Aise vijijini watu ni wambeya sana mjini wakasome

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Watoto wa kidugala

Well-known member
Platinum Villager
Joined
Jul 8, 2023
Messages
195
Reaction score
704
Points
93
Afya ni afya hakika wote tutakufa .
Habari wanakijii , leo naongea na nyie born town aisee ukweli maisha ya kijijni yanataka sana moyo maana wambeya ni wengi kuliko wema .

Naishi kijijini huku nimejenga , nina mambo yangu ya kizee kizee na ya kimaisha nayaendeleza , siwazi kuhama kijiji na wala siwazi kurudi kwetu jijini .

Hivyo msinishauri ila sasa maisha ya wanakijiji yanaboa sana yaani kuna mtu anaijua ratiba yako ya kutoka na kuingia mpaka namna ya muda mnaowasha taa za uhani na kuzima 😀

Nasema hivi maana nimekaa nikawaza baada ya wiki hili lote kuwa bize ndani ya nyumba napambana na mafundi na watu wengine wa chemistry yangu ndani ya nyumba , sijatoka nipo nafanya mambo yangu ndani kwa ndani , sasa leo shughuli zimeisha nikasema wacha nitoke kidogo .

Unajua hapa kijijini kwetu mambo ya kujichanganya na wanakijiji niliacha baada ya kuona mazoea nao yanaboa niulizie kwanini ?

Yaani utashangaa unakutana na mtu kisa ushakuwa na mazoea naye basi kama haupo atakuelezea mpaka yasiyotakiwa .

Hivyo nikaamua kuweka wa mbuzi , mimi nikitoka ni mwendo wa salamu tu , misiba nikienda ni mimi na diwani siunajua tena ili wanakijiji wakuheshimu kaa karibu na diwani tu .

Sasa diwani mwenyewe ananiita mshauri wake wa kijiji 😀

Basi bwana , leo nikawa natoka ile tu nafungua geti kuna jirani akanipiga mkono usijiulize nilikuwa na usafiri au nini , mwenzenu nina mikokoteni yangu japo naupenda mmoja wa urithi huo natamba nao hapa kijijini maana wa kitambo na unahimili harakati za hapa

Sasa ndugu jirani eti ananiuliza ww mbona umepotea sana ? Haupatikani siku hizi nikamuuliza sipatikani umekuja kwangu ? Je umenipigia basi ? Eti oooh hapana najua saa mbili unatokaga hapa ndani na unarudi mida ya saa saba , alafu ukitoka muda huo ni saa kumi na moja 🤔 , nikajikuta namjibu nilikuwepo uwe na asubuhi njema .

Sasa nikarecall back hawa kuna kipindi hapa kati niliumwa , taarifa zangu zikasambaa maana nilichukuliwa na zile gari za milio barabarani , huku nyuma nasikia wakawa wanasema yaani UKIMWI wa sasa hivi unashtukiza mpaka ni hatari 😀

Kwahiyo mimi walimaanisha nina ngoma na pia umenishtukiza kuanza kuumwa , haya niliambiwa na wanangu ninaowalea baada ya kuwa wanambiwa kibabu chenu kiko hoi na ngoma kimepelekwa hatujui kama kitarudi hivyo jiandaeni kurudi majumbani kwenu na magonjwa yenu .

Imagine , unamuambia mtoto ambaye ni muathirika wa hili gonjwa maneno magumu kama haya .

Sasa nakukanya wewe born town ukija kijijini kuwa na moyo mpana watu hawana kazi huku , wakitoka shamba mida ya saa saba basi ni muda wa kumjadili yeyote aliyeletwa mezani .

Sasa usijihisi vibaya kuwa na amani tumesemwa toka tunazaliwa utasemwa mpaka unakufa , wewe ni wewe ishi kama wewe .
Msiseme mzee mbona kinyonge , hawa nataka niwakate vidomo kabisa nitamchukua wife siku moja namuambia atinge uniform zake nitembee naye sehemu zote za makusanyiko hapa kijijini ili hata michepuko na wambeya wajue nikijua wanayonisema wife atawachenjia .

Asanteni .
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Ukiwa umekulia Ilala, Upanga na Kariakoo kuishi pande zenye baridi ni ngumu sana. Nawaza tu kwa baridi la huko kama usingekuwa umeishi Urusi usingeweza. Ila hata zile mbinu za urusi za kuguguda Vodka unazitumia huko.

Nina ekari zaidi ya 20 huko pwani kwa Mr Born Town natumai nitafutahia uzee wangu inshallah kama nitakuwepo. Hata kama sitakuwepo hao waliopo wataufurahia pia

Mjini kwa sasa siwezi kuhama kwa sababu shughuli zangu ziko huku kwa asilimia kubwa. Ila tu ukiishi mjini raha yake uwe kwako. Namshukuru sana Mungu siwazii kodi ya nyumba.

Kufuatuliana popote pale hata uwe masaki Sema tu kufuatiliana kunatofautiana. Masaki unakuta jirani anafuatilia kama umenunua gari mpya. Uswahilini ukipita na kuku hata jirani hakusalimii na hata ukimsalimia haitiki😬
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Nilienda kijijini 2020 hivi nilipita na videmu sio poa, ila huko ndipo nilipompata milavu bad news ni mjinga sana saivi naganga yajayo
Mdogo wangu kapime mapema uishi kwa matumaini.
Tuweke kindi la HIV humu ndani mshamba_mkuu sidhani kama atamalizq chuo salama huko Mbeya
 

Hakimu

Immortal Village Hero
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 3, 2023
Messages
2,711
Reaction score
6,226
Points
113
Mdogo wangu kapime mapema uishi kwa matumaini.
Tuweke kindi la HIV humu ndani mshamba_mkuu sidhani kama atamalizq chuo salama huko Mbeya
Hahha wanaojitunza hua ndio wanabaati mbaya wakigusa wapo connected
 

Similar threads

Afya ni Afya wote tutakufa . Wanakijiji habari zenu , Mimi najua waliowengi kwa wanakijiji mmesafiri vijijini na mijini , leo mwenzenu naikumbusha tena serikali kuwa hawa watu wa afya hasa kwenye hizi zahanati ni wazi kuwa wengi wao ni watabibu . Nisichoweza kupinga ni kuwa kwenye ulimwengu wa...
Replies
16
Views
266
Wakuu kwema? Binafsi yangu kuwaeleza watu kuhusu mipango yangu naona sio sawa maana watu niwajuaji sana wanaweza wakaanza kukushauri negatively au kukukatisha tama...
Replies
13
Views
762
Juzi nlikua naelekea Namanga kwenye shughuli za hapa na pale, nlipanda noah maana ndio usafiri wa huku. Sasa kilicho nishangaza nikwamba jamaa(dereva) kwanzia tumetoka Arusha hadi tunafika Namanga alikua ameweka wimbo mmoja yani hakuubadilisha.. mimi nmezoea nkipandaga nakuta ninyimbo za...
Replies
5
Views
485
Nakusalimu mwanaKF, ninafurahi kwakua umeamua kusoma bandiko hili... karibu sana, najua utapata kitu... Luka 17:11-14 Yesu alipokuwa njiani akienda Yerusalemu, alipitia mpakani mwa Samaria na Galilaya. Alipokuwa akiingia kwenye kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma wakakutana naye...
Replies
3
Views
257
Nigudi ee? Niko gudi piaa. Umeshawai kujiuliza familia ya baba mama na watoto inaweza kuishije ndani ya chumba kimoja? Baba na mama huwa wanafanyaje mambo ya faragha katika chumba kimoja na watoto hata kama wamelala? Hapo nimezungumza tu kuhusu family members bado vyombo, kitanda, makochi...
Replies
14
Views
414

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom