Mzazi wangu hataki kunisamee

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,883
Reaction score
3,969
Points
113
Wakuu kwema?
Mimi ni kijana wa kiume umri miaka 26, ni mtoto watatu katika familia ya watoto wa 5, mwaka huu namaliza chuo maswala ya misitu.

Baba yangu ni mstaafu alikua ni mwalimu wa chuo (lecturer) Chuo cha maendeleo ya jamii, mama yeye alikua anajishughulisha na mashirika ya kusaidia watoto, ila kwa sasa yuko tasaf, dada yangu mkubwa kaolewa ni mwalimu na kaka yeye ni dereva wa haya ma greda, na wadogo zangu bado wanasoma wawili.

Kilichofanya niandike hapa ni kwamba ilitokea issue hapa home, mzee wangu ni mtu wa wanawake sana, kwanzia tukiwa wadogo alikua ni mtu wamakesi na ugomvi kwaajili ya mambo yake haya ya wanawake(michepuko) yaani mpaka tumemzoea.

Ilifikia hatua mpaka wadada wa kazi wakawa nyumbani ni mwiko maana alishawai mbebesha binti wa kazi mimba, yani nikama ufahamu wake umefungwa kwenye mambo hayo kwa maana ni yeye na wanawake na pombe..

Sasa kwanzia mzee astahafu aliama nyumba akawa amepangisha na mwanamke mmoja na wana mtoto nae, nyumbani alikua anakuja mara moja au mbili kwa mwezi ili lilikua alina shida kwakua tulisha mzoea.

Mwezi wa tisa mwaka jana nlikua likizo cha ajabu tunashangaa fuso linakuja na ma vyombo, vitanda kabati, sofa, kumbe ni mzee kakorofishana na mke wake(mchepuko), akaja akaingiza vitu store na vingine ndani, akuongea na mtu.

Jioni akamleta na yule mtoto wake wa nje, wakawa wana kaa nae kwenye chumba cha wageni, uyu dogo ana miaka kama sita hvi, ni mchangamfu ilitokea familia yote ilimpenda hadi mama.

Kwa ufupi mambo yalikuja kuaribika baada ya mzee kupatana na yule mchepuko wake akawa anakuja nae mpaka home kumsalimia mtoto wake, sasa wakati anakuja kumbe alikua amampiga mama yangu vijembee..

Mimi sikujua maana nakuaga mishe mchana, kuna siku nikapigiwa simu na wadogo zangu kuwa mama yuko hospital, nikawai nkakuta kawekewa maji(drip) bahati nzuri anakuwaga na bima.

Alikuwa na presha baadae nlipo pata mda wa kuongea nae nikamuuliza unawaza nini mama akasema amna chochote, akaja akaruhusiwa fresh tukarudi home, nikamua nikae tu nisiende tena popote.

Wakati niko nyuma ya nyumba naanua nguo, ndio nasikia mama anaongea na simu kuna ndugu yake amempigia kutoka huko rombo, mama akawa anamueleza mambo yanayo msibu hapa nyumbanirfhfaw, yule mchepuko amemtukana matusi yote, na anakujaga hapa nyumbani anaanza kukagua kila kona, na ameleta dada wa kazi wa kukaa na mtoto wake, huyu dada wa kazi nae anamuonesha dharau, utafikiri ni rika lake..

Yaani nilivo skia vile mwili ulikua kama umepigwa shoti, nilinyooka kwa yule beki tatu, nkamwambia kusanya nguo zako zotee, akawa anielewi nikamla vibao viwili akashika njia ndani akakusanya nguo, nikampa nauli ya basi na hela ya gest, nkamwambia staki kumuona pale..

Mzee nkampigia simu nkamwambia kwa uzuri naomba jioni ukija tuongee akauliza kuna shida nkamwambia ndio..

Jioni akaja na jazba sana, akaanza kumpandishia maza matusi, na anajua anaumwa wala hakujali.

Nikaja nikamshika mkono nkatoka nae nje, nkamwambia maza ni mgonjwa, na unajua maana tulikupigia simu tukakueleza ila hata hospital hukuja.

Pili mama hana kosa mimi ndio nimemfukuza yule binti(sababu nikampa) nikamwambia hapa ni nyumbani na maza amepambana sana miaka yote tuwe na familia bora, na anamchango mkubwa katika familia hii, haiwezekani ulete mchepuko aharibu kitu huyu mama alipambania miaka yote, sasa hv ni mda wake wakupumzika, kama ni mchepuko wako sisi hatuna shda nae ila asiwe sababu ya kifo cha mama yangu..

Kama ulivokua nae huko unaweza kurudi hukohuko mkaishi nae, ila sio kuchanganya familia, dogo ni mtoto wetu yeye hana shida kila mtu anampenda, kwahyo nakuomba mkanye uyo mke wako mdogo aachane na familia hii, iliwezekana mkapangishe kama mlivokua mmepangisha ili muishi kwa amani.
Mzee akawa ameelewa ila cha kishangaza kesho wakati siko akaja na yule mchepuko, yule mchepuko anataka hati ya nyuma eti kwasababu tunataka kumuua mume wake, ameingia anasachi kila maali amepavuruga.
 
Last edited:
Nkapigiwa simu nikaja yule dada aliponiona aliingia kwenye gari akalock, nkaingia ndani namkuta maza yuko chini ameanguka analia, alafu mzee hana time nae, sijui hasira zilitoka wapi ila nlijikuta nmemrukia mzee nilichomoa mkanda nilimpiga mikanda ya kutosha, nilimuwasha vibao, maza akawa anapiga ukunga(yowe) kuomba msaada maana alijua na muua mme wake.

Nikampa masaa 24 ya kumuona pale nyumbani, kweli kesho akabeba vitu vyake akasepa..

Baada ya siku kama mbili mama akawa ataki hata kuniona anadai nmefanya jambo baya kumpiga baba yangu, ila sikujali chochote.

Baada ya mda kupita nlimuomba msamaa mama akanisamee, ila kivumbi kiko kwa mzee nimetuma na wazee, wachungaji, marafiki zake nimempigia simu ili tuyamalize maana nilifanya jambo lisilo la kiuungwana, lakini mzee hataki kabsa yeye kauli yake ni moja kuwa akipata nafasi atawaambia ili mambo yawekwe sawa.

Ila mpaka leo ajawatafta wazee ili tumalize, wazee wamekua wakimkumbushia ila anasema hana mda...

Je nifanye nini wadau maana nmechoka kwa kweli
 
Endelea kutafuta suluhu na mzee, akigoma kabisa basi achana nae

Tatizo mnaamini kwenye mambo ya laana, sijui kama utanielewa

Ila sioni kama umekosea popote
 
Kuna namna unaomba msamaha kiutu uzima. Zamani kama mtu hataki kukusamehe unafanya hivi

1. Kama ni mama unapiga magoti na kushika maziwa yake. Lazima atakusamehe asipokusamehe atapata tabu sana

2. Kama ni mwanaume unamshika kwenye uvungu wa korodani nje ha suruali atakusamehe

3. Kama ni mchaga unamwendea na ISALE wachaga tunaliogopa like jani sana, atakusamehe tu kilazima

Ila msamaha una nguvu sana. Kuishi na vinyongo ni kitu kibaya. Ila alichofanya mzee ni unyama sana. Alistahili makofi, heshima kwa mwanamke ni kitu cha kuthaminiwa.

Kama amekosa huruma kwa mwanamke tena mke wake, aside muua kwa presa. Mchepuko akichukua hati hapo basi
......
 
Huyo mchepuko angekuwa Dar mbona tungemfanyia mchezo ambao asingeweza kusahau.

Siku mzee atapomletea maza mchepuko siku hiyo nahesabu sina baba. Mambo yake ya kihuni akafajye huko sio nyumbani kwa mazaa.
 
Hakimu wewe umeokoka na uko na Yesu. Biblia inasemaje kuhusu hili swala
Tukiweka mbali biblia huyo mzee alistaili ngemtoa hata jino ili hata baada ya kupatana abaki na ukumbusho dogo alinizubua baada ya kufanya hivi

Inshort angetuliza hasira angeenda kwenye gari na rungu vunja vioo vyote vuta huyo mly nje piga piga mpaka akama alafu unarudi ndani unamkwida mzee suruali kwa nyuma (kama afande anasukuma mwizi) kisha unatupia nje unafunga mlango na onyo kali mwisho leo kesho nisikute vitu vyao la sivyo navitaifisha

kibiblia bwana kakosea ila kiubinadamu yuko right
 
Kuna namna unaomba msamaha kiutu uzima. Zamani kama mtu hataki kukusamehe unafanya hivi

1. Kama ni mama unapiga magoti na kushika maziwa yake. Lazima atakusamehe asipokusamehe atapata tabu sana

2. Kama ni mwanaume unamshika kwenye uvungu wa korodani nje ha suruali atakusamehe

3. Kama ni mchaga unamwendea na ISALE wachaga tunaliogopa like jani sana, atakusamehe tu kilazima

Ila msamaha una nguvu sana. Kuishi na vinyongo ni kitu kibaya. Ila alichofanya mzee ni unyama sana. Alistahili makofi, heshima kwa mwanamke ni kitu cha kuthaminiwa.

Kama amekosa huruma kwa mwanamke tena mke wake, aside muua kwa presa. Mchepuko akichukua hati hapo basi
......
Huyo mzee ndo kakosea

Ila mila zingine za kijinga, mzazi hataki kukubali kakosea eti ananuna
 
Huyo mzee ndo kakosea

Ila mila zingine za kijinga, mzazi hataki kukubali kakosea eti ananuna
Haya mambo tuyazungumze kama yalivyo

Kuna shemeji yangu kabla hadaway shemeji alikuwa mshikaji wangu wa damu sana. Yule jamaa huwezi amini wakati huo mzee wake hajawahi hata kuhangaika na maisha yake ya shule, alipambaniwa na watu wengine

Mzee wake alipoteza mda na mabahamedi tu. Kunywa na kuwala mabahamedi. Iko siku wakati mfadhili wake mkubwa (baba wa ubatizo) alifariki na jamaa hakuweza kumaliza chuo mwaka wake wa tatu

Alipomcheki mzee wake ampoge tafu hata ada amalize mzee kagoma. Jamaa alikuwa anaropoka tu " we mzee mseng@ sana". Kisha akaenda zake

Lile tusi lilimkaa jamaa mwisho akashauriwa akaombe msamaha. Jamaa akaenda kuomba msamaha. Too bad mzee akawa hataki kuzungumza nae. Akaja tuma wazee wengine wakambembeleze mzee wake

Mzee akakubali ila sharti amletee mbuzi wa kuomba msamaha. Jamaa ikabidi afanye hivyo na swala likapita.

Hasira hasara ila imishatokea imetokea. Binafsi inamuathiri kijana kuliko mzee wake.
 
Kuna namna unaomba msamaha kiutu uzima. Zamani kama mtu hataki kukusamehe unafanya hivi

1. Kama ni mama unapiga magoti na kushika maziwa yake. Lazima atakusamehe asipokusamehe atapata tabu sana

2. Kama ni mwanaume unamshika kwenye uvungu wa korodani nje ha suruali atakusamehe

3. Kama ni mchaga unamwendea na ISALE wachaga tunaliogopa like jani sana, atakusamehe tu kilazima

Ila msamaha una nguvu sana. Kuishi na vinyongo ni kitu kibaya. Ila alichofanya mzee ni unyama sana. Alistahili makofi, heshima kwa mwanamke ni kitu cha kuthaminiwa.

Kama amekosa huruma kwa mwanamke tena mke wake, aside muua kwa presa. Mchepuko akichukua hati hapo basi
......
Msamaa unausihana nini na kushika sehemu nyeti?
Changamoto ni namna ya kukutana na uyo mzee..
alafu anaweza hisi nataka mpiga tena
 
vijana wanapitia mambo mengi jaman
Haya mambo tuyazungumze kama yalivyo

Kuna shemeji yangu kabla hadaway shemeji alikuwa mshikaji wangu wa damu sana. Yule jamaa huwezi amini wakati huo mzee wake hajawahi hata kuhangaika na maisha yake ya shule, alipambaniwa na watu wengine

Mzee wake alipoteza mda na mabahamedi tu. Kunywa na kuwala mabahamedi. Iko siku wakati mfadhili wake mkubwa (baba wa ubatizo) alifariki na jamaa hakuweza kumaliza chuo mwaka wake wa tatu

Alipomcheki mzee wake ampoge tafu hata ada amalize mzee kagoma. Jamaa alikuwa anaropoka tu " we mzee mseng@ sana". Kisha akaenda zake

Lile tusi lilimkaa jamaa mwisho akashauriwa akaombe msamaha. Jamaa akaenda kuomba msamaha. Too bad mzee akawa hataki kuzungumza nae. Akaja tuma wazee wengine wakambembeleze mzee wake

Mzee akakubali ila sharti amletee mbuzi wa kuomba msamaha. Jamaa ikabidi afanye hivyo na swala likapita.

Hasira hasara ila imishatokea imetokea. Binafsi inamuathiri kijana kuliko mzee wake.
 
Haya mambo tuyazungumze kama yalivyo

Kuna shemeji yangu kabla hadaway shemeji alikuwa mshikaji wangu wa damu sana. Yule jamaa huwezi amini wakati huo mzee wake hajawahi hata kuhangaika na maisha yake ya shule, alipambaniwa na watu wengine

Mzee wake alipoteza mda na mabahamedi tu. Kunywa na kuwala mabahamedi. Iko siku wakati mfadhili wake mkubwa (baba wa ubatizo) alifariki na jamaa hakuweza kumaliza chuo mwaka wake wa tatu

Alipomcheki mzee wake ampoge tafu hata ada amalize mzee kagoma. Jamaa alikuwa anaropoka tu " we mzee mseng@ sana". Kisha akaenda zake

Lile tusi lilimkaa jamaa mwisho akashauriwa akaombe msamaha. Jamaa akaenda kuomba msamaha. Too bad mzee akawa hataki kuzungumza nae. Akaja tuma wazee wengine wakambembeleze mzee wake

Mzee akakubali ila sharti amletee mbuzi wa kuomba msamaha. Jamaa ikabidi afanye hivyo na swala likapita.

Hasira hasara ila imishatokea imetokea. Binafsi inamuathiri kijana kuliko mzee wake.
Mila za kipuuzi mno.

Ila kadri watu wanavyozidi kustaarabika, zitaisha tu.
 
Japo mimi na baba yako ni kopo na mfuniko upande fulani ila isinininyime uhuru kusema baba yako ni mjinga sana , ila pole sana mwanangu .

Sikushauri kuendelea kumuomba msamaha mzee wako maana kwa akili aliyonayo kumuomba msamaha ni kama kumuomba arudie anayofanya ila wewe uwe kimya kwa minajiri ya baba na kuogopa laana .

Son, hakuna laana ya baba mjinga wa namna hiyo , nikuombe kuendelea na maisha yako ila kikubwa jua ulichofanya ndiyo kitaebdelea kumlinda mama yako kwa wakati huu .

Note : presha ni mbaya , presha inauwa , kubali kuonekana mtovu wa nidhamu na mwingi wa jazba ila mama yako aishi kwa amani na furaha .
 
Shukran
 
Similar threads

Watu wengi wameendelea kuzungumzia suala la maadili, hasa kwa vijana. Kwa mfano hili wimbi la panyarodi linaloendelea kutajwa kwa vitendo viovu, hii ni miongoni mwa sababu kubwa ya mmomonyoko wa maadili. Inaonekana dhahiri baadhi ya wazazi wameshindwa kutimiza jukumu la malezi ya watoto wao...
Replies
10
Views
176
Habari na karibu ktk moja na mbili ya kuelimishana sisi kama mavijana. Tabia zako zina athari kubwa mahali pesa zako zinakwenda. Pesa haiwezi kamwe kuzidi mikononi mwa mtu mwenye tamaa ya kutumia hela tu. Jifunze kuwa na ujuzi wa kifedha. Usiwe na haraka ya kukimbia wakati haujajifunza...
Replies
9
Views
424
Mficha maradhi kifo humumbua, nateseka naumia sana toka niachane na ex wangu. Tulikuwa na uhusiano miaka 2 iliyopita, baada ya kufuma message WhatsApp namtongoza msichana mmoja hivi mtaani akavunja mahusiano. Kifupi tu yule msichana wa mtaani sio kuwa nilimpenda. Si mnatambua ndugu zangu kuwa...
Replies
17
Views
585
Wakuu ni uwakika? Mimi niko gud Mungu ni mwema. Sasa wandugu mimi nalileta kwenu jambo hili rafiki yangu alinishirikisha ili nimpe maushauri.. Jamaa yangu ana mke wake na amebahatika kupata ujauzito una miezi kama sita sasa, katika miezi yote ya ujauzito mambo yalikua sawa kabsa, ila kwanzia...
Replies
12
Views
318
Afya ni afya wote tutakufa . Salama ndugu zangu , jana jioni sana nilikuwa natoka maeneo yangu ya kujidai , vijana wanasema wenyewe , ghafla bin vuu nakutana na mchungaji mmoja ambaye kwa muonekano ni kuwa hali ya maisha imempiga bado sadaka hazijaleta baraka . Salamu nyingi na kunikaribisha...
Replies
8
Views
309
Back
Top