Raisi wa awamu ya pili Tanzania, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Muhindi Wa Kuchoma

Well-known member
Platinum Villager
Jul 9, 2023
3,787
3,770
113
Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amefariki leo, Februari 29, 2024 saa 11:30 Jioni katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.

Tangu Novemba 2023, alikuwa anapatiwa matibabu huko London, Uingereza na baadaye kurejeshwa nchini kuendelea na Matibabu katika hospitali ya Mzena hadi leo ambapo amepatwa na mauti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo kuanzia Machi 1, 2024, bendera zitapepea nusu mlingoti.

Atazikwa Machi 2, 2024 Unguja, Zanzibar.20240229_200102.jpg

Ali_Hassan_Mwinyi.jpg

Mwinyi, Ali Hassan alizaliwa May 8, 1925 in Dar es Salaam, Tanzania. Mtoto wa Hassan and Asha Sheikh Mwinyi, Ali Hassan Mwinyi.

Alipata Diploma kutoka Chuo Kikuu cha Elimu ya Watu Wazima, Dublin Uingereza kati ya 1954-56. Mhe. Mwinyi kitaaluma ni mwalimu, alifundisha shule za Msingi Mangapwani na Bumbwini Zanzibar. Zaidi, Mhe. Mwinyi ana cheti cha umahiri katika Lugha ya Kiingereza alichopata katika Taasisi ya Regent, Uingereza mwaka 1960 na Cheti cha Umahiri katika Lugha ya Kiarabu alipata Cairo, Misri mwaka 1972-74.

Mhe. Ali Hassan Mwinyi alijiunga na Afro Shiraz Party (ASP) mwaka 1964 na kushika nyadhifa tofauti za Serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ya Zanzibar mwaka 1963. Mwaka 1970 alikuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais. Ofisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kati ya 1982-83 alikuwa Waziri wa Afya, Mambo ya Ndani, Maliasili na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri kuanzia mwaka 1977 hadi 1982.


Historia fupi ya mzee Mwinyi
Mwaka 1983 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais na mwaka 1984 alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sehemu hii inakuletea baadhi ya hotuba alizozitoa wakati wa uongozi wake.
 

Similar threads

Raisi Samia amvua DKt Wilbroad Slaa hadhi ya ubalozi kuanzia leo Septemba 1, 2023. Taarifa imetolewa hivi punde na Ikulu katika mtandao wa kijamii wa X. Dk Wilbroad Slaa aliwahi kuwa Katibu wa Chadema Taifa na baadaye Balozi wa Tanzania nchini Sweeden. Dk Slaa alipewa hadhi hiyo mwaka 2017.
Replies
4
Views
266
Nina maana ukipata watu 20 au 30 kila siku mtu mmoja anatoa 5000 au 10000 na kila siku mtu mmoja anatoka. Siitatusaidia kidogo kupambana na maisha. Wewe ni prezidaa uwezi kimbia ukaacha app
Replies
102
Views
2K
Top Bottom