- Jul 8, 2023
- 195
- 704
- 0
Afya ni Afya wote tutakufa .
Wanakijiji habari zenu , Mimi najua waliowengi kwa wanakijiji mmesafiri vijijini na mijini , leo mwenzenu naikumbusha tena serikali kuwa hawa watu wa afya hasa kwenye hizi zahanati ni wazi kuwa wengi wao ni watabibu .
Nisichoweza kupinga ni kuwa kwenye ulimwengu wa mambo ya afya ni kuwa exprience inamatter zaidi kuliko vyeti .
Hivyo sishangai wala sikatai kuwa ukiwa mtabibu unaweza kufanya kazi ya MD endapo exprience yako ni kubwa kutokana na kuwa karibu na mtu wa taaluma hiyo japo ni kinyume na taratibu .
Sasa kutokana kuwa ni kinyume na taratibu na imefika mahali ndugu zangu wa afya huku vijijini hasa kwenye hivi vizahanati kujitwisha majukumu makubwa ambayo kiuhalisia hawana uwezo wa kumalizana na tatizo mpaka mwisho .
Natoa mfano , kwenye hivi vizahanati ni ngumu kukuta huduma ya matibabu kwa watoto wenye utapiamlo , hawaruhusiwi kumzalisha mwanamke mwenye kubeba mimba iliyo mimba ya kwanza kwake , hawaruhusiwi kumfanyia mtu yeyote upasuaji maana vifaa tiba havipo , hawaruhusiwi kutibu magonjwa sugu yoyote zaidi kazi ya wao ukifika na mojawapo ya shida tajwa watakupa referral ili uende hospitali au kituo cha afya chenye uwezo wa matibabu kwa gonjwa husika .
Sasa wao kazi yao ni ipi ?
Kwao ataenda mjamzito mwenye ujauzito wa pili na kuendelea , ataenda mtu aliyemuathirika wa Gonjwa la UKIMWI kupata ushauri na nasaha lakini pia kupewa dawa za kufubaza virusi na pia ataenda mama mjamzito kwaajili ya clinic .
Sasa imekuwa ni shida kwa hawa wataalamu hivi sasa wanavamia hata kazi wasizoruhusiwa lengo wajiingizie chochote kitu , imefika mahali watu wanaandikiwa madawa ambayo sio sahihi kikubwa bwana tabibu apate pesa .
Nimewiwa kuiomba serikali kwenye semina mbalimbali za afya na pia kutolewe muongozo kwa maandishi ili wanavijiji wajue fika kuwa kwa magonjwa yapi na yapi abaki hapo kijijini au aende mbele lakini uwe wito kwa wataalamu hawa kukumbuka kuwa kipi ni wajibu wao na kipi sio wajibu wao .
Asubuhi ya leo nimehudhuria mazishi ya binti wa miaka miwili aliyekuwa na utapiamlo ila wataalamu wa zahanati wamejikuta wanapambana kumtibu wao na mwisho wamempoteza .
Asanteni .