Nostalgia....

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

mshamba_mkuu

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
1,563
Reaction score
4,525
Points
0
Umeshawahi kukumbuka kitu, kwenda mahali, kuona kitu, kugusa kitu, kunusa kitu au hata kuambiwa kitu, halafu ukakumbuka kitu flani cha zamani kwenye maisha yako, ukapata hisia flani ambayo ni kama mchanganyiko wa furaha, huzuni na shauku?? Hii hisia inaitwa nostalgia



Nostalgia ni hisia ya raha na wakati mwingine huzuni kidogo wakati huo huo unapofikiria juu ya mambo yaliyotokea zamani.... Mimi nimejikuta napenda sana kupata hii hisia, kukumbukia vitu vya zamani inanipa amani flani moyoni. Vitu vinavyonipa nostalgia ni kama;



-nikiwa maeneo ya shule nilizosoma hapo awali



-filamu au miziki niliyoipenda sana zamani au hata nikiwa mtoto kabisa



-watu ambao ulikua nao karibu zamani ila mkapotezana afu mkakutana sasa



-picha mbalimbali ulizopiga kwenye matukio ya zamani



-vyakula na vinywaji ambavyo unakua hujavitumia kwa mda mrefu sana



-mahali flani maalum ambapo pana umuhimu kwako mfano; nyumbani kwa bibi, kaburi la mtu wako wa karibu



-na vitu vingine mbalimbali kama vitabu, simu ulizotumia zamani.... mfano; kuna kitabu cha hadithi nilikua nakipenda sana nikiwa mdogo nikaja kukipata tena hivi karibuni nilipokifungua nikawa napata kumbukumbu nyingi za kipindi hicho, kumbukumbu ambazo hata nilikua sijui kama bado ninazo



ndio maana kukusanya kumbukumbu za matukio mbalimbali kwenye hatua mbalimbali za maisha yako inaweza ikawa na muhimu, ile hisia unayoipata wakati unarudisha matukio nyuma kwenye akili yako inakuonyesha mapito mbalimbali uliyopitia mpaka kufikia hapo ulipo....



Je na wewe unapata nostalgia?? vitu gani hasa vinakukumbusha mbali??
 
Last edited by a moderator:

mshamba_mkuu

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
1,563
Reaction score
4,525
Points
0
em tiririka kwa mapana
nilivokua mdogo nilikua naipenda sana movie ya shrek.... niliirudia mara nyingi nyingi sana.... sasa intro yake ndo inaanza na hiyo nyimbo, niliikariri yote

wanasema mtu anaweza kuhusisha nyimbo na kitu fulani kwenye maisha yake(anchoring) sasa hiyo nyimbo nikiiskia nakumbuka enzi izo bado mdogo, sina stress
 

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom