Rich Communication Services (RCS) Technology ya kutuma SMS bila kifurushi

Robot

Robot
Joined
Sep 9, 2023
Messages
42
Reaction score
15
Points
8
Ifahamu Rich Communication Service (RCS) Ambayo hutoa Huduma ya utumaji SMS na MMS Kwa kutumia data au WiFi.

Umewahi kujiuliza utachat vipi na mtu ambaye mda huo ameishiwa SMS na Ikumbukwe ili nyote mchati Kwa sms lazima Wote muwe na kifurushi, Sasa fikiria una sms lakini Rafiki Yako Hana kifurushi cha SMS na mbaya zaidi Huenda hatumii Mitandao mingine kama kijijiforums, WhatsApp, Facebook au Instagram Sasa Google wametuletea Huduma ya utumaji wa ujumbe wa SMS na MMS Kwa kutumia data au WiFi yaani haihitaji kuwa na kifurushi cha SMS tunaweza sema RCS ni WhatsApp iliyo changamka Maana baadhi ya features za WhatsApp Zipo kwenye Mfumo huu wa RCS kama vile grey tick, blue tick, typing, kutumia faili na Picha.


Faida za RCS ni kwamba hutoa utumiaji ulioboreshwa na mzuri wa utumaji ujumbe.

Huduma hii ya Mazungumzo au Soga za RCS: Huonyesha mtu anapoandika, hutoa alaza ujumbe unapo somwa au kufiki kwa muhusika yaani ni kama utumaji wa WhatsApp Message Alama za kusoma ambazo huonyesha wakati mtu amesoma au kupokea ujumbe wako.
Alama za kusoma (Read receipt) pia zinaonyesha mtu unayewasiliana naye unaposoma ujumbe wako.

Huduma hii ya RCS hutuma ujumbe kupitia data ya mtandao wa simu na Wi-Fi yaani haikuhitaji kuwa na kifurushi cha kawaida Cha maongezi au sms
Huduma hii huruhusu ushiriki faili na picha za ubora wa juu yaani Kwa kutumia MMS unaweza mtumia mtu faili au Picha Kwa kupitia App ya Message Unapotumia gumzo za RCS, jumbe zako hutumwa kwa itifaki ya Huduma za Mawasiliano Mapya (RCS) kupitia Wi-Fi na data ya mtandao wa simu.

Soga za RCS zitawashwa tu wakati washiriki wote kwenye mazungumzo wana RCS. Soga za RCS hutolewa na Google au mtoa huduma wako wa simu.

Rich Communication Services (RCS) zinapatikana kwenye vifaa vya Android. Programu ya Messages kwenye Google hukujulisha wakati ujumbe wako umetumwa, kupokelewa, na kusoma aikoni zilizo karibu na ujumbe wako

Muhimu: Aikoni hizi zitaonekana kwenye ujumbe wa SMS au MMS.

Kipima muda (Alama ya saa) : Ujumbe wako unatumwa Hii alama itaonekana pindi unapo tuma ujumbe.

Cheki moja(one tick) : Ujumbe wako umetumwa Alama hii itaonekana kama ujumbe wako umetumwa.

Tick mbili(double tick) : Ujumbe wako umewasilishwa Hapa ujumbe wako unapo fika basi alama hii itaonekana.

Tick Mbili zenye rangi(Blue Tick) : Ujumbe wako umesomwa Mhusika anapo soma ujumbe wako basi tick hizi Mbili zitaonekana.

Kielelezo pichani Jinsi tick hizo huonekana

1702143107396.png

Unapotumia gumzo za RCS, ujumbe wako hutumwa kupitia Wi-Fi na data ya mtandao wa simu.

Maadamu umeunganishwa kwenye mtandao wa Wi-Fi ambao huhitaji kulipa ili kutumia, haipaswi kuwa na gharama ya kutuma na kupokea ujumbe (bando).

Ikiwa ujumbe wako utatumwa kwa kutumia data ya mtandao wa simu, gharama inategemea mpango wako wa data ya mtandao wa simu yaani kiufupi inakuhitaji uwe kwenye muunganisho wa Mtandao.

Google inaweza kuthibitisha nambari yako ya simu mara kwa mara kupitia SMS ili kutoa gumzo za RCS (huenda ukatozwa ada za SMS).

Jinsi ya Kutumia RCS
RCS Itawezeshwa Wakati waasiliani wote wanatumia RSC yaani hapa inahitaji Wote muwe mnatumia Huduma hii na Hapo mnaweza tumiana SMS hata kama Hauna kifurushi cha sms

Kama hauna Google Messages, idownload Play Store.
Baada ya Hapo itakuomba kujaza namba yako kama Sehemu ya RCS chats setup.
RCS chats inaweza kuzimwa au kuwashwa Wakati ukibonyeza kwenye Messages settings Harafu general settings then RCS chats Hapo ndipo unaweza kuwasha au kuzima Huduma hii.
Pia Kwa wanao humia Message ya kawaida Kwa Watumiaji wa Android unaweza update Message App yako Kisha utapata feature ya RCS Chat Bila Shaka wengi mlio download au kuupdate mmekutana na features Mpya basi na RCS imejumuishwa humo.

Ikumbukwe Rich Communication Services (RCS) Kwa Sasa inapatikana Kwa Watumiaji wa Android pekee.
 
Shukran kwa taarifa, hii itakua ngumu kuingiliwa kama whatsapp dhidi ya Gb whatsapp na zinginezo?
 
Shukran kwa taarifa, hii itakua ngumu kuingiliwa kama whatsapp dhidi ya Gb whatsapp na zinginezo?
Huku kunaweza kuwa na api so developers can develop their own apps with this feature
 
Natabiri hapo baadae kutakuwa na free WiFi and sending messages will totally br free
 
Natabiri hapo baadae kutakuwa na free WiFi and sending messages will totally br free
Free wifi, free school fee, free health insurance, free transport cost, free lunch, is inevitable in freeworld(666)
 

Similar threads

  • Article Article
My life was turned upside down when I found out my father was a rich man. Growing up on the poverty line, I worked tirelessly to afford a college education, even doing my classmates' laundry to save up for a special gift for the girl of my dreams. However, my world came crashing down when I...
Replies
27
Views
923
Habari wanakijiji... Napenda kuchukua fursa hii kukukaribisha mwanakijiji mwenye uhitaji wa ukumbi kwa ajili ya sherehe mbalimbali kama WEDDINGS, SEND OFF, KITCHEN PARTIES & OTHER CEREMONIES at BARACUDA HALL FOR EXECUTIVE SERVICES... Ukumbi unapatikana Dar Es Salaam, Tabata Baracuda uelekeo wa...
Replies
31
Views
336
Back
Top