Idadi ya wanaume yaongezeka kufanya vipimo vya DNA nchini Uganda

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Gily

KF Founder & Dragon IGM
Staff member
Jun 4, 2023
7,020
22,618
113
Idadi ya wanaume wanaotafuta vipimo vya vinasaba (DNA) kwa watoto wao imeongezeka, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani amesema.

Simon Mundeyi amesema asilimia ya wanaume wanaodai huduma ya DNA kwa watoto wao imeongezeka kwa asilimia 70. "Hivi majuzi, idadi ya watu wanaoomba huduma za DNA imeongezeka. Wiki iliyopita pekee, tulikuwa na takriban watu 40, ambao walikuwa wakitafuta huduma za DNA kupitia wizara kwa sababu wanajua kwamba tunadhibiti Maabara ya Uchambuzi ya Serikali," amesema Mundeyi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Monitor, vipimo hivyo vya DNA huonyesha uhusiano kati ya spishi au vitu (species or objects) na kwamba matokeo ya uchunguzi wa DNA mara nyingi hutumiwa na madaktari ili kuthibitisha kama mzazi ana uhusiano na watoto.

Maabara ya Uchambuzi ya Serikali ni kituo cha kupima chenye makao yake makuu Wandegeya, Jijini Kampala. Hata hivyo Msemaji huyo wa wizara hiyo hakutoa takwimu za miaka iliyopita. Hata hivyo, alisema miaka mitatu iliyopita wastani wa watu watatu wangetafuta huduma hizo kwa mwezi, lakini sasa idadi hiyo inakaribia mamia.

Mundeyi metanabaisha kuwa hajui ni kwa nini idadi ya wanaume wanaotafuta vipimo vya DNA kwa watoto wao inaongezeka. Hata hivyo mwezi Aprili, Askofu Mkuu wa Kanisa la Uganda, Dk Stephen Kaziimba, ameeleza kuwa asilimia 10 ya wanaume wanakana kuwa baba wa watoto wao.

Hivi karibuni, mmoja wa wafanyabiashar awa ndani, aliwapima watoto wake na kugundua kuwa wengi wao sio wake. Wiki iliyopita, Mahakama ya Wilaya ya Mukono iliamuru kufanyiwa uchunguzi wa DNA wakili Male Mabiriizi na ndugu zake ili kubaini ikiwa ni wa baba mmoja.

Mahakama inasikiliza kesi ambayo wahusika wanapigania mali ya Marehemu Mohamed Bazindule Lulibedda Mutumba.

Mtandao wa Monitor, umeendelea kueleza kuwa vipimo vya DNA vinavyohusiana na uzazi vimekuwa na utata nchini. Mnamo mwaka wa 2013, baada ya ajali mbaya huko Namugoona iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 38, miili saba iliteketezwa bila kutambuliwa na Polisi walilazimika kufanya DNA kwa jamaa za marehemu.

Hata hivyo, vipimo vya DNA vya baadhi ya watu waliojitokeza kuwa baba au kaka, havikulingana na marehemu. Lakini vipimo vya DNA kwa akina mama vililingana na vya marehemu.


MWANANCHI
 

Similar threads

Jumla ya wanawake niliolala nao inafikia watatu. Wa kwanza tukiwa shule ya msingi darasa la nne. Wa pili nikiwa secondary kidato cha tatu, siwezi msahau Tausi. Wa nne nimedumu nae kwenye mahusiano kwa miaka mitatu tumeachana. Je ushawahi lala na wanawake au wanaume wangapi? funguka
Replies
46
Views
681
Ushalala kwa mwanamke? Ulikuaje? Ulilala kwa amani au ulikua uahofia njemba atakuja kugonga hodi saa yoyote? Wadau wanadai hatakama unalipa kodi kulala kwa mwanamke ni mwiko maana kuna alie lipia umeme, mwingine gas, na kuna alie nunua saboofer
Replies
0
Views
265
Wakuu ni fresh? Nimeandika uzi huu kwasababu jamaa yangu anasumbuliwa sana na mke wake kisa tu ni mjamzito.... Kwa uchunguzi wangu mdogo nmeona kama raha ni chache kuliko mazala yanayo wapata watu katika kipindi hiki. Wanaume wamekuwa wakipata usumbufu sana kutoka kwa wenza wao ikiwemo...
Replies
11
Views
452
Hali hiyo inaweza pia kusababisha mashambulizi ya hofu, ambayo kwa kawaida hujumuisha baadhi ya dalili zifuatazo za kimwili: Kutokwa na jasho sehemu kubwa ya mwili Maumivu ya kifua Kichefuchefu au usumbufu wa tumbo Ugumu wa kupumua au kuhisi pumzi inakata Kizunguzungu au kuzirai Mapigo ya moyo...
Replies
16
Views
231
Kumekuwa na nadharia kuwa wanaume wengi ambao wameoa hawapendi kuvaa pete za ndoa. Je ni kweli? na kama ni kweli kwa nini hupendi kuvaa Pete ya ndoa?
Replies
14
Views
227
Top Bottom