Licha ya mtandao wa Twitter kuzuiliwa nchini China, Billionea ambaye ndiye mmiliki wa mtandao huo anatarajiwa kuanza ziara yake nchini humo wiki hii.
Hii inakuwa ni mara ya pili baada ya miaka mitatu kupita, Elon Musk kwenda nchini China, kwani mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2020 alipokwenda kwenye tukio la kampuni yake inayozalisha Magari.
Bado haijaelezwa haswa ni nini ambacho kinampeleka nchini humo, Ila taarifa zinasema moja kati ya watu atakaokutana nao nchini humo ni mkurugenzi wa kampuni yake ya magari ambayo ina ofisi zake Shanghai, China.