Mpe ujumbe mpendwa wako aliyetangulia mbele za haki

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,628
Reaction score
26,450
Points
113
Kifo ni fumbo kubwa sana kwa mwanadamu japo wako wengi waliojaribu kufumbua fumbo la kifo wameshindwa. Hata wanasayansi wakiobobea wamejaribu kutengeneza maisha ya Kudumu ila kifo kikawaita.

Hapa kupitia uzi huu tutawakumbuka ndugu zetu au marafiki zetu waliotangulia mbele za haki kwa kuwapa salamu za upendo na kishea kumbukumbu zao na wanakijiji wenzetu

Napenda kumkumbuka Ruby
Kuna msichana nilisoma nae shule ya msingi anaitwa Ruby. Ni ndugu yake muigizaji wa bongo movie Thea. Tulipenda sana kucheza nae mpira wa miguu na alipenda sana kutubutua na mpira wa kufuma

Tukiwa darasa la tano Ruby alipatwa na kansa ya mguu tena ule mguu aliopenda kupigia mpira. Akiwa anapata matibabu ocean road walilazimika kumkata mguu. Ruby msichana mdogo wa umri wa miaka 10 tu akawa na mguu mmoja

Baadae tena taarifa ikaja kuwa kansa imeamia mguu wa pili. Hapo hata kidonda cha mguu wa kwanza hakijapona. Sitasahau siku ile nilivyomuona mara ya mwisho akiwa mweupe sana kwa kukaa ndani mda mrefu. Tulishiriki maombi ya pamoja sikuwaza kuwa haya yangekuwa maombi yetu ya mwisho pamoja

Siku chache baadae rafiki yangu Ruby alifariki na akazikwa makaburi ya Kinondoni. Nimekuwa nikimkumbuka sana Ruby na nimemtafuta Thea zaidi ya mara moja kumuomba picha ya Ruby hata nipate kuwa na kumbukumbu ya picha yake bila mafanikio.

Ujumbe wangu kwa Ruby ni kuwa bado namkumbuka. Ingawa ametutoka bado hajanitoka moyoni mwangu. Nakukumbuka sana Ruby. Ningependa siku moja tuonane tena huko Sayuni. Najua nikifa leo moja kwa moja motoni ila nitafahya jitihada kuishi vyema tuwe pamoja karamuni. .

Napenda kumkumbuka Paulo
Maisha ya ulimwengu huu hayajawahi kuwa ya haki. Kifo kilimchukua rafiki yangu mpendwa Paulo. Hata sijawahi ona kaburi lake wala kumuaga safari yake ya mwisho.

Kwa miaka hiyo huyu rafiki yangu alizaliwa afe. Hakuwahi kufurahia matunda ya maisha ya duniani..Akiwa mdogo alipoteza wazazi wake wote kwa gonjwa hatari la UKIMWI. Kipindi hicho ulikuwa unaitwa miwaya au umeme.

Nimepoteza baadhi ya watu kwa gonjwa hili ila Paulo hakupata haki. Alipata UKIMWI kutoka kwa wazazi wake. Hata wazazi wake walifariki mapema bila hata kuwa na kumbukumbu nzuri juu ya wazazi wake.

Maisha ya Paulo yalikuwa ya kuumwa umwa kila wakati. Hakuweza kucheza vizuri na watoto wa rika lake. Mtaani wazazi walizuia watoto wao kucheza na Paulo. Hakika rafiki yangu huyu alitengwa na jamii. Alifariki akiwa na miaka 11 sikuweza hata kumuaga rafiki yangu huyu.

Natumaini iko siku nitapata kumuona tena Paulo na kucheza nae michezo ya utotoni. Hakuweza kufaidi kucheza na watoto wezake. Najua Paulo amekufa kifo chema akiwa na upako wa mwisho. Endelea kupumzika kwa amani Paulo. .
 
Kambi ya jeshi Chabruma .
Nakukumbuka sana Juma ulipewa gonjwa la UKIMWI ukiwa bado ungali mdogo , ulipenda kuniarika Songea nije tufurahie maisha .

Mara ya mwisho uliniita baada ya kupewa kambi uwe mkuu wa kambi ila ningejua nakuja kukuaga sio kufurahia kupandishwa cheo hakika nisingetia miguu yangu Songea .

Ila nashukuru ile moment haifutiki kichwani mwangu tulifanya mengi ila rafiki kwanini hukuniambia kuwa utaondoka juma moja baada ya mimi kuondoka ?

Naumia sana Juma endelea kupumzika salama sijui uko Firdaus au uko wapi ? Ila jua natamani kukutana na wewe tena rafiki yangu.

Rafiki yangu , mwanasiasa , siku moja kabla ya kifo chako ulinitumia kibonzo cha Kipanya juu ya yule jamaa uliyembana kwenye mkono wa sheria .

Ukawa unacheka sana huku ukiniambia nitamnyoosha huyu mtoto , ukweli na mimi nilimkandia sana kuwa lazima atulipe ila rafiki nawaza ikiwa kosa tulilolifanya ni kumsema yule bwana basi najua punde nitaungana na wewe ila ikiwa sivyo , endelea kupumzika japo nakukumbuka sana .

Tutaonana nikija huko uliko , kilichoniskitisha ni kukutana na mwanao wa kufikia baada ya utambulisho msibani ambaye sikuyajua kabla , nakuomba kokote ulipo unisamehe rafiki sikujia ningejua ningemuheshimu sana .

Uzee ni majuto , nendeni rafiki zangu badae tutaonana .
 
When my father rejected me my grandfather accepted me
May Allah grant my grandfather jannah
Aiseee machozi yananitoka
Hii mara ya pili naona umeandika kuhusu baba yako kukutelekeza. Ushauri wangu msamehe kutoka moyoni mwako kabisa. Kwamba kumsamehe ni kwa ajili yako na sio yake. Kwa nini nakueleza haya? ni hivi imeshatokea kwenye familia na kuhifadhi moyoni hufanya mambo haya kujiridia yanakuwa kama laana. Msamaha una maana kubwa sana Allah akupe nguvu hiyo. .
 
Huyu sijui hata kama nampenda au namchukia na kwa sasa sijui hata kama yupo hai. Ila Mungu atafanya wepesi
Hii mara ya pili naona umeandika kuhusu baba yako kukutelekeza. Ushauri wangu msamehe kutoka moyoni mwako kabisa. Kwamba kumsamehe ni kwa ajili yako na sio yake. Kwa nini nakueleza haya? ni hivi imeshatokea kwenye familia na kuhifadhi moyoni hufanya mambo haya kujiridia yanakuwa kama laana. Msamaha una maana kubwa sana Allah akupe nguvu hiyo. .
 
Huyu sijui hata kama nampenda au namchukia na kwa sasa sijui hata kama yupo hai. Ila Mungu atafanya wepesi
Haya mambo huwa yanajirudia unashangaa yanatokea na wajukuu wako. Msamaha unatosha kukuweka huru. Ila sasa hakikisha unaendelea na maisha yako sio kujishungulisha nae.
 

Similar threads

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Staa huyo wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa lebo ya WCB na Mkurugenzi wa Wasafi Media Diamond Platnumz ameandika kuwa “Nakumbuka Mwaka Mmoja wakati unafanya kazi ya Saloon kariakoo, tukiwa tunarudi usiku majira kama ya saa sita hivi kwenye Daladala...
Replies
12
Views
215

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top