Mchepuko wangu utanirudisha kwa mke wangu kwa lazima .

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Watoto wa kidugala

Well-known member
Platinum Villager
Joined
Jul 8, 2023
Messages
195
Reaction score
704
Points
93
Habari wanakijiji .
Ukweli usiopingika kwangu ni kuwa mwanaume rijali kukosa mchepuko inawezekana ila inahitaji nguvu kubwa ya Mungu mwenyewe .

Hapo zamani nikiwa mlevi sana nilipenda sana vidada vidogo vidogo ili niyasukume maisha yangu katika raha na mustarehe ukizingatia mke wangu ni mtu bize bize sana na kulijenga taifa .

Mwenzenu baada ya kuachia ofisi rasmi nilisema naacha pombe na wanawake nawatema nabaki na kipenzi changu tu mmoja yaani mke wangu wa ndoa ila sasa nilikuwa na michepuko mingi isiyokuwa na idadi , Mungu ni mwema alikuwa upande wangu yote niliitupilia mbali isipokuwa mchepuko mmoja kiukweli nilishindwa kuuacha maana bond yangu mimi na yeye ni ngumu kuamka na kusema tuachane .

Huyu ni mdada wa kihaya , niliingia naye kwenye mahusiano akiwa na umri mdogo na akiwa chuo kimoja hapo jijini kwa bwana Chalamila .
Nikamtunza kama mwanangu , nikala vinono vyake vyote na mwisho shule akahitimu , ofisini nikamvuta na sasa mfumo unamtambua .

Sasa nilijipa muda kuwa tunakoenda nitakaacha polepole ili nisikaumize maana masikini ya Mungu kanadai kapo tayari kawe ka mke kadogo ila nikijitizama na huu uzee aibu naona mimi 😀😀

Nikasema basi sawa ila moyoni nawaza nimueleze ukweli kuwa binti tafuta future husband mimi nina magonjwa yangu niache nitangulie kukuwekea siti huko Janatu Firdaus .

Sasa kiini cha stori yangu ni hapa kuwa kwa haya ninayoyaona itabidi nimuache kwa lazima maana simuelewi nimekuwa namvumilia sana ila sasa imetosha binti anategeshea mida ambayo anajua fika niko nyumbani na mama la mama , sasa mchepuko wa hivyo ni wa nini ?

Mara apige mavediocall yake alafu anajua fika muda huu siwezi pokea labda simu ya kawaida .

Kwa haya naona mchepuko unafosi niuache kwa hiyari kabisa .

Ni mengi ananikomoa ila kwa hili ni big no .

Sitaki ushauri ila nawakumbusha jitahidini kuweka mipaka na hawa michepuko wanaweza kukidharirisha .
 
Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Michepuko ni changamoto sana
Nilishakuwa na wangu mmoja aisee nikajisahau kabisa
Sasa siku moja dada wa kazi akaniomba tuongee. Yule dada wa kazi akanambia kuwa boss wake (demu wangu) huwa anaamka usiku anachanganya madawa anataka jina langu.

Wema haujawahi kuoza kwa sababu yule dada wa kazi nilikuwa namnunulia vizawadi vidogo vidogo basi akawa mwema kwangu. Kuja kuchunguza yule mchepuko anataka kunipika kwenye chungu kaja kwangu na muogo mbichi kaniletea zawadi. Nikashtuka kwa sababu tangia lini nikala mihogo mibichi? nikamchana ukweli kuhusu michezo yake

Sijui alihofia maisha yake maana alikuwa anatetemeka sana. Ila huwa watu wanaongea nyuma ya mgongo kuwa japo nacheka ni mkali sana. Tena wanasema muangalie hata macho yake brother mkali sana kuwa makini nae😀

Mchepuko akiwa na akili ni kama umeokota dhahabu chini.
 
mshamba_mkuu

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
1,563
Reaction score
4,525
Points
0
Kama uko serious sema niko tayari hata usiku huu .
Japo kaa jua kana matumizi mabovu kama unajitafuta muache kwanza ila kam tayari ushatengeneza ngome njoo uchukue namba , niko tayari kukaozesha kwa real futute husband
kwahiyo mzee hamna mwanaume mwamminifu kwenye ndoaa??

kabisa kabisa??
 
Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Kama uko serious sema niko tayari hata usiku huu .
Japo kaa jua kana matumizi mabovu kama unajitafuta muache kwanza ila kam tayari ushatengeneza ngome njoo uchukue namba , niko tayari kukaozesha kwa real futute husband
Sasa huyu dogo ni mwanafunzi
Pia yuko Mbeya pia mzee anasoma huko

Hapo hajiwezi ataweza kumuoa kweli🤣
 
Watoto wa kidugala

Well-known member
Platinum Villager
Joined
Jul 8, 2023
Messages
195
Reaction score
704
Points
93
aisee mnaishi kwa stress sana😂

viharusi vitawamaliza
Kikubwa kufurahi tu maana hata ninyi vijana stress zinawauwa kwa kutamani msiyoweza kuyapata maana dunia imebadilika hakuna cha nina degree wala diploma wote ni karume kuuza nguo za saula saula 😀😀
 
Nourhan

New member
Joined
Jul 15, 2023
Messages
23
Reaction score
63
Points
0
Nilijua tu ni Baba Wao ni Wao 😂😂😂 nimefurahi kwa kweli.
Habari wanakijiji .
Ukweli usiopingika kwangu ni kuwa mwanaume rijali kukosa mchepuko inawezekana ila inahitaji nguvu kubwa ya Mungu mwenyewe .

Hapo zamani nikiwa mlevi sana nilipenda sana vidada vidogo vidogo ili niyasukume maisha yangu katika raha na mustarehe ukizingatia mke wangu ni mtu bize bize sana na kulijenga taifa .

Mwenzenu baada ya kuachia ofisi rasmi nilisema naacha pombe na wanawake nawatema nabaki na kipenzi changu tu mmoja yaani mke wangu wa ndoa ila sasa nilikuwa na michepuko mingi isiyokuwa na idadi , Mungu ni mwema alikuwa upande wangu yote niliitupilia mbali isipokuwa mchepuko mmoja kiukweli nilishindwa kuuacha maana bond yangu mimi na yeye ni ngumu kuamka na kusema tuachane .

Huyu ni mdada wa kihaya , niliingia naye kwenye mahusiano akiwa na umri mdogo na akiwa chuo kimoja hapo jijini kwa bwana Chalamila .
Nikamtunza kama mwanangu , nikala vinono vyake vyote na mwisho shule akahitimu , ofisini nikamvuta na sasa mfumo unamtambua .

Sasa nilijipa muda kuwa tunakoenda nitakaacha polepole ili nisikaumize maana masikini ya Mungu kanadai kapo tayari kawe ka mke kadogo ila nikijitizama na huu uzee aibu naona mimi 😀😀

Nikasema basi sawa ila moyoni nawaza nimueleze ukweli kuwa binti tafuta future husband mimi nina magonjwa yangu niache nitangulie kukuwekea siti huko Janatu Firdaus .

Sasa kiini cha stori yangu ni hapa kuwa kwa haya ninayoyaona itabidi nimuache kwa lazima maana simuelewi nimekuwa namvumilia sana ila sasa imetosha binti anategeshea mida ambayo anajua fika niko nyumbani na mama la mama , sasa mchepuko wa hivyo ni wa nini ?

Mara apige mavediocall yake alafu anajua fika muda huu siwezi pokea labda simu ya kawaida .

Kwa haya naona mchepuko unafosi niuache kwa hiyari kabisa .

Ni mengi ananikomoa ila kwa hili ni big no .

Sitaki ushauri ila nawakumbusha jitahidini kuweka mipaka na hawa michepuko wanaweza kukidharirisha .
 
Similar threads

Wakuu kwema? Mimi ni kijana wa kiume umri miaka 26, ni mtoto watatu katika familia ya watoto wa 5, mwaka huu namaliza chuo maswala ya misitu. Baba yangu ni mstaafu alikua ni mwalimu wa chuo (lecturer) Chuo cha maendeleo ya jamii, mama yeye alikua anajishughulisha na mashirika ya kusaidia...
Replies
15
Views
518
Habari na karibu ktk moja na mbili ya kuelimishana sisi kama mavijana. Tabia zako zina athari kubwa mahali pesa zako zinakwenda. Pesa haiwezi kamwe kuzidi mikononi mwa mtu mwenye tamaa ya kutumia hela tu. Jifunze kuwa na ujuzi wa kifedha. Usiwe na haraka ya kukimbia wakati haujajifunza...
Replies
9
Views
424
Mficha maradhi kifo humumbua, nateseka naumia sana toka niachane na ex wangu. Tulikuwa na uhusiano miaka 2 iliyopita, baada ya kufuma message WhatsApp namtongoza msichana mmoja hivi mtaani akavunja mahusiano. Kifupi tu yule msichana wa mtaani sio kuwa nilimpenda. Si mnatambua ndugu zangu kuwa...
Replies
17
Views
587
Wakuu ni uwakika? Mimi niko gud Mungu ni mwema. Sasa wandugu mimi nalileta kwenu jambo hili rafiki yangu alinishirikisha ili nimpe maushauri.. Jamaa yangu ana mke wake na amebahatika kupata ujauzito una miezi kama sita sasa, katika miezi yote ya ujauzito mambo yalikua sawa kabsa, ila kwanzia...
Replies
12
Views
318
Afya ni afya wote tutakufa . Salama ndugu zangu , jana jioni sana nilikuwa natoka maeneo yangu ya kujidai , vijana wanasema wenyewe , ghafla bin vuu nakutana na mchungaji mmoja ambaye kwa muonekano ni kuwa hali ya maisha imempiga bado sadaka hazijaleta baraka . Salamu nyingi na kunikaribisha...
Replies
8
Views
309

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom