Faida 7 za kula ndizi

Hakimu

Immortal Village Hero
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 3, 2023
Messages
2,714
Reaction score
6,233
Points
113
Ndizi ni mojawapo ya tunda linalopendwa zaidi duniani, likiwa limesheheni vitamini na madini.
Ziko faida kadhaa za kiafya za ndizi ambazo ni muhimu kwa mlaji kula tunda hili. Faida hizi ni pamoja na:
1: Inasawazisha maji ya mwili "homoni": ndizi ina kiasi kikubwa cha potasiamu na vitamini B6 vitu vinavyokuza uzalishaji wa kiasi cha maji kinachohitajika.
Kulingana na wataalamu wa masuala ya lishe, ndizi zina madini ya potassium kwa wingi, ambayo mwili wa binadamu unahitaji, kwa mujibu wa Catherine Collins, kutoka hospitali ya St George mjini London.

1.NGUVU

Ndizi zina aina 3 za sukari asilia ambazo ni fructose, glucose na sucrose ambazo huusaidia mwili kupata nishati ya kutosha na kutengeneza nguvu.

2.KUIMARISHA MIFUPA

Ndizi huimarisha mifupa. Ndizi hurahisisha ufyonzaji wa kalsiamu, ambayo ni nzuri kwa mifupa. Kwa hivyo hufanya mifupa kuwa na afya na nguvu.
Ndizi zina, potasiamu pia na madini mbalimbali kama vitamini B6, C, magnesiamu, shaba, protini na mafuta.

3.KUPUNGUZA SUKARI KWENYE DAMU

Ndizi ambazo hazijaiva huwa na vitu vinavyojulikana kama "Pectin" na "resistenat starch" ambavyo vyote vinapunguza sukari kwenye damu, hivyo kula ndizi kabla au baada ya kula kunapendekezwa, lakini watu wenye kisukari wanapaswa kuepuka ndizi ambazo zimeiva sana.

4.KUSAIDIA MMENG'ENYO WA CHAKULA

Ndizi zinnaboresha mmenge'nyo wa chakula na zina "Fiber" za kutosha, ambazo huzuia mtu kuvimbiwa na ni nzuri kwa mmeng'engo.

5.KUIMARISHA AFYA YA UBONGO NA INI

Ndizi zina viambata vikali vya kuondoa sumu mwilini, kama vile "Dopamine" na "Catechins", na ni nzuri kwa afya ya ubongo na ini.

6.KUDHIBITI UNENE ULIOPITILIZA

Ukila ndizi zinakufanya ujisikie kushiba haraka, zinajaza tumbo haraka, hivyo kwa watu wanene ambao hawawezi kudhibiti hamu yao ya kula wanashauriwa kula ndizi mbichi.

7.NZURI KWA FIGO

Madini ya potasiamu ni muhimu kwa utendaji mzuri wa figo na kudhibiti shinikizo la damu.
Ndizi zinaweza kuwa na manufaa hasa kwa kuweka figo zako zikiwa na afya.
Utafiti wa mwaka 2019 uliohusisha zaidi ya watu 5,000 wenye ugonjwa wa figo wa hatua ya awali uligundua kuwa ndizi zina manufaa kwa figo kutokana na maudhui yake ya potasiamu.
Hata hivyo, baadhi ya watu wenye magonjwa ya figo ya kiwango cha juu wanashauriwa tofauti kutokana na ulaji wa ndizi.
 
Kuna faida kubwa ulaji wa ndizi sexually
Unaona bukoba wanawake wanakuwa wana maji mda wote wakati wasiokula ndizi wanakuwa wakavu.

Kwa wanaume ndizi zina faida nyingi ikiwemo kusaidia kudumisha afya ya uzazi wa mwanaume
 

Similar threads

Matunda mengi yana manufaa lakini tango linaonekana kutia fora kwa manufaa katika mwili wa binadamu. Kutokana na faida za Tango, unashauriwa kula tango kila siku, utaona manufaa yake. Kupunguza hatari za saratani Unywaji wa juisi ya tango hupunguza hatari ya saratani kwa wanawake hasa saratani...
Replies
7
Views
238
Tofali la kuchoma Hili ni tofali linalopatikana baada ya kutengeneza tofali la udongo na kulichoma kwa kutumia moto. Tanuri ya matofali unafunikwa kwa gana la udongo nje na chini yake moto inawaka kwa siku 2 au 3. Kutengeneza matoli wa njia hii ina gharama zaidi laini matofali yaliyochomwa...
Replies
0
Views
267
- Kuwa na maisha kamili/ full. - Kufanya maamuzi haraka, haina aja ya kushirikisha mtu.. mfano umepata kazi inayo kutaka kuama mkoa nk - Imarisha kazi au biashara yako bila kizuizi chochote, - Ishi maisha kwa njia yako mwenyewe. - Ishi bila kushughulika na fujo za mtu yeyote. Ongeza zingine
Replies
21
Views
361
Papai ni tunda la kushangaza na lenye afya. Ina 'antioxidants' ambayo hupunguza kuvimba na kupambana na magonjwa na kusaidia mtu kuonekana na umri mdogo. Virutubisho katika papai Kalori, Wanga, Nyuzinyuzi, Protini, Vitamini C, Vitamini A, Vitamini B9, Potasiamu, Kalsiamu na Magnesiamu. Faida...
Replies
5
Views
129
Watu wengi wameendelea kuzungumzia suala la maadili, hasa kwa vijana. Kwa mfano hili wimbi la panyarodi linaloendelea kutajwa kwa vitendo viovu, hii ni miongoni mwa sababu kubwa ya mmomonyoko wa maadili. Inaonekana dhahiri baadhi ya wazazi wameshindwa kutimiza jukumu la malezi ya watoto wao...
Replies
10
Views
177

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top