Bodaboda, baiskeli hatari kwa nguvu za kiume

Hakimu

Immortal Village Hero
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 3, 2023
Messages
2,714
Reaction score
6,233
Points
113
Kazi ya kuendesha baiskeli za kubeba abiria pamoja na baiskeli zinazopatikana kwenye vituo vya mazoezi (gym) vimebainika kuwa chanzo cha kupunguza uwezo wa wanaume wanaposhiriki tendo la ndoa.

Hayo yamebainika kupitia utafiti uliofanywa hivi karibuni na jopo la wataalam wa afya ya uzazi likiongozwa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta, Wamalwa nchini Kenya.

Matokeo ya utafiti huo uliowahusisha waendesha baiskeli (bodaboda) 115 wenye umri kati ya miaka 18 na 40, katika eneo la Bungoma, Mashariki mwa Kenya, ulibaini kuwa asilimia 35.9 walikuwa na matatizo ya uwezo mdogo wa kushiriki tendo la ndoa ipasavyo, kwakuwa wameathiriwa misuli ya uume.

Vijana hao walipimwa na wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Taifa ya Kenyatta wakishirikiana na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta, ambapo majibu yalionesha kuwa asilimia 39.5 walikuwa na tatizo la kusisimua misuli ya uume.

Utafiti huo ulionesha kuwa vijana hao waliathirika kutokana na kutumia nguvu nyingi katika kuendesha baiskeli na kwamba walioendesha baiskeli kwa muda wa saa 60 au zaidi kwa wiki ndio waliathirika zaidi.

Wamalwa alitahadharisha pia kuwa vijana wengi walio kwenye vituo vya kufanyia mazoezi (gym) wakiendesha baiskeli zisizokuwa na vizuizi maalum dhidi ya sehemu za uume, wako kwenye hatari ya kukutwa na tatizo la kutokuwa na uwezo wa kushiriki ipasavyo tendo la ndoa.

Aidha, matokeo ya utafiti huo pia yanaendana na matoekeo ya tafiti zilizofanywa na watafiti wengine sita wa Chuo Kikuu cha Moi zilizowahusisha vijana 131 wa mjini Eldoret, wenye umri kati ya miaka 18 na 56. Kati ya waliopimwa, asilimia 76 walibainika kuwa na matatizo ya kutosisimua ipasavyo misuli ya uume
 

Similar threads

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imebainisha kuwa taarifa iliyotolewa awali na Afisa Mkuu wa Usimamizi wa Kodi wa Mamlaka hiyo kuwa bodaboda wataanza kutozwa kodi sio rasmi Afisa huyo, Hamad Mterry alieleza kuwa Kodi mpya za Pikipiki za Matairi Mawili (Bodaboda) itakuwa Tsh. 65,000 na Bajaji...
Replies
4
Views
212
" Je unafahamu kuwa nchini Tanzania kuna mji mkongwe ambao usafiri wake mkuu ni baiskeli? Kwa muda wa miongo mitano sasa, wakazi wake wameendelea kutegemea zaidi usafiri huo ambao unatambua baisikeli za uchukuzi wa umma kwa jina 'daladala'. Mwandishi wa BBC @lasteck2023 ametembelea mji huo wa...
Replies
6
Views
205
Kwa mtu anayejua mpira,ndo ataelewa ninachosema, kibabage anaspeed, azizi k anaspeed, skudu anaspeed, msonda na mzize wana aspeed yani kuna timu zitapigwa goli nyingi. Yanga inayokuja itakuwa ya speed sana makabi naye anaspeed aisee
Replies
11
Views
173
Baadhi ya watoto hawakujua kwamba maisha yao yalikuwa "hatarini" katika mji wa Suffolk nchini Uingereza kutokana na kuwepo kwa 'hemlock' kwenye njia yao ya kawaida ya kwenda shuleni, mmea wenye sumu ambao unaweza kumuua mtu ikiwa ataumeza. Hata hivyo, hemlock sio mmea pekee unaohatarisha maisha...
Replies
10
Views
174
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya watu milioni moja duniani kote wanaambukizwa magonjwa ya zinaa kila siku. Magonjwa kutosikia matibabu ni tatizo kubwa la magonjwa ya zinaa (STDs) au (maambukizi ya zinaa) na ni kikwazo kikubwa katika kudhibiti magonjwa ya zinaa, WHO ilisema...
Replies
10
Views
254

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top