Jifunze kubeti (SOKA) hapa kwa urahisi... Kwa wanaoanza tu!

Allan

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 4, 2023
Messages
24
Reaction score
67
Points
0
Hello,

Kama unataka kujifunza kubeti au kuingia kwenye betting industry...
Aka MIKEKA...

basi uzi huu ni wako..

Nitakuelekeza hatua kwa hatua na kama una swali uliza..
Kumbuka hapa nitaongelea tu betting ya kwenye SOKA (football)

Kubeti ni nini?

Kubeti ni kubashiri , (matokeo au hata matukio yatakayojiri kabla hayajatokea kwenye mechi husika)

Sasa tuanze...
Kabla hujaanza kubeti ni vizuri kwanza kufahamu ligi mbali mbali na kisha chagua angalau ligi ZAKO MBILI AU TATU tu! Ambazo utakuwa unaDEAL nazo!
Hii itakusaidia kujua aina ya matokeo Yao na mwenendo wa ligi Yao na itakusaidia sana huko baadae!

Kuna aina mbali mbali za kubeti (KULINGANA NA MTAZAMO WANGU)
1. Kubeti kwa takwimu (kwa akili) hapa unaangalia aina ya ligi, head to head, majeruhi, nani Yuko nyumbani etc.. na unachagua bet KULINGANA na takwimu.
2. Kubeti kwa HISIA ( machale😂) yaani hapa unaweka mkeka kulingana na unavyojisikia wewe! Mfano Manchester united Vs Forest Green , uwanja wa Nyumbani wa man utd (old Tranford) ila machale Yako tu unaamua kumuua Man utd!😂

Itaendelea sehemu ya pili hapo kwenye comment
 
Sijawahi kubet ila juzi kuna mamba kapiga hela ya kutosha
 
Sehemu ya pili - MASOKO

sasa ili kuanza kubeti lazima ujue MASOKO.

MASOKO tunaweza kuyaita (options) au machaguo
Kuna MASOKO Mengi sana! Zaidi ya 50..
Lakini kwakuwa tunajifunza tutaangalia MASOKO manne tu ya kuanza nayo..

1. Soko la kwanza ( NJIA TATU -THREE WAY)
hili ndio soko mama zaidi yaani katika mechi kuwe na tokeo mojawapo katika matatu
Yaani
1. Timu ya nyumbani kushinda (chagua 1)
2. Sare (chagua X)
3. Timu ya ugenini kushinda (chagua 2)

Kwamfano
Man utd Vs Newcastle
Man UTD kushinda (1)
Newcastle kushinda (2)
Sare (X)

2. Soko la pili (over/under)

Hapa unatabiri magoli yatakayopatikana kwenye mechi (haijalishi yamefungwa na timu Gani)
Mfano over 2.5

Maana yake mechi itoe magoli yanayozidi mawili na
Under 2.5
Maana yake mechi itoe magoli yasiyozidi mawili

3. Soko la tatu - Both teams to score (yes/no)
Hapa timu zote zifunge magoli , au zote zisifunge au Moja tu ndio ifunge..

4. Soko la nne - Double chance

Hapa katika Yale matokeo matatu ya mpira wewe unaweza kuchagua mawili katika mechi moja mfano

Man utd Vs Newcastle

Unaweza kuchagua 1X (yaani man ashinde au atoe sare) au
12 (ni Moja mbili- sio kumi na mbili😂) yaani hapo man ashinde au Newcastle ashinde au

X2 ( yaani Newcastle kushinda au sare)


Jambo la mwisho ni (Odds - bei)
Katika Kila soko utakalochagua Kuna bei zake na ndio hizo zinaitwa odd

Kwahiyo utachukua iyo Odd ya hiyo soko lako utazidisha na kiasi Cha pesa unaweka!

Kumbuka odd (bei) zinajizidisha kwa kadri unavyoongeza mechi


Karibu kwa maswali...
Cheza kiustaarabu 😂😂😂
 
Nilikutana na mshikaji Ana buku tano anaenda kubeti apate hela ya kula mchana na usiku
 
Ukishaweka mkeka kabla mechi hazijaanza yaani Kuna amani flani hivi na ujasiri wa ajabu unakuja...


Game zikianza Sasa😝😝😝
 

Similar threads

Wahenga Walisema AKIBA HAIOZI. Simamia matumizi bora ya fedha zako, kujenga maisha yako. Kuweka akiba ni moja ya matumizi mazuri ya kuhifadhi fedha yako. Wengi hudhania kuweka akiba ni lazima uwe na kipato kikubwa, lakini ukweli ni kwamba kuweka akiba ni maamuzi. Weka angalau 5% - 40% kwenye...
Replies
11
Views
284
Kwenye Thread hii nitakuwa naleta mafundisho ya PHP kidogo kidogo mpaka tutakapofikia level za kuunda dynamic website yetu Nimuhimu kuwa na uelewa na HTML kidogo ili kuendelea
Replies
31
Views
553
Kwa mechi iliyopigwa kwa Mkapa majamaa wanakaba katika njia hawaruhusu penetration pass wala kufanya makosa ya wazi. Kwenye kumshambulia sasa umakini mkubwa na pasi zenye macho golini hawana parapara. Sioni mahala Yanga watapindua meza labda meza ya vikombe vya kawaha
Replies
12
Views
139
Back
Top