Mwanafunzi Ester aendelea na vipimo Meta Mbeya

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Gily

KF Founder & Dragon IGM
Staff member
Jun 4, 2023
7,020
22,618
113
Mbeya. Siku moja baada ya mwanafunzi, Esther Noah kupatikana akiwa hai, anaendelea na vipimo kwenye Hospitali ya Rufaa kitengo cha Wazazi Meta jijini Mbeya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mwanafunzi huyo (18) wa kidato cha tano katika shule ya sekondari Panda Hill alidaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Mei 18 mwaka huu na jana Juni 23 alipatikana akiwa hai.

Esther alikutwa mtaa wa Ifisi mji mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya akiwa kwenye nyumba ya mfanyabiashara wa mkaa aitwaye Azurath Mohamed ambaye alieleza kukabidhiwa na mteja wake aliyejulikana kwa jina la Baba Jose.

Akizungumza na Mwananchi Digital, leo Jumamosi June 24, 2023, mama mdogo na mlezi wa mwanafunzi huyo, Happy Yobi amesema kwa sasa wapo hospitali ya Meta kwa matibabu zaidi baada ya kufika nyumbani usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Juni 24.

Amesema hali yake si mbaya akibainisha kuwa ishu ya usalama ni ya kawaida kwani nyumbani kwao mtaa wa Forest nyumba waliyopo ina kila kitu ndani hivyo hawana wasiwasi sana.

“Tunaishi naye kwa tahadhari na umakini japokuwa nyumba ina kila kitu ndani hawezi kupotea, tulifika usiku na leo tupo hospitali hapa Meta kwa matibabu zaidi,”

“Ni mapema sana kuzungumza naye kila kitu, tumeamua asiongee chochote apumzike kwanza kwa sababu vyombo vya dora vilimuhoji kila kitu hivyo tuwaachie wao, mimi na mume wangu ndio tulimlea akiwa na miaka miwili hadi sasa,” amesema Happy.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo, Zephania James amesema wanaendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi akieleza kuwa mwanafunzi huyo alikuwa mpenda michezo na hakuwa na tabia mbaya zaidi.

“Alikuwa mtu wa kawaida anapenda kujichanganya na wenzake na alipendelea zaidi michezo, nidhamu yake ilikuwa nzuri na sijawahi kupata taarifa mbaya kutoka kwake,” amesema James.

MWANANCHI
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
Staff member
Jun 4, 2023
7,020
22,618
113
@Gily tunaomba utushushie nondo kinaendelea nini kwa binti huyu
UPDATES:
Mwanafunzi aliyepotea Mbeya apatikana kwa muuza mkaa - Ijumaa, Juni 23, 2023

Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa kidato cha tano, wa shule ya Sekondari ya Panda Hill aliyetoweka shuleni Mei 18, 2023, Esther Mwanyilu amepatikana akiwa hai katika chumba cha muuza mkaa eneo la Ifisi mji mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 23, mkoani hapo, Mkuu wa Mkoa huo, Juma Homera amesema chumba hicho kinamilikiwa na Azurati Mohamed ambapo baada ya mahojiano alidai binti huyo alikabidhiwa na mmoja wa mteja wake.

“Amepatikana akiwa hai maeneo ya Isisi mji mdogo wa Mbalizi akiwa katika chumba cha mwanamke mmoja ambaye ni muuza mkaa kwenye nyumba ya kupanga ya Azurati Mohamed, alikabidhiwa na mtu mmoja ambaye ni mteja wake wa mkaa,”amesema

Amesema mteja huyo anajulikana kwa jina la Baba Geofrey na kwamba baada ya makabidhiano hayo alisema amemwaribu mwanafunzi huyo hivyo akae naye siku mbili akimtafutia sehemu ya kumpangia.

Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoani humo kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi lilipomuuliza binti huyo iwapo anahitaji kwenda shule, alidai yupo tayari isipokuwa apelekwe shule nyingine.

“Nikipelekwa shule nyingine nitakuwa tayari kuingia darasani kusoma ila siyo shule niliyokuwa nasoma na naomba walimu wabadilike” amesema

Hata hivyo mkuu wa mkoa huo ameahidi kumpeleka kwenye shule yeyote aendelee kusoma.

Homela ameeleza kuwa katika vipimo vya awali walivyofanya havijaonesha kama anaujauzito, na wanatarajia kufanya vipimo vingine.

“Ikibainika kwamba anaujauzito itatakiwa abaki nyumbani hadi ajifungue kisha arudi shuleni kuendelea na masomo,”amesema

Homela amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchungu ikiwamo kumtafuta Baba Geofrey.

Mwanafunzi huyo amepatikana ikiwa ni siku moja tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa maagizo kwa mkuu wa mkoa huo kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

GAZETI LA MWANANCHI.
 

Urban Edmund

New member
Platinum Villager
Jun 26, 2023
636
1,320
0
Alishapatikanaga kweli ila baada ya kupatikana mimba alipimwa ikasoma nusu kwa nusu "in Homera voice"
 

Similar threads

Mary Katherine Schmitz alizaliwa mwaka wa 1962 huko jimboni California, mama yake ni Mary E, mwanakemia, na baba yake ni John G. Schmitz, mwanasiasa. Mary Katherine Schmitz alijulikana kama Mary Kay kwa familia yake. Mara baada ya kuzaliwa alipewa jina la utani “Mary Kay.” Pia baba yake alimpa...
Replies
24
Views
343
Top Bottom