Hadithi au Ukweli: Je kuna madhara kulala na kioo kutazama kitanda?

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Kumekuwa na watu wengi wakijitojeza wakodai kuwa kuna madhara kulala na kioo kutazama kitanda. Inaaminika kuwa kulala na kioo kutazama kitanda huleta:
  • Mikosi,
  • Kukosa usingizi,
  • Kuvunjika kwa ndoa,
  • Migogoro,
  • Ndoto mbaya nk.,

Nadharia hii inatoka wapi?
Dhana kwamba hupaswi kulala mbele ya kioo hutoka kwa feng shui. Feng shui ni falsafa ya zamani ya Kichina ambayo inahusisha kupanga nyumba yako, vitu, na nafasi ya kuishi kwa mpangilio maalumu ili kusawazisha maisha.

Kuna madai kuwa kulala na kioo chumbani ni jambo baya. Mengi ya haya yanahusiana na dhana ya msingi kwamba vioo vinaaminika kuwa milango kwenda kwenye ulimwengu mwingine, pia inasemekana kuwa na kioo katika chumba chako cha kulala huongeza mara mbili aina ya bahati uliyo nayo.

Kuongeza bahati yako maradufu kunaweza kuwa jambo zuri ikiwa mambo yanaonekana kukuendea vizuri, lakini ikiwa bahati mbaya imekuandama katika maisha yako kwa njia nyingi, inaweza kuwa jambo baya kulala mbele ya kioo. Inaaminika kuwa kuwa na kioo mbele ya kitanda chako huongeza bahati nzuri au bahati mbaya maradufu, kulingana na kile unachopitia kwa wakati huo.

Inafikiriwa kuwa inaweza kusababisha kukosa usingizi na hata kusababisha ndoto mbaya. Imani ni kwamba tunapolala roho yetu huondoka kwenye mwili wetu. Hii inapotokea na roho yetu inapoona taswira yako kwenye kioo inashtuka na husababisha ndoto mbaya katika usingizi wako.


Inashauriwa hivi:
Inashauriwa kuziba kioo wakati wa kulala kwa kukifunika ili kisiweze athiri energy iliyo ndani ya chumba chako.

Hivyo hivyo TV pia zinashauriwa zisitamaze kitanda chako kwa sababu kioo chake hufanania kioo. Ili kuzuia matokeo mabaya yanayotokana na hili unashairiwa kufunika kioo cha TV unapoenda kulala.
 

Katkit

Well-known member
Platinum Villager
Joined
Jun 8, 2023
Messages
693
Reaction score
2,144
Points
93
sidhani kama kuna ukweli wowote kuhusu hilo, binafsi sio muumini sana wa imani hizo.
 

Similar threads

  • Article Article
Riwaya: Hadithi Zimeamshwa: Minong'ono ya Pagoda ya Mbinguni Mwandishi: King of Dragonmarsh Imetafasiriwa: Hakimu Mchapishaji: KijijiForums Aina ya Riwaya: Epic Fantasy / Mapenzi ya Kusikitisha / Drama ya Giza Onyo:Hii ni kazi ya kubuni kabisa. Isipokuwa imeelezwa vinginevyo, majina yote...
Replies
4
Views
56
Wasalaaam.... Kumekuwa na imani mbalimbali miongoni mwa jamii yetu kuwa uchawi upo wengine wana imani haupo.. Je una amini uchawi upo???? Kwenye kijiji kimoja katika milima huko Scotland, Tonks Brown anasema anajivunia kuwa mchawi. Kwake sherehe za Halloween hazihusu tu mavazi, maboga au...
Replies
22
Views
464
Wakuu mko gud? Mimi niko gudi kabisa na mshukuru muumba wa mbingu na nchi niko mzima, na nina furaha na amani, nmeshiba, na nina kama afu kumi na tatu za kenyA mfukoni😊 Najua mpaka hapa nitakua nimeshakwaambukiza ka furaha na ka amani kwa wote ambao hamko sawa😀 Kumekuwa na misemo ya hekima...
Replies
9
Views
457
  • Article Article
Jumatatu naamkia makao makuu ya nchi , katika wiki kadhaa nyuma . Huko nafanya kilicho nipeleka , najipanga kurudi ila nasema wacha nimpigie rafiki yangu mmoja kutoka huko kwa washua ( Wahaya) Bila ajizi anapokea simu , makutano yanapangwa tunakuwa na muda mzuri sana kwenye kumbi za starehe...
Replies
23
Views
502
habari zenu.. nimekuwa mtu wa mashaka sana kuingia kwenye maisha ya kuishi na mwanamke,mimi ni mkiristo huwa nafikiriaga sana kubadili dini ilinipate mwanamke aliyeshikilia dini sana,kwa sisi wa kristo huwezi pata mwanamke aliyeshikilia dini haswa,kuna walio okoka ila dini hawajui kwenye...
Replies
18
Views
427

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom