Mungu anakua wapi wakati unapitia shida? MAJIBU haya hapa👇

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,897
Reaction score
3,986
Points
113
Nawasalim wote!✋👋
Mtu wa Mungu jifunze kuona uwepo wa Mungu katika taabu unayo pitia, katika mazingira yote tafuta kuona uwepo wa Mungu, kwani kama utakua kila wakati unaona tu matatizo na taabu bila kujaribu kutafuta kumuona Mungu utabaki katika taabu siku zote..

Mungu anakutizama kama mtu wa tofauti lakini wewe unajiona kama mtu wataabu, duni nk...
Usiipe shida unayopitia nafasi ya kukushape au kukupa jina, usiruhusu hali au mazingira au mfumo ukakupa jina (masikini, mgonjwa, mtumwa, tasa,nk)

Mungu anakujua kwa jina lako la ushindi kuwa wewe ni mzima, shujaa, mshindi, tajiri. nk ni wakati sasa wa wewe kuboresha usikivu wako, ili uweze kutambua uwepo wa Mungu katika shida yako.

Jua kwamba popote uendapo, yuko pamoja nawe!
Inaendelea👇
 

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,897
Reaction score
3,986
Points
113
mifano katika biblia👇👇

Waamuzi 6:12
Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa.
Kwa mstari huu wa biblia tunaona Gideoni anaitwa shujaa, kama ilivo kwako mwana KF wewe ni shujaa kwa Mungu, bila kuangalia unapita katika hali na mazingira gani, unatakiwa ukubaliane na uo ukweli ili maisha yako ya badilike...

Ila ukiangalia mstari unaofata utagundua kua Gideoni mwenyewe alikua haoni kua ni shujaa kama malaika anavomuona, alijiona, mnyonge, mtumwa, mwoga, na duni na akamtupia lawama Mungu...

Waamuzi 6:13
Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye Bwana, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.
 
Last edited:

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,897
Reaction score
3,986
Points
113
Danieli 3:23-25
23 Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto.


24 Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme.


25 Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.

Mfano huu unatosha tu kusema hata pale unapokua katika moto usione moto tu, mfalme aliona watu wanne katika tanuru na alitupa watu wa tatu, Kwanzia sasa tafta kumwona Mungu katika kila jambo...
Uwe na siku njema mwana kijiji Mwenzangu
 

mshamba_mkuu

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
1,563
Reaction score
4,525
Points
0
bandiko zuri....

ila naomba kuuliza, kama kwa Mungu kila mtu ni shujaa, shida zote ni za muda tu, kwanini kuna watu wanakufa kwenye shida?? ina maana Mungu amepanga waje duniani kuteseka?? kila mtu anamuomba Mungu apate maisha mazuri, lakini ni wachache sana wenye hayo maisha mazuri. Kwanini??
 

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,897
Reaction score
3,986
Points
113
bandiko zuri....

ila naomba kuuliza, kama kwa Mungu kila mtu ni shujaa, shida zote ni za muda tu, kwanini kuna watu wanakufa kwenye shida?? ina maana Mungu amepanga waje duniani kuteseka?? kila mtu anamuomba Mungu apate maisha mazuri, lakini ni wachache sana wenye hayo maisha mazuri. Kwanini??
Asante kwa maswali yako...
kwanza kabsa ni kweli watu wote ni mashuja(washindi) mbele za Mungu...
1: Kwanini watu wanakufa na shida au mungu kapanga waje kuteseka?

Mungu alipo umba dunia aliweka utaratibu katika kila jambo, na lengo la Mungu kwa wanadamu sio waishi maisha ya kuteseka,
kila tatizo unalo liona lina jibu lake kwa Mungu, ila tatizo ni uelewa wa watu juu ya majibu ya matatizo yao kutoka kwa Mungu...

mfano aliye tengeneza simu ameitengeneza kufanya kazi mbalimbali kupiga, text, calculator, touch,nk.. na maelekezo ya jinsi yakutumia yako kwenye user manual, kwahyo ukishindwa kutumia calculayor sio shida ya alie itengeneza bali wewe ulie shindwa kufata maelekezo... mstari unao sapoti hoja yangu👇👇

Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
 

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,897
Reaction score
3,986
Points
113
bandiko zuri....

ila naomba kuuliza, kama kwa Mungu kila mtu ni shujaa, shida zote ni za muda tu, kwanini kuna watu wanakufa kwenye shida?? ina maana Mungu amepanga waje duniani kuteseka?? kila mtu anamuomba Mungu apate maisha mazuri, lakini ni wachache sana wenye hayo maisha mazuri. Kwanini??
2: kila mtu anaomba maisha madhuri kwanini wachache wanafanikiwa?

Mungu hana upendeleo, kwamba apange huyu atoboe maisha huyu, asitoboe... Nooo...
Warumi 2:11 kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu...
Ili kufanikisha jambo lolote lazima ufate utaratibu, sasa watu wengi hawafati utaratibu walio ekewa wa kimungu wanataka kufuata akili zao,
kuomba kufanikiwa ni sahihi lakini pia kuna mambo mengine ya kufata pia...
 

mshamba_mkuu

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
1,563
Reaction score
4,525
Points
0
kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu...
ndio ana upendeleo....

angalia sehemu mbalimbali kwenye dunia.... ulaya, marekani wana uafadhali wa maisha, njoo huku africa....

anampa tajiri mwenye nacho zaidi afu anamuacha maskini anakufa kwa njaa....

halafu utaskia 'sababu zake hazijulikani'
 

Urban Edmund

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 26, 2023
Messages
636
Reaction score
1,321
Points
0
mamilioni ya watu wasio na hatia wanakufa kwa magonjwa, kukosa chakula, vita.... kuna uelewa gani unahitajika hapo??

kwanini yeye asiingilie kati

ndio ana upendeleo....

angalia sehemu mbalimbali kwenye dunia.... ulaya, marekani wana uafadhali wa maisha, njoo huku africa....

anampa tajiri mwenye nacho zaidi afu anamuacha maskini anakufa kwa njaa....

halafu utaskia 'sababu zake hazijulikani'
Mwamba huyu apa
 

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,897
Reaction score
3,986
Points
113
mamilioni ya watu wasio na hatia wanakufa kwa magonjwa, kukosa chakula, vita.... kuna uelewa gani unahitajika hapo??

kwanini yeye asiingilie kati
Aingilie kati? mbona alishamaliza kila kitu,,,,
bado tutarudi tu palepale uelewa wa watu ndio unasababisha wapitie hayooo...
Kila tatizo linaufumbuzi wake, ni kazi kwa wanadamu kufata utaratibu... soma hapaa👇

Zaburi 115:16
Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.
 

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,897
Reaction score
3,986
Points
113
ndio ana upendeleo....

angalia sehemu mbalimbali kwenye dunia.... ulaya, marekani wana uafadhali wa maisha, njoo huku africa....

anampa tajiri mwenye nacho zaidi afu anamuacha maskini anakufa kwa njaa....

halafu utaskia 'sababu zake hazijulikani'
Mungu hana upendeleo, hao unaowasema wameweka jitiada katika kutumia vitu walivo pewa... na kitu kingine ukiwa masikini sio kigezo cha kuonewa uruma, kufata utaratibu ndio namna pekee yakuepukana na madhila yote
 

Muhindi Wa Kuchoma

Well-known member
Platinum Villager
Joined
Jul 9, 2023
Messages
3,821
Reaction score
3,805
Points
113
mshamba_mkuu unaamini uchawi upo?
Je unaamini kuna watu wanachukuliwa misukule?
Je unaamini watu wanapandisha majini?
Je kuna vinyamkera? vibwengo? majini?nguva?
 

Similar threads

Heri ya mwaka mpya 2024 Villagers... Nipo kitandani tangu juzi mwili umepata hitilafu za kiafya kidogo ndo nipo naupambania hapa, hopefully ntakuwa sawa ASAP! Straight to the point, hii forum forum yetu bafo inajitafuta lakini binafsi mimi ishanitendea makuu mno 🤣🤣🤣. Sijawahi juta kuwa...
Replies
22
Views
734
Ni mwaka mpya ninafurahi kwa kila ambaye atasoma uzi huu ujue umeundwa kwa ajili yako Wewe utesekaye na kulemewa mwilini hadi rohoni basi leo miujiza ya Mungu itakuwa pamoja nawe Swali kuu ni umewahi muhisi na kuisikia sauti ya Mungu wako, umewahi omba hapo hapo likatendeka? Mungu wako si...
Replies
1
Views
431
Wapendwa nawasalimu.🙋 Nakupongeza kwa kuamua kufungua na kusoma uzi huu, Karibuuu... Ni mambo mengi mabaya na magumu na yakukatisha tamaa yametupata, hatungekuwa hapa leo kama sio kwa msaada wa Mungu. Uwezo huo wa kuweza kumudu hali ngumu na mbaya katika maisha na kuweza kusimama, baada ya...
Replies
1
Views
402
Nawasalimu, alafu moja kwa moja kwenye mada. Mungu amekuwa akikuonyesha kibali kila siku, je, unashukuru vya kutosha kwa kuona hivyo? Je, unaweza kuona hata ishara ndogo kabisa ya uaminifu Wake katika maisha yako? Siri ya kuwa na maisha utele ni kushukuru...... Yesu alipoinua ile mikate 5...
Replies
6
Views
402
Afya ni afya wote tutakufa . Salama ndugu zangu , jana jioni sana nilikuwa natoka maeneo yangu ya kujidai , vijana wanasema wenyewe , ghafla bin vuu nakutana na mchungaji mmoja ambaye kwa muonekano ni kuwa hali ya maisha imempiga bado sadaka hazijaleta baraka . Salamu nyingi na kunikaribisha...
Replies
8
Views
309

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom