Madereva daladala Arusha wagoma, abiria wapanda toyo

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,617
Reaction score
26,429
Points
113
Arusha. Wakazi wa Jiji la Arusha wakiwamo wanafunzi waliofungua shule leo Jumatatu Julai 3, 2023 wamepitia msoto wa hali ya juu kutokana na kukosa usafiri.

Adha ya usafiri imesababishwa na mgomo wa daladala unaoendelea katika barabara zote za Jiji la Arusha na Arumeru kushinikiza kuondolewa kwa bajaji katika ruti zao.

Akizungumzia hali hiyo miongoni mwa abiria, Amina Hassan amesema mgomo huo umeanza leo asubuhi umesababisha mateso makubwa kwa wakazi wa Jiji la Arusha pamoja na wanafunzi wanaotumia usafiri huo kuwahi makazini na shuleni.

"Tunaomba Serikali itafute suluhu ya jambo hili kwani tunaoteseka ni wananchi na hili jambo la daladala kugoma imekuwa siyo mara moja," amesema.

Ramadhani Ally aliiomba serikali kusikilizwa madai ya daladala na kutatua changamoto hiyo.
"Shida hawa daladala wanataka wao wenyewe ndio wafanye kazi ya usafirishaji wakati hii ni biashara huria, inafaa kila mtu acheze kwenye nafasi yake kupata kipato.

“Hivyo tunaomba Serikali isikilize madai yao kama yana maana watatuliwe lakini kama ni haya ya ubinafsi wenzao wasifanye kazi basi wanaohamasisha mgomo wafutiwe leseni," amesema.
Akizungumzia mgomo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro, Locken Adolf amesema kuwa utitiri wa bajaji umeathiri biashara ya daladala hivyo wanaiomba serikali kuzipunguza.

"Ukubwa sa eneo la Arusha, hazitakiwi kuzidi zaidi ya 100 lakini sasa zimekuwa nyingi na zimekuwa kero sana na zimeteka ruti zote za daladala. Pia zinafanya biashara ya kupakia abiria kama wanavyofanya wenzao jambo ambalo siyo makubaliano wakati zinaingia mjini," amesema.

Amesema kuwa katika ufuatiliaji wamebaini bajaji nyingi ndani ya Jiji la Arusha hazina leseni lakini zinaruhusiwa kufanya kazi tofauti na daladala ambazo zimekuwa zikipigwa faini kila hatua.

"Tunataka kujua anayesimamia hizi bajaji ni nani na ana sauti gani kwenye mamlaka za serikali zinazosimamia usafirishaji, kwa kuwa wao wanafanya kazi kinyume na sheria, taratibu na makubaliano lakini hawafanywi chochote wanazidi kupeta tu," amesema.

Akizungumzia adha hiyo Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), Mkoa wa Arusha, Amani Mwakalebela amesema kuwa wamesikia mgomo huo na wanaendelea na taratibu za kushughulika na madai ya madereva hao wa daladala.

"Sisi tumesikia madai yao na tunaendelea kuyafanyia kazi hivyo niwaombe warudi barabarani kuendelea kutoa huduma na tutawapa majibu ya suluhu ya changamoto yao," amesema.

Katika hilo Mwakalebela amekiri ongezeko la bajaji ndani ya Jiji la Arusha hasa ruti za Sombetini-Ngusero, pia njia ya Majengo, pamoja na ile ya Uswahilini -Dampo ambapo wameanza kuhukua hatua.

"Kweli kuna ongezeko la bajaji ambapo katika 350 zilizosajiliwa na zoezi kufungwa lakini kwa haraka haraka kuna zaidi ya bajaji 2,000 ambazo zinafanya kazi na kugeuka kero, hivyo tulichoamua ni kuomba oda ya mahakama kuzipiga mnada bajaji ambazo tutazikamata hazina usajili wala leseni na uzuri tulishafunga mwaka jana," amesema Mwakalebela.


MWANANCHI
 
yah! nazinapunguza usumbufu mwingi kwa abiria asietaka mikiki, kama utapanda hiace kuna kuku mwingine kabeba ndizi, mwingine anakula mahindi choma, mwingine kajipulizia manukato makali, mwingine anaongea nasimu mara mabishano ya mpiraa,, mpaka unashuka kichwa kinauma
 
Sio kweli
ni kweli.... huku mbeya watu wanaziogopa sana kwasababu hiyo....

mimi nilikua sijui, ila kuna lecturer mmoja mwenyeji wa huku alituambia....

siku moja nikapanda tumejaa weee, ikafika kwenye mteremko ikalala kiupande, ikatudondosha.....

sirudii tena.
 
Sio kweli
zinasababisha sana ajali pia....

mimi naamini public transport no.1 kwenye miji inapaswa kua daladala
ni kweli kabsa hii ni kutokana na nature ya watu waopanda hizo gari wengi wana vimizigo vidogovidogo vingi... japo isiwe ndio kuzuia na bajaji jamani
 
ni kweli.... huku mbeya watu wanaziogopa sana kwasababu hiyo....

mimi nilikua sijui, ila kuna lecturer mmoja mwenyeji wa huku alituambia....

siku moja nikapanda tumejaa weee, ikafika kwenye mteremko ikalala kiupande, ikatudondosha.....

sirudii tena.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Nimecheka kaa fala aseeee. Pole mkuu 😅😅🤣🤣🤣🤣😆😆😆.

Njaa haikuuma,
 

Similar threads

Hamjambo? Mimi sijambo 😃. Wakuu nimekutana na mjadala asubuhi wakati naelekea katika shughuli za watu hizi... Mjadala ulikua mzito, ndio mara ya kwanza kukutana na mjadala kila mtu anauchangia kwenye gari.. yaani walikua wanaushambulia haswaa.. Mjadala ulianza baada ya daladala nliyokua...
Replies
12
Views
425
Hapa ni yote magumu tunayopitia kwenye daladala Kigumu zaidi kwangu mimi nihiki, kunasiku nilipanda daladala tegeta to gerezani Bwana we gari imefika jogoo imeshona na mimi nimesimama karibu na mlango wa gari mara akapanda kadada kamevaa abaya limemkaa hatari tena la pink fulani hivi Yule...
Replies
72
Views
813

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top