Simba yaizidi Yanga Bajeti ya msimu wa 2023/2024

Anonymous

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
515
Reaction score
143
Points
0
1687957166705.png

Klabu pendwa zaidi nchini za Simba na Yanga kila moja imeweka wazi bajeti ya msimu wake ujao katika kujiimarisha ili kutimiza malengo waliyojiwekea kwenye michuano ya Kitaifa na Kimataifa.

Simba kupitia kwa CEO wake Imani Kajula imetangaza Bajeti ya Bilioni 24 kwa msimu wa 2023/2024

”Eneo la kukuza mapato, kwa mfano Bajeti yetu ya mwaka 2023/2024 ni Bilioni 23 nadhani mlisikia za wenzetu sitaki kulinganisha, mtakumbuka. Lakini kwa nini tunaamini kwamba ni muhimu tukuze mapato kuwa timu inayoongoza Afrika kunahitaji sana fedha, kuongoza Klabu kubwa ni gharama kubwa sana kwa hiyo mapato ni jambo la muhimu sana.”- Mtendaji Mkuu Imani Kajula.

Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kutangaza bajeti yake ambapo kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Fedha, Sabri Sadick imetangaza Bilioni 20.8 kwa msimu ujao wa 2023/2024

”Ndugu wajumbe pia tumeweza kutengeneza bajeti ya msimu ujao, kutokana na mafanikio haya tuliyopata msimu huu kwa maana hiyo na msimu ujao tunatarajia kupata mafanikio zaidi na zaidi, kwa hivyo katika makadirio yetu, matumizi pekee ya bajeti yatafika mpaka bilioni 20.8 lakini vyanzo vya mapato bado tupo nyuma kidogo.”- Mkurugenzi wa Fedha, Sabri Sadick

BONGO5
 

Similar threads

kocha mpyaaaaaaaa tutegemee makubwa wana msimbazi
Replies
2
Views
958
Naona kabisa baada ya ile sare na dynamo na kiwango Cha jumla Cha wachezaji naona kabisa Uongozi unafikia makubaliano ya pande zote mbili.. Naona kabisa
Replies
6
Views
500
Eeeeeee bwana weeee, siku tuliokuwa tunaisubiri kwa hamu na Hali na Mali ya kushuhudia msimu mwingine was mashindano, hasa baada ya Yanga kuwa na msimu mzuri uliopita Je huu utakuwa wa Nani? Ngao ya jamiii ilipigwa mechi Yanga na Azam, Yanga akaibuka kidedea kwa 2-0 Kikapigwa Tena kesho...
Replies
89
Views
937

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top