Fursa: Mtaji Laki 1 - Mayai ya Kuchemsha

Muhindi Wa Kuchoma

Well-known member
Platinum Villager
Joined
Jul 9, 2023
Messages
3,821
Reaction score
3,805
Points
113
Kama hujaamua kutoka ndani na kuingia mtaani ama kwa lugha nyengine kama hujaamua kufuta aibu kichwani mwako basi hii makala haikufai.

Mradi huu utakuhitaji kuajiri kina/binti mmoja au zaidi kulingana na upatikanaji na uaminifu wa vijana ambao unahisi watakufaa.

Katika mfano wangu ambao nitatumia eneo la dar:

1. Nita ajiri vijana watatu ambao nawafahamu mwenendo wao.

2. Nitanunua mayai trey 9 pamoja na trey zake. Hapa nitatumia kati ya 70,000 hadi 90,000.

3. Nitanunua chumvi pakti moja.

4. Nitachemsha hayo mayai trey zote 9.

5. Kila kijana ataondoka na trey tatu asubui na kwenda kuuza maeneo ya mchanganyiko ikiwa either ni stendi na sehemu kama hizo.

6. Makubaliano kwa vijana hao watatu ni kwamba kila trey ambayo mtu anauza nitamlipa shilingi 3000. Na bei ya yai wanapaswa wauze shilingi 500.

7. Mapato kwa siku ya kwanza yatakuwa 500x30x9 = 135,000. Kati ya hizo nitawapa vijana shilingi 9,000 kila mmoja.

8. Ratiba itaendelea hivyo kwa muda na nitapanua biashara itakapobidi.

Gharama zingine ndogo ndogo ni kama mkaa na chumvi na ni kiasi kidogo sana.

Hivyo gharama zetu ni:
Mayai na trey zake = maximum 90,000
Malipo kwa vijana = 27,000
Chumvi, mkaa = 3,000

Jumla 120,000.

Mauzo 135,000 toa gharama 120,000 sawa na faida 15,000. Kuanzia siku ya pili faida itaongezeka mana hatununui mayai na trey zake bali tunanunua mayai pekee.


 
Wazo zuri ukiwa na vijana waaminifu. Maeneo kama kariakoo kuna mzunguko mkubwa wa watu ukiwa na vijana watatu unauza hesabu nzuri
 

Similar threads

Niaje wandugu, refer to the heading above😁😁 Mazingira unayoishi au ulipokulia umepaona fursa au ndio kikwazo cha wewe kutusua? Je umeshawai kukaa nakutafuta kuona fursa ktk mazingira unayo kaa(unapo ishi?) Au umeshawai kumuuliza Mungu ufanye nini kutoka katika mazingira hayohayo unayo ishi...
Replies
1
Views
242
Hili ni swali ambalo nimeulizwa ila nimeona nije niombe msaada kwa mabisnez mani wa KF Ukizingatia mtu mwenyewe hawezi kutembea all the time mtaani anatafuta tu njia ya passive income Ushauri wako Gily Kondeni0112
Replies
1
Views
417
Wakuu kwa mtaji huu naweza fanya biashara gani alafu jioni nikatimba class
Replies
6
Views
185
Back
Top