Simba Sports Club Special thread

KijijiForums

Official Account
KF Moderator
Joined
Jun 5, 2023
Messages
26
Reaction score
57
Points
0
Simba SC ni moja kati ya timu nne kongwe kabisa hapa nchini ikianzishwa mwaka 1936 jijini Dar es salaam. Zingine ni vinara Yanga SC 1935, African Sports 1936 na Coastal Union 1938.

Simba imepitia majina mengi toka kuanzishwa kwake mpaka sasa. Ilipoanzishwa mwaka 1936 iliitwa Queens jina lilidumu mpaka mwaka 1948 walipofanikiwa kupanda ligi daraja la kwanza na wakati huo mkoa wa Pwani ulianzisha ligi maalumu iliyokuwa ikijiendesha kwa misingi bora ya kisasa.

Wakati huu ndio Simba ilianza kupata ufadhili unaoeleweka mfano jezi nzuri za kisasa na viatu wakati wenzao wakiwa bado wakilisakata kabumbu peku peku .

Simba walibadilishwa jina na kuitwa Eagles baada ya kuonekana jina la Queens linawaletea kebehi kwa watani wao wa jadi Yanga SC ambao kabla ya mwaka 1930 walijulikana ‘ New Young ‘.

Jina la Eagles yaani tai kwa lugha ya kiswahili halikudumu sana. Lilikaa kwa muda mchache sana na kubadilishwa kuwa Sunderland.

Hili ndio jina ambalo wengi wanalifahamu sana . Ni jina ambalo wekundu hawa wa msimbazi wana kumbukumbu nalo kubwa na ndefu kidogo.

Baada ya nchi kupata Uhuru mwaka 1961 na miaka minne baadae kuanzishwa ligi daraja la kwanza yenye sura ya kitaifa yaani ligi iliyoshirikisha timu zote za bara na visiwani, Sunderland ndio ilikuwa timu ya kwanza kubeba kombe la ligi hiyo mwaka 1965 na kulitetea tena kombe hilo mwaka 1966.

Hivyo katika historia Simba SC wakitumia jina la Sunderland waliweza kunyakua ubingwa wa ligi daraja la kwanza mara mbili kabla ya jina hilo kufa mwaka 1971 baada ya raisi wa kwanza wa Zanzibar hayati Abeid Karume kuwashauri kubadili jina kwa sababu ya maudhui yake kikoloni na ndipo jina la Simba SC lilipozaliwa.

Sunderland wakitumia jina jipya la Simba SC iliwachukua miaka miwili kujipanga kurudisha makali yao katika ligi. Mwaka 1973 walitwaa tena ubingwa wa ligi daraja la kwanza ingawa waliporwa tena na Yanga 1974. Hivyo kihistoria Simba hii mpya ilitwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya kwanza mwaka 1973
 
Wana msimbazi mambo vipi?

Club ya Simba imetangaza kuwa kambi yake ya maandalizi ya msimu mpya (Pre Season) 2023/2024 itaiweka nchini Uturuki kwa muda wa wiki tatu.
 
Simba Day

Wana Simba
 
Mmyamaa

Dakika ya 6
Simba Sc 1- Power Dynamo 0
 

Similar threads

kocha mpyaaaaaaaa tutegemee makubwa wana msimbazi
Replies
2
Views
958
Naona kabisa baada ya ile sare na dynamo na kiwango Cha jumla Cha wachezaji naona kabisa Uongozi unafikia makubaliano ya pande zote mbili.. Naona kabisa
Replies
6
Views
500
Eeeeeee bwana weeee, siku tuliokuwa tunaisubiri kwa hamu na Hali na Mali ya kushuhudia msimu mwingine was mashindano, hasa baada ya Yanga kuwa na msimu mzuri uliopita Je huu utakuwa wa Nani? Ngao ya jamiii ilipigwa mechi Yanga na Azam, Yanga akaibuka kidedea kwa 2-0 Kikapigwa Tena kesho...
Replies
89
Views
936

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top