- Joined
- Jun 4, 2023
- Messages
- 7,617
- Reaction score
- 26,430
- Points
- 113
Inatokea mara chache sana kwa mwanamke kupata mimba mbili kwa wakati mmoja, au kupata ujauzito akiwa mjamzito.
Wataalamu wanaorodhesha sababu tatu za kibaiolojia ambazo zinapelekea ugumu wa hilo kutokea:
1. Mayai kutozalishwa ama kutoka. Kawaida mwanamke anahitaji kutoa yai lenye afya ili apate ujauzito. Mara baada ya yai la kwanza kutoka na kufanikiwa kurutubishwa na kupandikizwa kwenye mji wa uzazi, homoni za uzazi ama ujauzito hutoa taarifa kwa ovari kwamba mayai hayaitajiki tena kwa sasa. Ikiwa mwanamke ana ujamzito, mji wa mimba hautapokea mayai tena, na virutubisho vyote vitakavyozalisha vitamwambia asijiandae kwa kuzaa.
2. Ukizungumzia mji wa uzazi ama mfuko wa uzazi, inakuwa ngumu kwa yai lingine lililorutubishwa ikiwa kuna la kwanza limerutubishwa na kupandikizwa kwenye mji huo.Kawaida utando wa mji huo hutanuka kusaidia kulishika yai la kwanza, hivyo ni ngumu kwa yai la pili kusaidika kwenye kingo za uzazi na utando huu.
3. Wakati wa ujauzito, kuna kitu kinachoitwa 'mucus plug', ni uteute kama makamasi unaotoka kwenye mfumo wa uzazi , ambao kazi yake sio kulinda tu mji wa uzazi dhidi ya maambukizi lakini pia inazuia mbegu za kiume kupita.
Kwa sababu hizi, wataalama wanaendelea kujiuliza inawezekanaje kupata mimba ukiwa na mimba?
Picha: Mwanamke mwenye mimba mbili huwa na watoto tumboni wanaotofautina kwa vitu vingi ikiwemo kimo na damu
Mpaka sasa kuna visa kama 10 vilivyoripotiwa duniani kuhusu wanawake waliopata ujauzito wakiwa wajawazito, ingawa inaelezwa huenda kukawa na visa vingi tu ambavyo hajiweza kurekodiwa. Hivi karibuni huko nchini Australia mwanamke anayeitwa Kate Hill, ambaye amekuwa na aina hii ya ujauzito mara mbili kwa siku 10.
Alijaliwa kuwa na mabinti wawili, Charlotte na Olivia, ambao waliitwa mapacha, ingawa walikuwa na siku kumi tu za kuishi.
Wote walizaliwa siku moja, lakini walikuwa na kimo tofauti na aina ya damu tofauti.
Kibaiolojia, suala hili kama halipaswi kutokea, kawaida vichocheo ama homoni za mimba huzuia ama hufunga mfumo wa mwanamke, na kumfanya ashindwe kutoa mayai wakati wa ujauzito. 'Ndio maana ujauzito juu ya ujauzito ni jambo la kushangaza'
Hakuna anayejua hasa kwa hakika, kwanini hili linatokea.