HISTORIA YA WACHAGA.....

The great manenge

New member
Platinum Villager
Joined
Jul 8, 2023
Messages
1,320
Reaction score
2,995
Points
0
Natumaini wote wanzima humu..

LIFAHAMU KABILA LA WACHAGA


chagaa.jpg


Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.


Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000 hata hivyo Wachagga wote duniani wanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 2.5 ambapo wengi wao wanaishi nje ya mkoa Kilimanjaro kwenye miji mikubwa wakifanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo hasa biashara.


Wachagga wako wengi zaidi katika miji ya Nairobi, Dar es salaam, Arusha, Mombasa Mwanza, Kampala na miji mingine yote Afrika nzima.

Vikundi vya Wachagga
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogo madogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia Mashariki Tarakea, Rombo hadi magharibi ya Kilimanjaro Siha, Machame. Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Marangu,Wa-Kilema, Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vunjo, Wa-Uru, na -Uru, na Wa-Siha.


Lugha ya Kichagga
Lugha ya Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katikaKirombo, Kimarangu, Ki-Old Moshi,Kikibosho, Kimachame, Kikirua na Kisiha. Lugha hizi zinakaribia kufanana kulingana na jinsi makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Ki-Old Moshi kinafanana na Kikirua, ambacho nacho kinafanana kidogo na Kimarangu. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho. Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo

Historia ya elimu kati ya Wachagga
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Kikristo walijenga makanisa na shule. Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania.


Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamishinari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi. Wakati wakazi wa mikoa mingine walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1,2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro vimezidi sana idadi ya shule katika mikoa mingine yote.

800px-Tengeru_market.jpgchagaa.jpg


Ni vema pia kusema kwamba shule hizi kuvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi wachagga tu. Hivyo hii imepelekea wachagga kuwa wengi katika nafasi mbalimbali serikalini na kwenye makampuni binafsi huku wengine wakiwa wamiliki wa biashara kubwa na kushikilia nafasi za juu kabisa za kumiliki mali ndani na nje ya Afrika Mashariki.

Kilimo na chakula
Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe,viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya na vitunguu.

Ndizi za Wachagga
Ingawa wachaga wa leo wanakula vyakula mbali mbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi. Kuna ndizi za aina mbalimbali na hutumika kwa matumiza tofauti. Mfano ndizi kisukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda. Ndizi mshare kukatwa zikiwa mbichi na kupikwa chakula mbalimbali pamoja na nyama ya ngombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko,kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika.


Aina nyingine ni ndizi-ngombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.
Aina nyingine ni ndizi-mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa ya Darisalamu utaona ndizi- mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku-vumbi au kiti-moto.

Wachagga na muhogo
Inasemekana kuwa “mchagga halisi, hali muhogo – akila muhogo atakufa”. Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yao; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani hasa wa Machame walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba huko huko Kilimanjaro, majirani na watani wa wachagga yaani Wapare walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.

Ulaji kiti-moto
Pamoja na kilimo cha mazao, wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la “kiti moto” ni moja ya mambo yaliyoenezwa na wachagga. Ulaji wa “kiti moto” haukupendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo waisalmu kwao kula nguruwe ilikuwa “ruksa”.

Majina ya Kichagga
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: mfano familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama Kimaro, Swai, Massawe, Mushi, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka Old Moshi na Vunjo. Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu na Kilema. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba na kadhalika hutoka Kibosho.
Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.

350px-Various_food_dishes.jpg
Utawala wa jadi ya Wachagga
Watawala wa kichagga waliitwa “Mangi”. Hawa walihodhi mashamba, ngombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (wajerumani), Mangi Sina wa kibosho – anajulikana kwa uhodari wake wa vita katika kupigana na wamachame na kupora ngombe na mazao yao na Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo. Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa ma-Mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia wanaaminika walikuwa ni kama mabepari wa kwanza wa ki-jadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao. Usemi maarufu wa “u-Mangi-meza” inawezekana kuwa umetokana na watawala hawa wa kichagga.

wachaga.jpg

Ardhi
Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi. Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni “kihamba”. Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi uchagani ulipelekea wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya nk wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula. Ukienda kwenye mikoa hii utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta katika makusanyio ya wachaga mikoani mbali mbali.

Maoni juu ya Wachagga
Ingawa wanaume wa kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na hufuga ngombe na kazi za shambani. ila kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongon mwao. Wanawake wa kichagga (hasa kutoka Rombo) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Ingawa kipato cha wachaga ni kikubwa kulinganisha na cha makabila mengine, takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa kuongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo kunatokana na wazazi kujali zaidi kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto. Wengi wa wototo ni wale ambao wazazi wao ni watu wapombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba uchagani kuna vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa nibiashara kubwa. Karibu kila kaya kumi natano kuna kila cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya dede sita au lita mia moja. Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo Hii inawezekana kuwa matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchaggani kama Old Moshi na Kibosho ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi mchana na jioni. Sababu nyingi ni kazi; mama wa kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hawana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani hivyo wanakuwa nyumbani ama wenyewe au na mayaya. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za kibiashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi. Pia baadhi ya wamama wa kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri tofauti na chakula walichoandaliwa watoto japo ni chakula kilekile.

Katika kipindi cha sikukuu hasa za Krismasi na mwaka mpya, Wachaga wengi hupenda kurudi nyumbani, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu, wanaukoo kukaa pamoja na kujadiliana mambo jinsi yalivyokwenda katika kipindi kizima cha mwaka.

Pia wakati mwingine katika kipindi hicho Wachaga hutumia muda huo kama sehemu ya kwenda kuwatambulisha watoto kwa bibi na babu zao, hasa wale waliozaliwa mijini.


Je, Wachaga wana asili ya Uyahudi?

Wakati fulani Wachaga walinasibishwa na Uyahudi. Ilidaiwa kuwa kabila hilo lina nasaba na Wayahudi wa Ethiopia.
Wakati fulani Wachaga walinasibishwa na Uyahudi. Ilidaiwa kuwa

kabila hilo lina nasaba na Wayahudi wa Ethiopia.

Hata hivyo, kabila hilo linalopatikana kaskazini mwa Tanzania, linaelezwa kuwa limetokana na mchanganyiko wa wahamaji kutoka makabila mbalimmbali wakiwamo Wakamba, Wataita, Wamasai na Wasambaa.


Hao wanaotajwa kama Wayahudi wa Ethiopia wanajulikana kama ‘Beta’ na waliishi katika ufalme uliojulikana kama Aksumite.

Huo ulikuwa ni ufalme wa zamani ambao uliokuwapo katika maeneo ambayo sasa ni Eritrea, kaskazini mwa Ethiopia, sehemu kubwa ya mashariki mwa Sudan na kusini/mashariki mwa Yemen.

Wengine wanawaita ‘Falasha’ au ‘Mafalasha’. Hao hawakuwahi kuhama kuelekea kusini kiasi cha kufikiriwa kuwa ndio waliokuja kulowea kuuzunguka Mlima Kilimanjaro.

Hata hivyo, historia ya ‘Mafalasha’ na ile ya ‘Wachaga’ zinatofautiana sana, kiasi kwamba hakuna mahali popote unapoweza kukuta mfanano wao wowote hata kwenye tamaduni zao.

Hadi mwaka 1975 Mafalasha wengi hawakutambuliwa rasmi kama Wayahudi, na wengi wao walisafirishwa kwa ndege kupelekwa Israeli kati ya mwaka 1984 na 1985.

Kuanzia Alhamisi ya Novemba 21, 1984, Mafalasha takriban 8,000 kutoka Ethiopia walikwenda Israeli. Falasha wa mwisho alisafirishwa Jumamosi ya Januari 5, 1985. Kwa wiki hizo saba, zaidi ya ndege 30 zilishiriki kuwasafirisha Wayahudi hao wa Ethiopia kuwapeleka Israeli.

Ni kweli, kwa mujibu wa simulizi fulani, Malkia wa Sheba (wa Ethiopia) alikutana na Mfalme Sulemani na kuzaa mtoto aliyeitwa Menelik (alikuja kuwa mfalme wa Ethiopia) na kwamba uzao wa Mafalasha hao ulitokana na Menelik.

........GOD BLESS WACHAGGA ....
 
Mimi ni mchaga na nishawahi jaribu kuandika historia ya wachaga. Kifupi hii historia ni sehemu tu ya historia ya wachaga
 

Similar threads

Pata Historia Fupi ya Marehemu Mwenyekiti wa kamati ya mazishi akainuka na kuanza kusema "kinachofuata sasa ndugu wafiwa na marafiki wa marehemu ni kusoma historia fupi ya marehemu tuliyemzika hapa leo. karibu ndugu uliyeandaliwa kwa shughuli hiyo Msomaji: "Ifuatayo in historia fupi ya...
Replies
6
Views
488
Wanakijiji amani ya Mungu iwe nanyi Naomba msaada kwa ajili ya mtoto huyu wa mjomba. Kwanza mjomba alizaa na mwanamke wa kichagaa wakaachana sababu sifahamu kwani nilikua mdogo kiasi. Sasa baadae mjomba akaja kuoa mwanamke mwingine wa kichaga ambae yupo bae mpaka sasa. Msaada ninao taka kutoka...
Replies
12
Views
311
Back
Top