Faida za tango kwa wanawake

KijijiForums

Official Account
KF Moderator
Joined
Jun 5, 2023
Messages
26
Reaction score
57
Points
0
Matunda mengi yana manufaa lakini tango linaonekana kutia fora kwa manufaa katika mwili wa binadamu. Kutokana na faida za Tango, unashauriwa kula tango kila siku, utaona manufaa yake.

Kupunguza hatari za saratani
Unywaji wa juisi ya tango hupunguza hatari ya saratani kwa wanawake hasa saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya mapafu.

Kupunguza uzito
Tango huzuia magonjwa mengi na hupambana na unene. Tango husaidia sana kupunguza uzito, linaweza kumsaidia mtu kupungua kwa kupata virutubisho vingi muhimu.

Vitamini
Tango lina faida nyingi kiafya, limejaa vitamini K, C, na A, pia zinapatikana nyuzinyuzi na madini ya potasiamu na kalisi (calcium). 95% ya tango ni maji hivyo huulinda mwili kutokana na ukavu.

Hupunguza maumivu kwenye viungo na mifupa
Osteoporosis ni ugonjwa wa mifupa, husababisha mifupa kuwa dhaifu na unaweza kusababisha mifupa membamba kuvunjika hata ikiwa umepinda kidogo. Matango yana madini kama kalsiamu, shaba, magnesiamu na potasiamu ambayo huimarisha afya ya mifupa na matatizo ya mifupa yanayohusiana na umri.

Tango lina nafasi kubwa katika urembo
Huondia uharibifu wa kuzeeka ngozi
Tango lina nafasi kubwa katika urembo wa nywele, ngozi na kucha.
Watafiti wanasema tunda hili huboresha kinga ya mwili.

Matango huimarisha afya ya akili Matango yana flavonoids, ambayo ina nguvu ya kuboresha afya ya akili. Inaboresha kazi ya ubongo na huongeza kumbukumbu. Pia hulinda seli kutokana na uharibifu unaohusiana na kuzeeka.

Hufanya kazi muhimu katika usagaji chakula
Tango lina nyuzinyuzi nyingi na maji, ambavyo vyote ni muhimu kwa usagaji chakula. Vilevile huzuia kiungulia. Kunywa juisi ya tango kila siku husaidia kutibu vidonda vya tumbo.

Ni tiba ya bawasiri
Tango hutuliza bawasiri na huondoa maumivu.

Hufanya kazi muhimu katika usagaji chakula
Tango lina nyuzinyuzi nyingi na maji, ambavyo vyote ni muhimu kwa usagaji chakula. Vilevile huzuia kiungulia. Kunywa juisi ya tango kila siku husaidia kutibu vidonda vya tumbo.

Kupambana na bakteria
Tango lina uwezo wa kupambana na bakteria, fangasi na virusi, na baadhi ya watafiti wanapendekeza watu wanaotumia dawa za VVU kula tango - ili kupunguza virusi kuzaliana.

BBC Swahili
 
Somo zuri ila dada zetu wanayatumia vibaya sana
Wanayatumiaje?
Oya hivi hili Ladies Lounge tunaruhisiwa kuchangia? maana nina mengi ya moyoni 1😃
 

Similar threads

Tofali la kuchoma Hili ni tofali linalopatikana baada ya kutengeneza tofali la udongo na kulichoma kwa kutumia moto. Tanuri ya matofali unafunikwa kwa gana la udongo nje na chini yake moto inawaka kwa siku 2 au 3. Kutengeneza matoli wa njia hii ina gharama zaidi laini matofali yaliyochomwa...
Replies
0
Views
267
- Kuwa na maisha kamili/ full. - Kufanya maamuzi haraka, haina aja ya kushirikisha mtu.. mfano umepata kazi inayo kutaka kuama mkoa nk - Imarisha kazi au biashara yako bila kizuizi chochote, - Ishi maisha kwa njia yako mwenyewe. - Ishi bila kushughulika na fujo za mtu yeyote. Ongeza zingine
Replies
21
Views
361
Papai ni tunda la kushangaza na lenye afya. Ina 'antioxidants' ambayo hupunguza kuvimba na kupambana na magonjwa na kusaidia mtu kuonekana na umri mdogo. Virutubisho katika papai Kalori, Wanga, Nyuzinyuzi, Protini, Vitamini C, Vitamini A, Vitamini B9, Potasiamu, Kalsiamu na Magnesiamu. Faida...
Replies
5
Views
129
Watu wengi wameendelea kuzungumzia suala la maadili, hasa kwa vijana. Kwa mfano hili wimbi la panyarodi linaloendelea kutajwa kwa vitendo viovu, hii ni miongoni mwa sababu kubwa ya mmomonyoko wa maadili. Inaonekana dhahiri baadhi ya wazazi wameshindwa kutimiza jukumu la malezi ya watoto wao...
Replies
10
Views
177
Ndizi ni mojawapo ya tunda linalopendwa zaidi duniani, likiwa limesheheni vitamini na madini. Ziko faida kadhaa za kiafya za ndizi ambazo ni muhimu kwa mlaji kula tunda hili. Faida hizi ni pamoja na: 1: Inasawazisha maji ya mwili "homoni": ndizi ina kiasi kikubwa cha potasiamu na vitamini B6...
Replies
6
Views
213

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top