Biashara ndogo za kufanya bila kuwa na fremu

The great manenge

New member
Platinum Villager
Joined
Jul 8, 2023
Messages
1,320
Reaction score
2,995
Points
0
Habari Wanakijiji
Kumekuwa na malalamiko mengi kwa vijana kuwa pesa ya kukodi fremu ni kubwa sana,na haswa hapa mjini tatizo hilo limekuwa changamoto ambayo kuiepuka uwezi na hawa madalali sasa wanatumia huhitaji wa fremu kuwa ajili kwao,basi katika kuangalia fursa unazoweza kuzifanya bila kuwa na fremu nimeona niwalete nanyi mpate kuzijua sasa. Fursa zenyewe hizi hapa:

1.UDALALI WA VITU,VYUMBA ,VIWANJA NYUMBA NA MASHAMBA
Hii anaweza fanya mtu yeyote,cha msingi uweke tu matangazo kwenye mitandao ya jamii kama Instagram,fb n.k
Pia unaweza bandika mabango kwenye kuta za nyumba,nguzo za umeme ,unaenda kwa wenye nyumba za kupanga unawaelekeza kuwa utawatafutia wapangaji,basi kili chobaki ni kupiga pesa zako tu.

2.KUTOA HUDUMA MBALIMBALI.
Hii unaweza kuifanya nyumbani kwako,ila ni kwa watoto wachache,kwa kuwa maisha yamekuwa ni magumu na hakuna mda wa kukaa bure basi inapelekea watu wengi wa mjini kuwa bize na kazi siku nzima,basi wanatafuta mtu wa kuwaangalia watoto wao kipindi wa kiwa kazini,hii fursa ni kubwa sana cha msingi uwe mwaminifu kwa watu na jamii inayokuzunguka.

3.BIASHARA YA KUOKOTA NA KUUZA VITU CHAKAVU,CHUMA CHAKAVU NA PLASTIC/MACHUPA.
Sasa hivi majengo mengi yanabomolewa kila kukicha,machuma kibao yamejaa mtaani na chupa za maji zilizotupa ovyo,basi unaweza kuokata kisha ukatafuta wateja wa hivyo vitu,kuna watu siku hizi wananunua magodoro mabovu,oil chafu kwa mafundi pikipiki hapo ni wewe tu kuacha aibu na kuchangamkia hii fursa.

4.KUUZA MBOLEA NA MIFUPA YA KUKU NA NGOMBE.
Unaanza kutafuta oda kwa watu wenye majumba wanahitaji mbolea kwa ajili ya kuotesha maua na mboga mbogana wafugaji wa kuku,basi kazi yako utakuwa kuokota mbolea na mifupa kutoka machinjoni,na kwenha kuwauzia.

5.BIASHARA YA KUUZA MABAKI YA CHAKULA KUTOKA MAHOTELINI.
Tafuta watu wafugaji wa paka,mbwa na nguruwe unakusanya mabaki yote ya chakula kutoka kwenye mahoteli,alafu unaenda kuwauzia wafugaji wa wanyama.

6.KUTENGENEZA MALIGHAFI NA MAPAMBO MBALIMBALI.
hii unaweza kujifunza kwa watu wenye ujuzi au kwenye you tube kule wanafundisha jinsi ya kutengeneza vitu mbalimbali mtandaoni.

........HITIMISHO..........
 

Similar threads

Mapendekezo ya wafanyabiashara Kasi ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Wafanyabiashara kwa sababu kuna mambo mengi mazuri yanayoweza kustawisha biashara na sekta binafsi. Serikali inatakiwa kutochoka kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara, kwa sababu wao ndio wanajua shida...
Replies
1
Views
191
Mambo matatu muhimu wakati wa kuanzisha biashara 1. Hata kama unayo pesa ya kuanza biashara kubwa. Anza kidogo kisha ikuze kutokana na mzunguko unavoenda. 2. Kama ikiwezekana usifungue biashara mbali sana na eneo lako la umahiri. 3. Anza na mtindo mmoja wa biashara, na katika aina moja ya...
Replies
15
Views
418
Una wazo gani la biashara? Wengi hupenda kufanya biashara ila wanakwama kwa kukosa mitaji. Hebu eleza hapa unataka kufanya biashara gani na unategemea itakuwa ya mtaji wa kiasi gani. .
Replies
30
Views
690
Habari! Leo nitawaeleza mchanganuo wa biashara hii ya chips biashara ambayo imepamba moto maeneo ya mijini hasa dar es salaam Kwanza biashara hii huathiriwa na vitu vingi kama zilivyo biashara nyingine Nakumbuka mitaa flani nilikuwa nikiishi kulikuwa na huyo mama wa kichaga alikuwa anapata...
Replies
6
Views
274
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema haitafunga maduka wala biashara ya mfanyabiashara yeyote kwa kuwa huo ndio utaratibu waliojiwekea. “Kwa sasa TRA haihusiki kufunga biashara au maduka ya mfanyabiashara yeyote na ikitokea mtu amejitambulisha kuwa ni mtumishi anayetoka katika ofisi yetu...
Replies
3
Views
701
Back
Top