Majaliwa apigilia msumari agizo la Magufuli - Jumatatu, Julai 03, 2023

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,617
Reaction score
26,430
Points
113
Tanga. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha inaratibu utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli la mikoa ya kanda ya kaskazini kuagiza mafuta kutoka ghala la Kampuni ya GBP lililopo jijini Tanga.

Alitoa agizo hilo jana, baada ya kufanya ziara ya siku moja jijini hapa na kutembelea ghala la kuhifadhia petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Awali akimkaribisha Waziri Mkuu, Mbunge wa Tanga, Ummy Mwalimu alimlalamikia akisema kwamba licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na GBP wa kujenga ghala la kupokea, kuhifadhi na kusambaza mafuta nchini na nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, wanunuzi wa mikoa ya kanda ya kaskazini, bado wananunua mafuta yanayoingizwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

"…hili linatuumiza sana watu wa Tanga, licha ya Rais John Magufuli kutembelea ghala hili na kuagiza wanunuzi wa mikoa ya kanda ya kaskazini kununua mafuta kutoka Tanga kwa sababu ni karibu, utekelezaji wake unasuasua... Serikali inatakiwa kuingilia kati," alisema Ummy, ambaye pia ni Waziri wa Afya.

Alisema ghala hilo limejengwa kimkakati, ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa malori yanayotumia Bandari ya Dar es Salaam na kwamba alitarajia wafanyabiashara wa mikoa ya jirani pamoja na kanda ya kaskazini, wangeona umuhimu wa kutumia mafuta ya kutoka Tanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa GBP Tanzania, Saad Badar alisema ujenzi wa ghala hilo ulianza mwaka 2002 kwa kuhifadhi lita za ujazo 25 milioni, ikipokea meli za lita za ujazo 6,000.

"Septemba 2015 tulifanya upanuzi tukapokea lita 200 milioni na meli ya tanki la lita 70,000 na uwezo wa kupakua tani 40 milioni kwa saa na tani milioni tano hadi milioni sita kwa siku.

"Tumeweza kuhudumia masoko ya nchi za Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nchi nyingine za Maziwa Makuu kutokana na uwezo mkubwa wa ghala letu katika kuhifadhi na kupakia shehena kwenda nchi za nje,” alisema Badar.

Agizo la Majaliwa
Akizungumza katika ziara hiyo, Waziri Mkuu aliziagiza taasisi zinazohusika na nishati katika Wizara ya Nishati kuhakikisha wanunuzi wa mafuta kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini wananunua kutoka ghala la GBP Tanga.

"Haiwezekani Mtanzania afanye uwekezaji mkubwa kama huu, halafu tumkatishe tamaa kwa kushindwa kusimamia wanunuzi kuja Tanga kununua mafuta. Wizara ya Nishati na taasisi zinazosimamia nishati, naagiza kwa mara nyingine malalamiko haya iwe ni mwisho," alisema Majaliwa.

Akiwa bandarini hapo, Majaliwa alisema Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya uwekezaji mkubwa wa upanuzi wa bandari iweze kumudu kuhudumia shehena kubwa kwa haraka.

Alitembelea bandari hiyo kushuhudia maendeleo ya mradi wa uchimbaji wa kina na upanuzi wa gati ambao utagharimu Sh429.2 bilioni hadi kukamilika.

Akitoa taarifa ya upanuzi wa bandari hiyo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Juma Kajavala alisema awamu ya kwanza ilikuwa ya uchimbaji wa kina kutoka mita tatu hadi kufikia mita 13.

Awamu nyingine ilikuwa ya upanuzi wa gati hadi kufikia mita 450 ndani ya maji, hivyo kuiwezesha bandari kupokea na kuhifadhi shehena nyingi kwa wakati mmoja.


MWANANCHI.
 

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top