- Jul 9, 2023
- 3,821
- 3,805
- 113
Japo haiwezekani kuishi Mars kutokana na kukosa baadhi sifa ambazo zinaweza kusapoti uhai. Wanasayansi wengi wamekuwa wakitabiri kitakuwa na watu siku moja huko sayari ya Mars.
Hivi karibuni shirika la mambo ya anga la marekani NASA, limekuwa likifanya utafiti wa kina juu ya Mars. NASA wanadai ifikapo mwaka 2035 kutakuwa na ziara ya kupeleka watu huko Mars.
Kwa kasi ya utafiti inayoendelea natabiri kuwa mwaka ifikapo mwaka 2040 kutakuwa na watu wanaishi Mars. Ingawa maisha huko hayatakuwa kama hapa duniani. Itawalazimu watu:
1. Kujenga nyumba ndani ya ardhi. Nyumba hizi zitakuwa na mfumo wa kuzalisha hewa ya oxygen na maji safi ya kunywa. Hakuna miti kama duniani ya kuzalisha hewa ya oxygen hivyo hata kutoka nje ya nyumba itawalazimu watu kuvaa nguo maalumu "space suits" na kubeba mitungi ya gesi oxygen. Pia kutakuwa na vimondo na mawe ya angani yatakayoangukia Mars.
2. Mionzi ya jua inaweza kuwa ya athari kubwa ikiwa watu watatembea ardhini bila kinga maalumu. Hili swala limeleta mijadala mikubwa hivi karibuni. Wengi wamesema mionzi hii hatarishi haitakuwa hatarishi sana ikiwa watu wataishi ardhini.