Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa afariki dunia

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Muhindi Wa Kuchoma

Well-known member
Platinum Villager
Jul 9, 2023
3,787
3,770
113
Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa amefariki dunia, akiwa anapatiwa matibabu jijini Dar es Salaam.

Tangazo la kifo cha Lowassa kimetangazwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango.

Katika tangazo fupi alilolitoa kupitia televisheni ya taifa, Mpango amesema kuwa Lowassa amefikwa na umauti katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

''Amefariki leo akipatiwa matibabu kwa ugonjwa wa kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu. Hayati Ngoiyai Lowassa ameugua kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu tangu tarehe 14 mwezi Januari mwaka 2022''.

Alikuwa akipatiwa matibabu katika taasisi hiyo ya moyo kisha kupelekwa Afrika Kusini na baadaye kurudishwa tena katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.

Lowassa alihudumu kama Waziri Mkuu wa Tanzania chini ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa miaka mitatu, toka 2005 mpaka 2008 alipolazimika kujiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia hii leo.

Mwaka 2015 Lowassa alikihama chama tawala cha CCM baada ya kukosa tiketi ya kuwania urais kupitia chama hicho.

Alitimkia chama kikuu cha upinzani cha Chadema ambapo aliungwa mkono kugombea urais na vyama vilivyounda umoja wa upinzani wa UKAWA kwa wakati huo.

Lowassa hata hivyo alishindwa katika uchaguzi huo na aliyekuwa mgombea wa CCM John Pombe Magufuli. Lowassa alirejea CCM mwaka 2019.

Lowassa alizaliwa Agosti 26, 1953 amefariki akiwa na umri wa miaka 70 na anaacha alama kama moja ya miamba ya siasa za Tanzania.

lowassa-in.jpg
 

Hakimu

Immortal Village Hero
Staff member
Jun 3, 2023
2,637
6,116
113
Mungu alitoa na leo ametwaa jina lake lihimidiwe
 

Similar threads

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alithibitisha kujitolea kwa umoja huo kwa wazo la kuijumuisha Ukraine katika safu zake. "Ninatarajia viongozi washirika kukubaliana juu ya vipengele vitatu ambavyo vitaileta Ukraine karibu na uanachama wa NATO. Kwanza, ni lazima tuidhinishe mpango wa...
Replies
2
Views
164
Dar es Salaam. Sakata la Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma kuongezewa muda wa utumishi wa wadhifa huo sasa limetinga mahakamani baada ya wakili mmoja kufungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu Masjala Kuu, akipinga hatua hiyo. Wakili huyo, Humphrey Malenga amefungua kesi hiyo siku chache baada ya...
Replies
1
Views
543
" Je unafahamu kuwa nchini Tanzania kuna mji mkongwe ambao usafiri wake mkuu ni baiskeli? Kwa muda wa miongo mitano sasa, wakazi wake wameendelea kutegemea zaidi usafiri huo ambao unatambua baisikeli za uchukuzi wa umma kwa jina 'daladala'. Mwandishi wa BBC @lasteck2023 ametembelea mji huo wa...
Replies
6
Views
200
Dar es Salaam. Sakata la Jaji Mkuu, Profesa Ibrahimu Juma kuendelea kusalia kwenye nafasi hiyo limechukua sura mpya baada ya Wakili wa kujitegemea, Humphrey Simon Malenga kufungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu Masjala Kuu, Dar es Salaam kupinga kiongozi huyo kuongezewa muda wa utumishi huo...
Replies
2
Views
574
Dar es Salaam. Sakata la Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuhudumu katika nafasi ya Jaji Mkuu wa Tanzania limeibua utata baada ya Jaji wa Mahakama ya Rufani, Stella Mugasha kudaiwa kuandika barua akieleza uamuzi wa kumwongezea muda ni uvunjaji wa Katiba na kutozingatia misingi ya sheria. Hata...
Replies
0
Views
491
Top Bottom