Umewai kukutana na changamoto ya dada wa kazi?

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,883
Reaction score
3,969
Points
113
Niaje?
Hope uko gudi kama mimi..

Wadada wa kazi maarufu kama beki tatu wamekua msaada sana katika familia zetu, hii ni kwasababu ya ubize wa kutafuta maisha kwa wana familia(mme&mke)....

Changamoto inakuja pale tuu unapopata dada wa kazi ambaye ni kichomi, yaani mauza uza yakutosha...

Ndugu zangu hawa wadada wa kazi ni hatari (wengi wao), kabla ajaja kwako chukua mda kumjua vizuri..

Siku hizi kuna hadi madalali wa kukuunganisha na dada wa kazi kutoka kila mkoa, ndugu yangu kua makini..

Nitaleta mikasa hapa ya hawa madada wakazi mta shangaa, ngoja kwanza niendelee na ujenzi wa taifa...

Usikose mwendelezo...
 
Wadada wa kazi wa singida wanaanza kuhisi joto mapema sana. Ukienda kazini wanaleta wanaume nyumbani kwako
 
Wadada wa kazi wa singida wanaanza kuhisi joto mapema sana. Ukienda kazini wanaleta wanaume nyumbani kwako
Joto kwa baridi hili la Arushaa? Naona nitabia tu
 
Kisa cha kwanza..

Kuna familia ilitaftiwa mdada wa kazi, huyu dada ni wa huko mbeya.

Kusema ukweli uyu dada alikua na tabia njema na yakuvutia, mstaarabu saana, niwale mabinti akikusalimia anapiga goti, akikunawisha mikono anapiga gotiii, akikupa maji ya kunywa anapiga goti mpaka umalize kunywa....

Yaani ikafikia mahali akaombwa apunguze kupigapiga magoti, ila hakawa aelewi mwendo ni uleule..

Uyu dada alikua mchapakazi kweli ila shida ikawa kwenye budget, na maanisha kuhusu kupikapika yaani mchele kilo kumi haukai, kiujumla gharama za chakula zikaongezeka pale ndani sii sukari sii unga sii samaki sii mayai, hayaonekani yanapoelekea..

Ikabidi yule binti achunguzwe pengine anauza vitu, au anagawa kwa watu(majirani).

Katika kupeleleza peleleza siku moja mwenye nyumba(baba) akarudi kwa kushtukiza alipata dharura, sasa alipoingia ndani akamwita dada wa kazi, holaa, yaani dada aitiki..

Baada ya kuita sanaa (mnoo) ndio akasikia sauti ya dada inaitikia jikoni ila kajifungia kwa ndani..

Baba wa watu akamuuliza mbona umejifungia jikoni nini shida? Binti anajibu akiwa kule jikoni, nafungua ngoja kwanza, mzee ikabidi mkali akamwambia fungua au niuvunje huu mlangoo..

Binti wa watu ikabidi afungue kwa uwoga, mzee akaingia kule jikoni aangalie nini kinaendelea(kichwani akiwaza labda binti aliingiza msela).

Kilicho mshangaza mzee wawatu, alikuta wali umepikwa lile sufuria kubwa la kilo mbili (kumbuka binti aliachwa home yeye na mtoto mdogo) kwahyo kivyovyote wasingeweza kumaliza msosi wote ule..

Jamaa akamuweka dada wakazi kikaangoni kutaka kujua alikua anapika chakula chote kwa ajili ya nani?

Binti alipoona mzee yuko seriazi akaaza kujilizaliza pale, akasena babu na bibi yake wanamtokeaga live(walishafariki kitambo) wanasema wananjaa kwahyo wanamwamrisha apike kingi ili nao wale..

Binti akaongezea kuwa siku akipika chakula kidogo usiku awanamtokea na wanamwadhibu, kwahyo ili kukwepa adhabu yeye anapika cha kutosha kisha anatenga cha familia kinachobaki kwenye sufuria anawaachia wazeewake, jamaa alichoka ikabidi amrudishe yule binti kwao kesho yake...
kwa changamoto yoyote ya uandishi mnisamehe

Kaa tayari kwa mkasa wa pili
 
Tatumai kwenye miendelezo yako hatutakosa vijana wa hovyo
 
Mkasa wa pili

Ilikuwa mwaka 2018, familia moja ilikua na uitaji wa dada wa kazi, wakatafuta sana bila ya mafanikio, ndio akili ikawajia kulikua na kijana wa kazi(za ngombe) alifanyaga kazi kwao zamani akaacha na kurudi kwao singida, kwahyo wakamtafuta ili awasaidie kutafta dada wa kazi.

Kweli yule kijana aikuchukua roundi ndani ya siku kama tatu akawa ameshampata, so wakafanya utaratibu wote binti akasafiri mpaka arusha...

Ikawa heri kwakua binti alikua ni mchapa kazi kwelikweli ukizingatia kazi yake kubwa ilikua ni kukaa na binti mkubwa waiyo familia(alikua ajiwezi, mlemavu) yule dada wa kazi alikuwa hana kinyaa kwahyo kazi aliiweza vizuri sana..

Changamoto ikawa huyu binti kuna wakati hataki kusemeshwa(au kujichanganya na watu) ila ikipita mda flani anarudi kawaida.,, ikaenda hivohivo hadi wakamzoea.

Ikapita kama miezi nane hivi yule binti kwanzie afike arusha na akuwai kurudi kwao kuwasalimu zaidi ya kuwapigia tu simu... sasa pale nyumbani watoto waile familia wakawa wamerudi(wote wakike) kwa ajili ya sikuku za mwisho wa mwaka, kwahyo nyumba ilikua na shamrashamra za kutosha (walokole tunaita Vibe)...

Wakati vibe linazidi kuongezeka ikawa yule binti wa kazi kama kawaida yake lile tatizo lake au tuseme pepo likapanda akawa ataki kusemeshwa ni mwendo wa kujitenga na watu(chumbani mda wote au nje)... hawa wageni awajazoea hali ya huyu dada maana ndio kwaanza wamefika nyumbani hata wiki haijakata...

Kwahyo wakaanza kumsema yule binti aache kiburi akiitwa aitike, akisemeshwa ajibu sio anangalie watu kama nyanya mbichi..

Mama yao akawaambia huyu ndivo alivyo mwacheni kichwa kikikaa sawa utamwona anakuja mwenyewe, mimi nimeshamzoea mbona...
Wale mabinti wakaja juu hatariii wanasema unamzoesha ujinga, huyu ni mfanyakazi inakuwaje akupande kichwani, kiburi apeleke kwenye familia yake, yaani yule binti alichambwa vya kutosha siku hiyo...

Kama kawaida ya sikukuu lazima shopping ziusike, kwahyo familia wakajazana kwenye nguruwe( toyota noah) hao mjini wakamuachia maelekezo ya kutosha yule mfanya kazi, na mkwara juu kwamba tukute ujafanya kama tulivyo kuagiza uonee...

Shopping ilienda vizuri sana na atimae wakarudi nyumbani, lakini kilicho wa sikitisha na kuwapa hasira hawa wandugu ni kwamba, huyu binti akufanya kazi hata moja, ikabidi wamsake kwa hasira sana ili wamuoneshe dawa ya kiburi inakuwaga nini...

Walimtafuta, walimwita ila akuitika, lakini mmoja wawale binti wa nyumba ile alisikika akipiga kelele(yowe) kutokea chumbani, ndipo watu wote wakakimbilia kujua nini kinaendelea..

Hawakuamini macho yao baada ya kukuta yule binti wa kazi kajininginiza / kajinyonga na kanga...

Kufupisha stori, baada ya majirani kujulishwa na uongozi wa kijiji plus polisi, kimbembe kikaja siku ya kusafirisha mwili kuelekea singida..

Safari ilianza kombora saana(kosta moja na Cruza moja) familia na majirani na mimi nilikuwepo, tulifika singida maarufu kama singapore, tulipo karibia na kwakina binti tulikuta watu wengi kama mkutano wa mwampoosa ukitusubiri, ila cha ajabu ni kwamba walikua wanatuzuia tusiendelee(walikua wametuzunguka).

Wanalia wanapiga ukunga(yowe) wengine wameshika mawee, yaani kifupi waliisi mtoto wao alifanyiwa ukatili ndio maana akajinyonga, kwahyo wanasema rudini nae tunamtaka akiwa hai, wengine wanasema kama mlivo mrudisha mtoto wetu maiti nanyie mtarudi maiti(uku wameshika mawe)

Yaani ilikua shida nilijuta nmeenda kule kutafta nini, wakati huo wengine wameanza kupasua gari vioo, kuna vijana wanatoa wazo watuchome ndani ya gari...

Kama mungu saidia kumbe wazee wa kanisa kushirikiana na uongozi wa kijiji walipiga simu polisi ndio ikawa pona yetu...

Mkasa mwingine unakuja
 
Similar threads

Kwema.... Hivi ulishawahi kwenda sehemu ambayo hujawahi kufika toka uzaliwe alafu ukajikuta mazingira unayajua vinzuri na hujawahi kufika??
Replies
8
Views
290
Ukweli usio pingika kuwa wanaume karibia wote walishawahi kujihusisha na kitendo cha kujichua Humu kunawatu wazima je ni jinsi gani kwa mtu ambaye anapanga kukutana na mtu kimwili anaweza kamatia goma bila kuharibu show Nipeni njia gani na mazoezi ya kufanya, jinsi ya kubehave wakati wa...
Replies
15
Views
267
Back
Top