Mchanganuo wa biashara ya Chips

Hakimu

Immortal Village Hero
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 3, 2023
Messages
2,699
Reaction score
6,206
Points
113
Habari! Leo nitawaeleza mchanganuo wa biashara hii ya chips biashara ambayo imepamba moto maeneo ya mijini hasa dar es salaam

Kwanza biashara hii huathiriwa na vitu vingi kama zilivyo biashara nyingine

Nakumbuka mitaa flani nilikuwa nikiishi kulikuwa na huyo mama wa kichaga alikuwa anapata wateja kuliko wauza chips wengine, Siri ilikuwa ni utamu wa chips, hapunji na lugha nzuri kwa wateja

Twende kazi mtaji ambao utatumia hapa ni chini ya 500,000 twende kazi

MAMBO MUHIMU KWENYE BIASHARA

Kwanza lazima uzingatie eneo lenye frusa na uhitaji wa bidhaa hii, asikwambie yeyote biashara ni sehemu ukishindwa kupata sehemu ambayo utauza basi tegemea hasara, maeneo yenye watu wengi (njia, barabara), saloon za kike n.k ni baadhi ya maeneo ambayo ni mazuri kwa biashara hii

Usafi ni kero kwenda kwa mtu anavidonda,makucha marefu, uchafu au kunuka jasho, mazingira yasafishwe zuia nzi na wadudu wengine wasumbufu

Usiri ikiwezekana basi hakikisha wateja wako wanapata privacy wakati wa kula sio mtu anakuja anakula, mara rafiki yako kaja masihara, matusi na mikelele pia zingatia kutoonekana wakati wana jisosomola


Gharama za vitu muhimu

Jiko la chips = 50,000
Jiko la mishikaki = 35,000 - 45,000
Kabati la vioo = 200,000 - 300,000
Sahani 10 = 15,000
Meza ndogo = 50,000
Vifaa vya kazi 50,000

Gharama za kuendeesha biashara

Kodi = 3,000 - 5,000
Mkaaa= 7000 - 12,000
Ndoo ya viazi= 15,000 - 30,000
Kuku (Kulingana na idadi) * 5,000 - 7000
Mayai trei moja = 8,000
Mafuta lita 3 @14,000
 
Biashara ya Chips ni biashara ngumu sana kwa sababu ya gharama za kuandaa. Mfano
1. Bei ya mafuta iko juu sana
2. Bei ya mkaa iko juu pia

Huwezi Pata faida nzuri kama unauza ndoo mbili. Nimeona watu wengi wakiuz chips ndoo mtaani. Na hapo wanalalamika biashara ni mgumu
 
Biashara ya Chips ni biashara ngumu sana kwa sababu ya gharama za kuandaa. Mfano
1. Bei ya mafuta iko juu sana
2. Bei ya mkaa iko juu pia

Huwezi Pata faida nzuri kama unauza ndoo mbili. Nimeona watu wengi wakiuz chips ndoo mtaani. Na hapo wanalalamika biashara ni mgumu
Ni kweli
 
aisee zinalipa sana hii kitu japo kila biashara inalipa ukisimuliwa hii inasisimua zaidi
 

Similar threads

Mapendekezo ya wafanyabiashara Kasi ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Wafanyabiashara kwa sababu kuna mambo mengi mazuri yanayoweza kustawisha biashara na sekta binafsi. Serikali inatakiwa kutochoka kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara, kwa sababu wao ndio wanajua shida...
Replies
1
Views
191
Mambo matatu muhimu wakati wa kuanzisha biashara 1. Hata kama unayo pesa ya kuanza biashara kubwa. Anza kidogo kisha ikuze kutokana na mzunguko unavoenda. 2. Kama ikiwezekana usifungue biashara mbali sana na eneo lako la umahiri. 3. Anza na mtindo mmoja wa biashara, na katika aina moja ya...
Replies
15
Views
418
Habari Wanakijiji Kumekuwa na malalamiko mengi kwa vijana kuwa pesa ya kukodi fremu ni kubwa sana,na haswa hapa mjini tatizo hilo limekuwa changamoto ambayo kuiepuka uwezi na hawa madalali sasa wanatumia huhitaji wa fremu kuwa ajili kwao,basi katika kuangalia fursa unazoweza kuzifanya bila kuwa...
Replies
12
Views
226
Una wazo gani la biashara? Wengi hupenda kufanya biashara ila wanakwama kwa kukosa mitaji. Hebu eleza hapa unataka kufanya biashara gani na unategemea itakuwa ya mtaji wa kiasi gani. .
Replies
30
Views
690
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema haitafunga maduka wala biashara ya mfanyabiashara yeyote kwa kuwa huo ndio utaratibu waliojiwekea. “Kwa sasa TRA haihusiki kufunga biashara au maduka ya mfanyabiashara yeyote na ikitokea mtu amejitambulisha kuwa ni mtumishi anayetoka katika ofisi yetu...
Replies
3
Views
701
Back
Top