Je, ni bora kuoga na maji ya moto au baridi?

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Kuoga maji baridi
Ni jambo gani la kwanza linalokuja akilini unapofikiria juu ya kuoga baridi?

Faida za kuoga maji ya baridi
Kwanza maji ya baridi hukufanya uchangamke, hili ni tofauti na maji ya moto.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Thrombosis Research Institute, watu wanaooga maji ya baridi wanaongeza uzalishaji wa seli nyeupe za damu.

Utafiti huu unaeleza kuwa kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha metaboli mwili unapojaribu kujipasha moto, ndipo seli hizi nyeupe ambazo hupambana na maradhi zinapozalishwa.

Kumbuka hata wakati wa kuoga maji baridi kasi ya upumuaji hubadilika na kukufanya kuongeza kiasi cha oksijeni mwilini.

Pia, hulainisha ngozi na nywele tofauti na ilivyo kwa maji ya moto ambayo huchubua ngozi, hasa kwa kuondoa mafuta laini yanayolinda ngozi na nywele na kuzifanya ziwe kavu.


Kuoga moto
Watu wengi hupendelea kutumia maji ya moto kuoga pale hali ya hewa inapobadilika na kuwa ya baridi au wakati mwingine mtu anaumwa hivyo anatumia maji ya moto.

Lakini kwa ajili ya urembo na afya ya ngozi, maji ya moto yanatajwa kuwa ni kitu muhimu. Hizi hapa ni baadhi ya faida zitokanazo na matumizi ya maji ya moto angalau mara tatu kwa wiki

Kulainisha na kutunza ngozi: Maji ya moto husaidia kulainisha ngozi yako tofauti na ukitumia maji ya baridi. Maji ya moto hasa yaliyo katika jakuzi ambapo utatumia muda mrefu kidogo ngozi yako ikiwa kwenye maji, husaidia kuilainisha ngozi yako na kuiweka katika hali nzuri.

Usingizi: Kama huwa unapata matatizo kupata usingizi usiku, amka oga kwa kutumia maji ya moto kwani husaidia kulainisha misuli ya mwili wako na itakaa sawa na utaweza kupata usinngizi.

Kukuweka katika hali nzuri: Kuna wakati mwingine mtu hujisikia uchovu wa mwili na kutotaka kufanya chochote (Off mood). Ukioga kwa maji ya moto yatakusaida kukuondolea uchovu na utajisikia mwenye nguvu na upo tayari kukabiliana na changamoto za siku.

Kuchangamsha ubongo: Unapooga kwa kutumia maji ya moto husaidia kuchangamsha ubongo na kuufanya uweze kufanyakazi kwa ufanisi na kwa haraka zaidi.

Kushusha shinikizo la damu: Ukiachanna na masuala ya urembo, kuoga maji ya moto kunatajwa kuwa ni njia ya haraka ya kusaidia kushusha shinikizo la damu. Tafiti zinaonyesha kuwa mtu mwenye shinikizo la damu la kupanda, akioga kwa maji ya moto husaidia kushusha.

Kusaidia mzunguko wa damu: Ukioga kwa kutumia maji ya moto husaidia kusisimu na kuitanua mishipa ya damu hivyo kuwezesha damu kuwa na mzunguko mzuri mwilini.

Unapendelea kuoga maji ya moto au baridi?
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Inategemea na hali ya hewa, ila kwangu mizani inaegemea kwenye ya vuguvugu
FAIDA ZA KUOGA MAJI YA VUGUVUGU

1. Husaidia kupata usingizi nyakati za usiku

2. Huwafaa wenye maradhi ya njia ya hewa, kama kifua, kikohozi na mafua

3. Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu Loughborough wwamegundua kupitia utafiti liwa kuoga kwa maji ya moto ni sawa na kufanya mazoezi kwa saa moja
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Hasara za kuoga maji ya moto

1. Maji haya huweza kudhuru ngozi kwa kuharibu seli za keratin

2. Kwa wagonjwa wa ngozi hayafai

3. Huweza kuleta muwasho kwani joto hupelekea seli za ‘mast’ kutoa ‘histamine’ na kupelekea muwasho

4. Hayashauriwi kwa wenye maradhi ya moyo

Licha ya kuwa maji ya moto ni mazuri kiafya, unashauriwa kuto oga kwa maji ya moto sana kwani huathiri ngozi.

Hasara za kuoga maji ya baridi

1. Hayafai wakati wa maradhi.

Kwa watu ambao wana aina fulani ya ugonjwa sugu, hawashauriwi pia. Kwa kuwa kinga dhaifu inaweza kuharibiwa kwa kupokea maji baridi. Kwa hivyo, kama tunavyoona tu katika hali mbaya, tunaweza kusema kwamba kuoga au kuoga na maji baridi wakati wa baridi kunaweza kuwa na madhara.
 

Similar threads

Licha ya kwamba aina zaidi za tofali za kujengea nyumba lakini watu wengi hujiuliza sana kati ya tofali za kuchoma na tofali za bloku au tofali za simenti ni zipi bora zaidi? angalau zipi zinafaa zaidi kwa ujenzi? kuhusu kulinganisha gharama za hizi aina mbili.
Replies
14
Views
604
Afrika Kusini (Alama: 15.42): Afrika Kusini inaongoza kama nchi yenye ujasiriamali zaidi barani Afrika. Ikiwa na wafanyakazi wenye ujuzi wa hali ya juu, ari ya ushindani, na mazingira rafiki ya biashara, inajivunia uchumi wa pili kwa ukubwa katika bara na ni kitovu cha ukuaji wa viwanda katika...
Replies
9
Views
324
Viwango vya kubadilisha fedha ni muhimu katika uchumi wa dunia kwa sababu vinaathiri biashara ya kimataifa, uwekezaji na utalii. Kuelewa jinsi viwango vya ubadilishaji vinavyofanya kazi na jinsi vinavyoathiri sekta mbalimbali za uchumi ni muhimu kwa biashara, watalii na serikali. Viwango vya...
Replies
8
Views
239
Wasalaam Kumekuwa na ubishani mwingi kuhusu yupi ni mwanamziki bora wa kike kuwahi kutokea. Kwenye Billboard Award Top Artist Taylor Swift amekuwa akiongoza kupata tuzo zaidi ya mara nne wakifatuwa na Christina Aguilera, Adele, Alicia Keys, Mariah Carey, and Rihanna. Ila binafsi katika...
Replies
10
Views
855
  • Question Question
Kutokana na umuhimu wa bank kwa matumizi mbalimbali leo ningependa ma expert wa humu kutoa nondo juu ya akaunti za bank na faida kwa mtumiaji wa namna fulani Unaruhusiwa kujadili bank yeyote ila mimi ningependa tuanze na hizo hapo juu Karibuni
Replies
11
Views
209

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom