Muda wa kustaafu Jaji Mkuu wazua jambo

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Gily

KF Founder & Dragon IGM
Staff member
Jun 4, 2023
7,020
22,618
113
Dar es Salaam. Sakata la Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuhudumu katika nafasi ya Jaji Mkuu wa Tanzania limeibua utata baada ya Jaji wa Mahakama ya Rufani, Stella Mugasha kudaiwa kuandika barua akieleza uamuzi wa kumwongezea muda ni uvunjaji wa Katiba na kutozingatia misingi ya sheria.

Hata hivyo, barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na Jaji Stella isiyokuwa na tarehe kwenda kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi waandamizi wa Serikali walisema hawajaipata.

Wengine waliotumiwa nakala ya barua hiyo yenye kurasa kumi ambayo jana ilikuwa ikisambaa mitandoni ni Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, Jaji wa Rufani, Augustine Mwarija, Jaji Kiongozi, Mustapger Siyani, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Eliezer Feleshi na Katibu Mkuu Kiongozi.


PRIME
Muda wa kustaafu Jaji Mkuu wazua jambo
Jumatano, Juni 28, 2023

Jaji wa Mahakama ya Rufani, Stella Mugasha
By Baraka Loshilaa & James Magai
Muktasari:


Dar es Salaam. Sakata la Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuhudumu katika nafasi ya Jaji Mkuu wa Tanzania limeibua utata baada ya Jaji wa Mahakama ya Rufani, Stella Mugasha kudaiwa kuandika barua akieleza uamuzi wa kumwongezea muda ni uvunjaji wa Katiba na kutozingatia misingi ya sheria.


Hata hivyo, barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na Jaji Stella isiyokuwa na tarehe kwenda kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi waandamizi wa Serikali walisema hawajaipata.

Wengine waliotumiwa nakala ya barua hiyo yenye kurasa kumi ambayo jana ilikuwa ikisambaa mitandoni ni Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, Jaji wa Rufani, Augustine Mwarija, Jaji Kiongozi, Mustapger Siyani, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Eliezer Feleshi na Katibu Mkuu Kiongozi.

Gazeti hili lilimtafuta Jaji Stella kupitia simu yake ya mkononi kujua usahihi wa barua hiyo akasema, “aaah! Sina barua kwenye gazeti.”

Alipoelezwa barua hiyo inasambaa mitandaoni ambayo ameituma kwa mtendaji mkuu wa mahakama alijibu, “hiyo kwenye gazeti hainihusu, mimi nimeipeleka kwa wahusika.”

Profesa Elisante alipoulizwa na Mwananchi kwa ujumbe mfupi wa maneno, kama ameshaipokea barua hiyo iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na maoni yake kuhusu barua hiyo alijibu hana maoni.

“Sina comments. Nitumie pia hiyo link kwenye mitandao,” alijibu Profesa Elisante kwa ujumbe mfupi.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Feleshi ambaye mwandishi wa barua hiyo ameielekeza nakala kwake, alipoulizwa kwa ujumbe mfupi kama alikuwa ameshaipokea kwanza aliuliza Mwananchi ni wapi limeiona barua hiyo

“Niko kwenye kikao. Wewe umeiona wapi,” aliuliza Dk Feleshi.

Lakini alipoelezwa kuwa Mwananchi limeiona kwa mawakili kadhaa wa kujitegemea kupitia mtandao wa WhatsApp, alijibu kwa kwa ujumbe mfupi, “sijapokea.”

Hatua hiyo ya Jaji Stella inakuja siku chache tangu gazeti hili liripoti juu ya nani kumrithi Profesa Juma ambaye muda wake wa kuhudumu ulikoma Julai 15 mwaka huu.

Profesa Juma alizaliwa Juni 15, 1958, Musoma mkoani Mara na Juni 15, 2023 alitimiza miaka 65.

Aliteuliwa katika wadhifa huo Septemba 10, 2017 na aliyekuwa Rais wa wakati huo, John Magufuli, mara baada ya Jaji Mkuu, Mohamed Chande kustaafu.

Msingi wa Jaji Stella kudaiwa kupinga nyongeza ya muda wa Profesa Juma unaakisi Ibara ya 118 (2) ya Katiba ya Tanzania inayoweka ukomo kuwa Jaji mkuu kustaafu atakapotimiza umri wa miaka 65.

Katika barua hiyo, Jaji Stella anadaiwa kuandika kuwa, “Jaji mkuu amenielekeza kukufikishia salamu, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Jaji Kiongozi kwamba, Rais Samia Suluhu Hassan amemuongezea muda (Profesa Juma) aendelee kuhudumu katika nafasi ya Jaji mkuu baada ya muda wake wa kustaafu ambao ni Julai 15, 2023.

“Jaji mkuu anakushukuru sana wewe Jaji wa Mahakama ya rufani na Jaji Kiongozi kwa ushirikiano mkubwa sana mliompatia kwa muda wote ambao amekuwa katika kutumikia Mahakama.”

Barua hiyo iliyoandikwa kwa mtendaji mkuu wa Mahakama, Profesa Ole Gabriel iliendelea kueleza, “aidha, Jaji mkuu anaomba mumfikishie salamu …kwa majaji wa Mahakama ya Rufani na wale wa Mahakama Kuu…”

Jaji Stella katika barua yake hiyo akinukuu andiko lililoonyesha Profesa Juma kuendelea na kibarua chake, alibainisha kwamba andiko hilo halionyeshi muda alioongezewa kiongozi huyo, akisisitiza hata kuongeza muda ni kuvunja sheria.

“Sina ugomvi wowote na Profesa Juma na nimefanya naye kazi kwa uaminifu kwa zaidi ya miaka 10. Kwa kiapo changu cha kazi ya Jaji ninawajibika kulinda na kutetea Katiba ya nchi. Vilevile, kwa mujibu wa Ibara ya 26 (2) ya Katiba, pia mimi kama raia nina wajibu na haki ya kutetea na kuhakikisha Katiba ya Nchi inalindwa ipasavyo,” aliandika.

Hata hivyo, Jaji Stella akinukuu katiba, aliweka bayana Ibara ya 118 (2) inajitegemea na kusimama yenyewe kwenye ukomo uliotajwa hivyo umri wa kustaafu kwa Jaji wa Rufani uliotajwa ndani ya Ibara ya 120 (1) ya Katiba ndicho kitu pekee cha kuangaliwa ili kufahamu umri wa kustaafu Jaji Mkuu ambao ni miaka 65 tu.

Kutokana na Ibara hiyo, nyongeza ya muda kwa Jaji wa Rufani haimhusu Jaji Mkuu asilani.

“Ukomo wa umri wa miaka 65 uliwekwa kwa makusudi ili kuondoa dhana potofu ya uchifu au usultani katika nafasi hiyo. Hivyo kwa kuwa Bunge lilimaanisha kilichomo katika Ibara ya 118 (2) ya Katiba na si vinginevyo, kitendo cha kumuongezea muda Profesa Juma baada ya miaka 65 ni sawa na kuliwekea Bunge mdomoni maneno ambayo halikusema wala kukusudia na ni uvunjaji wa Katiba,” alibainisha.

Jaji Stella alirejea mwaka 1995 na 2000, ambapo Ibara ya II8 haikuwa na kipengele kinachoweka umri wa miaka 65 kuwa ni ukomo wa Jaji Mkuu kuhudumu katika nafasi hiyo.

“Mwaka 2005 kupitia Sheria ya Mabadiliko ya kumi na nne katika Katiba, Sheria Na. 1 ya mwaka 2005, Ibara yote ya 118 ilifutwa na kutungwa upya. Mabadiliko hayo yaliridhiwa na Rais April 6, 2005.

Ibara ya 118 (2) inaeleza, Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuwa Jaji wa Rufani na atakuwa ndiye Kiongozi wa Mahakama ya Rufani na pia Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 116 ya Katiba na atashika madaraka mpaka atakapotimiza umri wa kustaafu kama Jaji wa Rufani, isipokuwa kama: (a) atajiuzulu; au (b) kiti chake kitakuwa wazi kutokana na maradhi au kifo, au (c) atavuliwa wadhifa wa Jaji Mkuu na Rais,’’ aliandika.

Jaji Stella akiakisi kilichotokea sasa alielezea kuwahi kuwepo kwa mjadala ndani ya Mahakama kuhusu uhalali wa Majaji waliotimiza umri wa kustaafu na kuongezewa muda wa kuhudumu ikiwa ni pamoja na Jaji Mkuu.

Wakati wa mjadala huo, Jaji Stella alieleza kuwa Jaji Mwarija alikuwa ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa na Mtendaji wa Mahakama kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Novemba, 2006.

MWANANCHI.
 

Similar threads

Soon as I can I want to learn a new language. Mimi ni mwepesi kujifunza na mambo mengi napenda kujifunza mwenyewe (self taught). I want to ask you guys how long did it take to learn one language? I took short time to learn PHP na JS ila kwenye MYSQL nina week kadhaaa bado sijafika mbali...
Replies
14
Views
344
Dar es Salaam. Sakata la Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma kuongezewa muda wa utumishi wa wadhifa huo sasa limetinga mahakamani baada ya wakili mmoja kufungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu Masjala Kuu, akipinga hatua hiyo. Wakili huyo, Humphrey Malenga amefungua kesi hiyo siku chache baada ya...
Replies
1
Views
545
Dar es Salaam. Sakata la Jaji Mkuu, Profesa Ibrahimu Juma kuendelea kusalia kwenye nafasi hiyo limechukua sura mpya baada ya Wakili wa kujitegemea, Humphrey Simon Malenga kufungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu Masjala Kuu, Dar es Salaam kupinga kiongozi huyo kuongezewa muda wa utumishi huo...
Replies
2
Views
574
Top Bottom