Ikitokea shetani amekufa leo utaacha kufanya dhambi?

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,883
Reaction score
3,969
Points
113
Wakuu nawasalimu mara tatu...

Ikitokea shetani amekufa leo utaacha kufanya dhambi?

Watu wengi wamekua wakimsingizia shetani kila kitu, ila ukweli ni kwamba hata shetani akifa leo bado kuna wakuu wataichukua ile nafasi ya shetani.

vp unahisi utakua mtu safi kama shetani atakufa au kuondolewa?

Karibu
 
Hahaha hata ukisema kula mifupa ya kuku ni Dhambi hata kama haina maana watu watatafuna

Watu wanapenda kutenda dhambi
 
Umetisha ila kaka ndio ulikataa kutoa ushuhuda?
wee jamaa ni tomaso, ushuhuda wangu hauna impact yeyote kwako coz, wako wengi walio tokewa na malaika kwenye biblia ungewaamini hao kuliko mm.

Sio kama najisifu wala nini ila hata sauti ya Mungu mwenyewe nmesha wai isikia akiniambia baadhi ya mambo.. so kama unataka kuthibitisha kuwa na kiu wewe binafsi kutaka kuexperience spiritualy things ili usisimuliwe na mtu, utaenjoy sana...
 
wee jamaa ni tomaso, ushuhuda wangu hauna impact yeyote kwako coz, wako wengi walio tokewa na malaika kwenye biblia ungewaamini hao kuliko mm.

Sio kama najisifu wala nini ila hata sauti ya Mungu mwenyewe nmesha wai isikia akiniambia baadhi ya mambo.. so kama unataka kuthibitisha kuwa na kiu wewe binafsi kutaka kuexperience spiritualy things ili usisimuliwe na mtu, utaenjoy sana...
Haya niambie vya kufanya ili niexpirience
 
Haya niambie vya kufanya ili niexpirience
Sina hiyo fomula ila kikubwa ni kujua na kukubali kuwa Mungu ndio muanzilishi wa mawasiliano kati yake na mwanadanu, Yehova ni Mungu anayezungumza..
Nikimaliza kupika nikila nikishiba, nkicheki epsode moja ya FAUDA ntajaribu kukuandikia tips
 
Sina hiyo fomula ila kikubwa ni kujua na kukubali kuwa Mungu ndio muanzilishi wa mawasiliano kati yake na mwanadanu, Yehova ni Mungu anayezungumza..
Nikimaliza kupika nikila nikishiba, nkicheki epsode moja ya FAUDA ntajaribu kukuandikia tips
Poa
 
Mkuu Hakimu jana nilinogewa na series hadi nikambonji.

Hizi ni baadhi ya tips, utachukua utakazo ona zinafaa zingine utaweka kapuni.

1:Elewa kuwa malaika wako katika mfumo wa roho japo wanaweza kuvaa mwili na wakaonekana kwa mfano wowote, moto, mtu, n.k

Kwahyo ili uwaone malaika live lazima yeye awe katika mwili na uwe na neema ya kumtambua

Pia unaweza kumuona malaika katika dimension nyingine (ya kiroho) pale tu wewe utakapokua katika dimension hiyo ya kiroho, au kwenye ndoto, au kupitia maono.

2:Kazi ya malaika ni kuleta taarifa, kutulinda, kutuonya kutusaidia n.k

Kwahyo swala la kuwaona haliko ndani ya uwezo wako, utawaona pale utakapo pata neema hiyo(kuletewa ujumbe, kuonywa kusaidiwa nk)

Kumbuka 2 Korintho 5:7 (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona) ile kwamba huwaoni haimaanishi hawapo. kuna walio waona malaika wakataka kuwabaka, kuna walio elezwa habari mbalimbali na malaika ila wakapuuza kwahyo unaweza kuwaona hao malaika na usibadikike chochote ktk imani yako
 
3: Njia pekee tulio pewa na Mungu sisi kuongea nae ni kupitia MAOMBI, yaani wewe unapotaka kuwasiliana nae lazima utumie njia ya maombi.
Ila yeye (Mungu) anapotaka kuwasiliana na sisi anazo njia nyingi za kutumia, anaweza akasema na wewe moja kwa moja, kwa ndoto, kwa maono, kupitia malaika, kupitia neno, ndege, wanyama n.k

Kwahyo yeye anaamua atumie njia ipi kuwasiliana na wewe, sio wewe unaamua coz yeye ndio aliye zianzisha njia hizo kifupi aumpangii...

Anaweza akawa anaongea na wewe kwa ndoto, ila wewe ukawa hauzitilii maanani na unasubiri umsikie live, au kupitia malaika, so unatakiwa kuwa sensitive kwanzia sasa na uwe tayari kumsikia kwa njia yeyote.
 
4: Mpokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako(okoka).
Kwanza kabsa niseme Mungu anaongea na mtu yeyote yule akitaka, uwe mlevi, mpagani, muuaji, mlokole, msabato, yoyote yaani.

Kuokoka ni kuishi maisha ndani ya kristo, hii nimeiweka kama tips coz kuishi ndani ya kristo nipamoja na kufuata neno lake, kuomba, kuishi katika njia zinazo kupasa, kukaa katika mamlaka yako ya utawala n.k
Wakati ukifanya yote hayo ndani ya wokovu kuexperience hayo unayo taka inawezekana kwa asilimia kubwa kubwa sana.

Binafsi yangu baada ya kuokoka kati ya2020-2021 sikuwai kutamani au kutaka kukutana na malaika ila nlikua na bidii katika kusoma neno, kusikiliza mafundisho plus kuomba..

First time malaika nliwaona kwenye ndoto ila sikutia maanani, ikaendelea hivo mpaka baadae nkawa naelewa coz nilikua nakutana na vitu walivyokua wakiniambia.

Mfano kuna day alinitokea kwenye ndoto akaniambia kunabinti yuko Dar es salam mpatie shilingi 47,000/=, nikamuuliza kwa utani mimi nipo arusha nitanpaje hela mtu aliye mbali huko, akatabasamu akachukua mkono wangu wa kulia akawa kama anafanya handshake ndoto ikaisha, asubuhi nikaamka natazama mkononi nkakuta kuna namba za simu za tigo, nikapiga nkamueleza nmeambiwa nkutumie kiasi hiki cha pesa, akasema nayeye alikua kwenye maombi ya mfungo ili apate iyo hela alipie ili arudiemtiani wa 4m4, nikamtumia... ile namba mkononi ilichukua wiki kama mbili ndio ikapotea mkononi....

Kukutana na malaika live akiwa na umbo la mtu inaitaji neema kuwajua au kuwatambua hapohapo kwa haraka kwamba huyu ni malaika.

Nakumbuka nlipokua natafta field, nlikosa na mda wakuanza ulikua umepita wiki moja na siku kazaa, siku hiyo nmebeba baasha yangu nkapanda town(Arusha) nkiwa kwenye gari nkasema moyoni nmechoka kutafuta field naenda town Mungu naomba wewe uwe connection yangu maana sina anae nijua kwenye bank yeyote hapa town.

Kwahyo nkashuka sanawari ili nipite bank zoote, mpaka kieleweke, ila nlipokua nashuka na road akatokea mzee mmoja, anaonekana mjanja mjanja wa mji, akanisalimu kama ananijua mda mrefu, (aliniita jina langu TUMAINI nifate mpaka ofisini ili uanze field kesho) nkamuambia asante, nkaanza kumfata ila nkamuuliza umenijuaje? umejuaje natafta field? yule mzee hakunijibu, alikua anaonekana yko na haraka, kwahyo nkawa namfata tu, tukaingia kwenye taasisi moja kubwa(ya kimataifa) yeye alikua anatoa ishara tu kwamba yuko na mimi(getin).

Tukafka ofis moja akaniambia tusubiri(hatukuingia), punde akaja mmama akatuambia boss anakikao ila anaweza kutusaidia yule mzee akanipa ishara kwa kichwa sikuelewa ndio akaniambia mpe iyo barua ya maombi ya field, nikampa ile barua yle mama akatuambia tusubiri hapo nje, kulikua hamna maali pakukaa so tulilazimika kwenda kukaa nje ya mlango wa ofisi ingine uliokua na viti vya wageni, yule mzee hakukaa ila aliniita jina tena akaniambia wewe msubiri huyo mama atakupa maelezo yote alafu akaondoka.

Nikasubiri kama dakika 30-45 yule mama akatoka akaniita na akanipa maelekezo nkaanza field kesho yake...

Yule mzee sikuwai kumuona mpaka leo,
 

Similar threads

Kwema wadau wa kijiji forum Je shetani/ibilisi ni nani?? Ibilisi (Shetani)- malaika aliyeanguka ambaye Mungu alimpindua kutoka mbinguni kwa sababu yeye, akiwa na kiburi, alitaka kuchukua nafasi ya Mungu. Shetani hapo kwanza hakuwa adui wa Mungu, Yeye aliumbwa na Mungu kama walivyoumbwa...
Replies
26
Views
353
Back
Top