Unyanyasaji kijinsia kumpiga Mwanamke

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,627
Reaction score
26,448
Points
113
Ukatili haujali tabaka
Je. wanawake na wasichana kutoka katika familia zenye hali nzuri ya kiuchumi pia huathiriwa na ukatili wa kijinsia? Watu wengi hudhani kuwa wanawake na wasichana kutoka katika familia zenye ukwasi hawana matatizo na wana uhuru sana. La hasha!

Kwa uzoefu wa TAMWA, kundi hili pia linakutana na ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na ukatili unaotokea nyumbani, kazini, mitandaoni na hata barabarani au mitaani. Tushiriki kupinga ukatili wa kijinsia kwani hauchagui tabaka la mtu.
1689955118890.png

Kipigo kwa mwanamke
Kumpiga mwanamke ni unyanyasaji na
udhalilishaji. Kipigo husababisha chuki, woga, visasi na uhusiano mbaya ndani ya familia. Mwanaume wa kweli hawezi kumpiga mwanamke. Mwanamke jasiri hutoa taarifa kuhusu vipigo.

Utafiti uliofanywa na TDHS unaonyesha kuwa kila wanawake 10 wanawake 3 wamewahi kufanyiwa vitendo vya ukatili. Na kwamba wanawake wa 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15

Kumpiga mwanamke ni ukatili wa kijinsia.
Kipigo huondoa upendo, furaha, ushirikiano
mzuri katika familia, pia husababisha chuki,
visasi kwa watoto na athari za kisaikolojia
katika familia. Mazungumzo na majadiliano ni njia bora ya kutatua migogoro
1689955173403.png
1689955203400.png

1689955348932.png
 
Imetokea mtaani kwetu mwanamke kachelewa kurudi on time kutoka kazini. Mwanaume akaanza kumkaripia katoka kulala na mwanaume. Akamvua nguo na kumdhalilisha sana mbele za wapangaji wenzake kuwa kalowa. Sungusungu waliitwa jamaa akachezea kipigo cha mbwa mwitu na kesi iko mahakamani yupo rumande

Kuna haja ya wanaume wapewe elimu kuhusu UKE maana wengine hawajui unaweza kulowa wenyewe.
 
mi naona tatizo liko kiakili kabisa,

mtu kama anamchukulia mwanamke kama chombo huyu ana uwezekano mkubwa wa kupiga wanawake....

na wapo wengi sana, ile ishu ya mtu wa kenya kumuacha mke wake anywe sumu wanaume wengi waliitetea
 
Kuwe na mifumo imara ya kutetea sio tu wanawake hata wanaume wanaopitia unyanyasaji wa kijinsia
 
Similar threads

Swahili Version: Wanaume hawa walikataa kumpisha mwanamke kukaa. Walidai kuwa wamechoka na mwanamke anaweza kusimama. Pia walisema mwanamke anaweza kufanya kile ambacho mwanaume anaweza kufanya, wakimanisha anaweza kusimama. Kwa hiyo hawakuona inafaa kumpa kiti. Mmoja wa wanaume alisema sisi...
Replies
12
Views
196
Say No to domestic violence and Spousal Abuse (both Physical and Psychological!) Ukatili wa kijinsia ni nini? Ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote ambacho kinaweza kusababisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii, ikiwa ni pamoja na kutishiwa maisha, kunyimwa...
Replies
14
Views
200

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top