Wasalaam
Toka niingie madarakani na kuwa Raisi wa KijijiForums nimepata sonona sana. Kwa nini?
Nimepata sonona kutokana na majungu ya watu humu ndani na nje ya hapa. Kwa sababu nimekuwa nikitwa majina ya ajabu ajabu ila leo mwana kijiji kunifata PM na kuniita Mama Samia nikavunga akaendelea mama huyoo. Hizi si dharau kabisa ??? mwanaume unaitwaje mama?
Kuna wengine wananiita kwa kebei kabisa kama huyu
@AlmightyGod na
@mshamba_mkuu . Utawasikia raisiiiiii, prezidaaa, muheshimiwaa, Mzee wa michongo, kipipa, tumbo, Jiwe, Kitiii (nadhani wanamaanisha
). Kuna mtu kwenye thread zake ananitag kitii kimezungumza
Hata mke wangu nyumbani baada ya kumweleza sasa mimi ni raisi wa KijijiForums na yeye ni first lady naona majungu yamezidi. Baada ya kuniomba jambo lake nikamkatalia. Asubuhi hii hakuniamsha niwahi kazini namuliza kwa nini hukuniamsha? anasema kaniamsha sana sema mimi ni raisi mlala hoi
si dharau hizi?
Sasa heshima ni kitu ya bure kwa wale wanaoendeleza utani mnanichukulia kuwa mimi ni "mwana" mtajua hamjui kuwa kama mimi ni "mwana haramu (pig
)" au "mwanahamisi - mama raisi".