
Kwani hata walimu tarajali wanapokua vyuoni huvaa Sare hasa Hawa wa shule za msingi. Kwa nini wasiendelee kuwa na Sare hata wanapokua makazini ili
1. Kuwatambulisha wao Kama walimu kupitia mavazi hata wanapokatiza mitaani Kama Kada zingine i.e police na nurse 2. Kuleta usawa kwao wenyewe walimu kwani Sare husaidia Kwa namna fulani kuondoa Tabaka la wanaotupia na wasiotupia. 3. Nadhani ingechochea hata wanafunzi kuzipenda zaidi Sare zao Kwa kuwa watawaona walimu wao ni miongoni mwao
 
Walimu hawana haja ya kuvaa sare kwakua huduma yao wanatoa kwa watu wanaowatambua (wanafuzi) lakini pia hata rika wanatofautiana sana na wanafunzi. Ndio maana ukienda shuleni ukamuuliza mwanafunzi akuonyeshe mwalimu fulani atakuonyesha, Ingekua kuna haja ya kuvaa sare kama wangekua hawana vituo specific vya kuhudumia yani leo unamkuta shule hii kesho unamkuta shule ile, keshokutwa kwingine.

Tofauti na hospitalini au polisi kwanza kabisa ni kazi nyeti zenye uwezo wa kumuathiri mtu moja kwa moja, chukulia ukutane na mtu amevaa kawaida lakini amebeba SMG/AK47 yupo anarandaranda tu, kwaiyo hata vikundi vya uhalifu isingekua rahisi kuwagundua mapema, au polisi pia wangeweza kutumia mwanya huo kufanya uhalifu pale wanapoona fursa.

Chukulia pia unahitaji msaada wa haraka hospitalini au hata njiani, hospitalini inakua rahisi kujua yupi ni mhudumu wa afya ili kupata msaada kirahisi tofauti na wangekua hawavai sare. Pia njiani unaweza kupata tatizo ukasaidika mapema kama kuna askari karibu kwakua utamtambua kirahisi na sare zao.
 
Ni kweli
1. Polisi wanavaa sare
2. Wanajeshi wanavaa sure
3. Hospital madakatari na mansion wanavaa sare
4. Bank huwa wanavaa sare baadhi ya siku
5. Wafungwa wanavaa sare huko kifungoni


Kujenga usawa shuleni walimu wavae sare maalumu
 

Similar threads

Wakuu kwema? Najua walimu niwatu wanaopaswa kupewa heshima kwakua wametutoa ujinga mwingi.. Ila kuna mambo ambayo nikiwa nasoma walimu walikua wanafanya nikifikiria kwa sasa naona kama walikua na akili za kitoto au walizingua... je kuna jambo walimu wako walizingua? Au kuna utoto walimu walikua...
Replies
13
Views
385
Dodoma. Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limetoa wito kwa wananchi wote wanaomiliki au wanaouza mavazi, viatu, mabegi na vitu vinavyofanana na sare za majeshi nchini kuvisalimisha ndani ya siku saba kuanzia leo. Wito huo umetangazwa leo Alhamisi Agosti 24, 2023 jijini Dodoma na Kaimu...
Replies
3
Views
1K

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top