Je unaweka akiba? Jifunze kuweka akiba

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Wahenga Walisema AKIBA HAIOZI.

Simamia matumizi bora ya fedha zako, kujenga maisha yako. Kuweka akiba ni moja ya matumizi mazuri ya kuhifadhi fedha yako. Wengi hudhania kuweka akiba ni lazima uwe na kipato kikubwa, lakini ukweli ni kwamba kuweka akiba ni maamuzi.

Weka angalau 5% - 40% kwenye akiba.
Wataalamu wanapendekeza kwamba hazina hii ya dharura (akiba) iwe sawa mara tatu au sita ya mshahara wako wa kila mwezi, kwa sababu ni bima ya kibinafsi ikiwa utapoteza kazi yako au kukabiliwa na gharama za afya zisizotarajiwa.

Mfano.
Kila siku unatenga Tsh.1000 au Tsh.5000/ au 10000/

Au unapanga kwamba kila wiki utaweka akiba ya Tsh.10,000/ au Tsh.50,000/= Au Tsh.100,000/

Hii itakusaidia kujizatiti (commitment) katika uwekaji wa akiba. Maana mfumo uliozoeleka na unaosisitizwa wa kuweka akiba ni kutenga asilimia 10% au 20% ya kila pesa unayopata.

Epuka matumizi yasiyo na lazima
Wengi wetu tuna matumizi yasiyo na lazima ambayo yanatupotezea mda na fedha kila siku.

Katika matumizi yako angalia matumizi yapi ambayo yanakigjarimu fedha na hayana ulazima. Matumizi haya yaache kabisa ili uweze kuongeza kipato chako cha akiba.

Tumia kiasi kidogo kwenye matumizi yasiyo ya msingi
Kuna matumizi mengi ambayo sio ya msingu mfano unakuta mtu anapitia sehemu anakula mishikaki akiwa anaelekea nyumbani, wakati huko nyumbani teyari kuna nyama. Tumia pesa kidogo kwa bidhaa ambazo hazichangii kwa kuishi kwako.

Kujenga mazoea ya kuishi kwa kipato chako
Kwa kawaida, tabia/mazoea yako hutengenezwa hasa na kipato chako. Watu wanaishi maisha ya gharama sana yasiyoendana na kipato Chao. Hapa unahitaji kuzingatia haswa nidhamu katika suala la matumizi ya fedha.

Jaribu kuishi kwa uchache wakati huu na usiwe na manunuzi ya kighafla. Baadaye siku za usoni, utagundua kuwa kutotumia pesnihovyo ni rahisi zaidi kuliko matumizi ya pesa ovyo.

Je unaweka akiba? njoo tujifunze kwa pamoja namna ya kuweka akiba.

Toa ushauri namna gani unaweza hifadhi akiba yako.
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Namna unaweza hifadhi akiba yako
Zipo njia ambazo ni nzuri zikitumika kwa kuweka akiba kwa faida zitaongeza maendeleo ya wengi. Njia hizo ni:

Moja, ni kununua fedha za kigeni. Mara nyingi fedha za kigeni mfano Dola za Marekani, Euro, Pound ya Uingereza na fedha kutoka Bara la Asia kama vile za Saudi Arabia, huwa zinapanda thamani ukilinganisha na za Tanzania.

Mfano, ulinunua Dola moja ya Marekani Novemba, mwaka jana kwa Sh1,300. Mwaka huu unaiuza kwa Sh2,100. Ukipiga hesabu umepata faida ya Sh800. Kama ulinunua Dola 10,000, leo hii ikiziuza una faida ya Sh1 milioni, na kadhalika.

Mtindo wa kununua dola kwanza unapunguza kubeba lundo la fedha nyingi, inakuzuia kuitumia bila sababu, hivyo kuendelea kuwa akiba, kukulinda na kukuwezesha uwe na faida pale mfumuko wa bei unapoongezeka na inaweza kukusaidia iwapo itakulazimu usafiri nje ya nchi. Ukisafiri nje ya nchi itakufanya usitumie fedha nyingi za kununua za kigeni kwa gharama kubwa.

Pili, ni simu benki. Huu ni mfumo ambao upo sana siku hizi eneo la Afrika Mashariki. Siku hizi kampuni za simu zimewezesha mtu kuweka akiba.

Huduma imeboreshwa zaidi kwa kuweza kuzihamishia kwenye akaunti za benki, kulipia huduma na bidhaa au kuzitoa katika nchi nyingine kulingana na aina ya fedha za eneo husika.

Hii inamuwezesha hata kama mtu akiwa mbali na benki na kuwa na uwezo wa kuokoa muda kwa kutumia pesa alizoweka kwenye simu yake kwa kuzitoa kwa wakala aliye karibu naye.

Vilevile, kwa kutumia simu waweza kuvuta fedha kutoka kwenye akaunti yako ya benki na kuziingiza kwenye simu yako na kuwa huru kuzitoa ili kuzitumia eneo lolote kwa kutumia mawakala.

Siku hizi pia kwa kutumia akiba kwenye simu unaweza kupata huduma nyingine kupitia simu hiyo kama vile kununua umeme, kulipia bili ya maji, matibabu, king’amuzi na hata tiketi za kuingia kwenye michezo ya soka au tamasha. Mtu aweza kudunduliza fedha kidogokidogo kwenye simu yake.

Tatu, kuweka akiba kwa kutumia benki na taasisi nyingine za kifedha. Hii husaidia sana kuhamasisha huduma za kuweka akiba kwa malengo kama vile kumsomesha mtoto au amana.

Uwekaji wa fedha za namna hiyo pia huweza kusaidia kuwa na fedha za kukabili dharura na kuwa na mitaji mikubwa ya kibiashara na hatimaye kuleta maendeleo makubwa yaliyokusudiwa.

Nne, ni kumkopesha mtu na kurudisha kwa riba. Siku hizi aina hii ya ukopeshaji imeenea sana, hasa mijini na vyuoni. Hii imetokana na watu kuzidi kukua sana kiuelewa, wamebadili mwelekeo kutoka kumkopesha mtu pasipo riba hadi kuwa na faida.

Watu wameerevuka na kufahamu kuwa fedha ya mwezi au wiki hii ni tofauti na ya mwezi au wiki lijalo. Tatizo lililopo ni kwamba hakuna maandishi ya kukopeshana kwa walio wengi kwa sababu za kujali utu. Lakini ukweli ni kwamba wanadamu wengi wana tabia ya kubadilika. Kama huna maandishi ya kukopeshana itakuwa vigumu kupata fedha zako pale anapokuwa si mwaminifu.

Tano, ni kuwekea bima mali zako na biashara yako. Hii ni njia ambayo ni muhimu sana maana hakuna mtu anayeweza kuzuia majanga ambayo ni ya asili au ya kawaida, hivyo bima hasaidia sana siku ukipata ajali ya biashara kwa kuibiwa au kuungua.

Sita, ni kununua vitu kama nyumba, ardhi na vifaa vya gharama vyenye kudumu muda mrefu. Hivi waweza kuviuza baadaye kwa bei ya juu.

Maendeleo ya mtu mmojammoja ni mafanikio ya taifa. Taifa lenye akiba ya kutosha kwa kawaida linakuwa imara na wananchi wenye akiba kwa njia mbalimbali kama nilivyoorodhesha, ni watu wenye maisha ya uhakika. Dharura zote wanaweza kuzikabili na hapa ndipo pia mitaji mikubwa ya biashara inatokea. Kuweka akiba ni jambo la msingi, tuanze leo kuweka akiba.

 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
sasa ukute una watu wengi wanakutegemea, na una mshahara kidogo, utawekaje akiba??
Swali Zuri sana.
Watu wanaokutegemea ni watu wa namna gani?

Hapa jirani kuna mama mtu mzima labda miaka 50 hivi anamalizia. Huyu mama hafanyi kazi yeyote anategemea mwanae wa kiume wa miaka 30 hivi atafute amletee.

Ukitazama kuna wamama wa Rika lake wako wanajituma kwa shunguli ndogo ndogo na wanaendelez maisha yao.

Umejifunz nini? kabla sijaendelea
 

mshamba_mkuu

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
1,563
Reaction score
4,525
Points
0
Swali Zuri sana.
Watu wanaokutegemea ni watu wa namna gani?

Hapa jirani kuna mama mtu mzima labda miaka 50 hivi anamalizia. Huyu mama hafanyi kazi yeyote anategemea mwanae wa kiume wa miaka 30 hivi atafute amletee.

Ukitazama kuna wamama wa Rika lake wako wanajituma kwa shunguli ndogo ndogo na wanaendelez maisha yao.

Umejifunz nini? kabla sijaendelea
huyo mama case yake ni tofauti

sasa ukute mtu ana familia, wake na watoto... hapo vipi
 

Muhindi Wa Kuchoma

Well-known member
Platinum Villager
Joined
Jul 9, 2023
Messages
3,821
Reaction score
3,805
Points
113
Kuweka akiba kwa ajili ya kustaafu
Kuweka akiba kwa ajili ya kustaafu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa una maisha mazuri ya baadaye. Utakuwa na uwezo wa kuacha kufanya kazi nje ya lazima katika umri wa kuridhisha na kujikimu wewe na familia yako bila mapato ya kawaida.

Uhitaji wa akiba ukiwa umepoteza Kazi
Katika uchumi wa leo, hakuna dhamana ya utulivu wa kazi. Ikiwa itatokea ukapoteza kipato chako ghafla, kuweka akiba itakusaidia kukusonga hadi upate ajira mahali pengine. Akiba zitafanya kile ambacho dharura hufanya wakati ambapo hutarajii.

Fanya akiba yako Ikufanyie Kazi
Ikiwa umehifadhi pesa za kutosha, unaweza hata kuchukua fursa hii kuwwkeza akiba yako kidogo. Kuweka pesa kwenye miradi ambayo unaweza kutumika unapohitaji, lakini pia unapotaka, ni uwekezaji bora.
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
huyo mama case yake ni tofauti

sasa ukute mtu ana familia, wake na watoto... hapo vipi
Sasa kama kazi yako inakubana kiasi cha kutoweza kuweka akiba kuna mawili
1. Utafute kazi nyingine - Part time Job ili kukidhi mahitaji ya kuweka akiba

2. Tafuta kazi nyingine - Kazi yenye maslai mazuri
 

Similar threads

Hello, Kama unataka kujifunza kubeti au kuingia kwenye betting industry... Aka MIKEKA... basi uzi huu ni wako.. Nitakuelekeza hatua kwa hatua na kama una swali uliza.. Kumbuka hapa nitaongelea tu betting ya kwenye SOKA (football) Kubeti ni nini? Kubeti ni kubashiri , (matokeo au hata...
Replies
16
Views
915
Kwenye Thread hii nitakuwa naleta mafundisho ya PHP kidogo kidogo mpaka tutakapofikia level za kuunda dynamic website yetu Nimuhimu kuwa na uelewa na HTML kidogo ili kuendelea
Replies
31
Views
553

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom