Ikitokea shetani amekufa leo utaacha kufanya dhambi?

4: Mpokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako(okoka).
Kwanza kabsa niseme Mungu anaongea na mtu yeyote yule akitaka, uwe mlevi, mpagani, muuaji, mlokole, msabato, yoyote yaani.

Kuokoka ni kuishi maisha ndani ya kristo, hii nimeiweka kama tips coz kuishi ndani ya kristo nipamoja na kufuata neno lake, kuomba, kuishi katika njia zinazo kupasa, kukaa katika mamlaka yako ya utawala n.k
Wakati ukifanya yote hayo ndani ya wokovu kuexperience hayo unayo taka inawezekana kwa asilimia kubwa kubwa sana.

Binafsi yangu baada ya kuokoka kati ya2020-2021 sikuwai kutamani au kutaka kukutana na malaika ila nlikua na bidii katika kusoma neno, kusikiliza mafundisho plus kuomba..

First time malaika nliwaona kwenye ndoto ila sikutia maanani, ikaendelea hivo mpaka baadae nkawa naelewa coz nilikua nakutana na vitu walivyokua wakiniambia.

Mfano kuna day alinitokea kwenye ndoto akaniambia kunabinti yuko Dar es salam mpatie shilingi 47,000/=, nikamuuliza kwa utani mimi nipo arusha nitanpaje hela mtu aliye mbali huko, akatabasamu akachukua mkono wangu wa kulia akawa kama anafanya handshake ndoto ikaisha, asubuhi nikaamka natazama mkononi nkakuta kuna namba za simu za tigo, nikapiga nkamueleza nmeambiwa nkutumie kiasi hiki cha pesa, akasema nayeye alikua kwenye maombi ya mfungo ili apate iyo hela alipie ili arudiemtiani wa 4m4, nikamtumia... ile namba mkononi ilichukua wiki kama mbili ndio ikapotea mkononi....

Kukutana na malaika live akiwa na umbo la mtu inaitaji neema kuwajua au kuwatambua hapohapo kwa haraka kwamba huyu ni malaika.

Nakumbuka nlipokua natafta field, nlikosa na mda wakuanza ulikua umepita wiki moja na siku kazaa, siku hiyo nmebeba baasha yangu nkapanda town(Arusha) nkiwa kwenye gari nkasema moyoni nmechoka kutafuta field naenda town Mungu naomba wewe uwe connection yangu maana sina anae nijua kwenye bank yeyote hapa town.

Kwahyo nkashuka sanawari ili nipite bank zoote, mpaka kieleweke, ila nlipokua nashuka na road akatokea mzee mmoja, anaonekana mjanja mjanja wa mji, akanisalimu kama ananijua mda mrefu, (aliniita jina langu TUMAINI nifate mpaka ofisini ili uanze field kesho) nkamuambia asante, nkaanza kumfata ila nkamuuliza umenijuaje? umejuaje natafta field? yule mzee hakunijibu, alikua anaonekana yko na haraka, kwahyo nkawa namfata tu, tukaingia kwenye taasisi moja kubwa(ya kimataifa) yeye alikua anatoa ishara tu kwamba yuko na mimi(getin).

Tukafka ofis moja akaniambia tusubiri(hatukuingia), punde akaja mmama akatuambia boss anakikao ila anaweza kutusaidia yule mzee akanipa ishara kwa kichwa sikuelewa ndio akaniambia mpe iyo barua ya maombi ya field, nikampa ile barua yle mama akatuambia tusubiri hapo nje, kulikua hamna maali pakukaa so tulilazimika kwenda kukaa nje ya mlango wa ofisi ingine uliokua na viti vya wageni, yule mzee hakukaa ila aliniita jina tena akaniambia wewe msubiri huyo mama atakupa maelezo yote alafu akaondoka.

Nikasubiri kama dakika 30-45 yule mama akatoka akaniita na akanipa maelekezo nkaanza field kesho yake...

Yule mzee sikuwai kumuona mpaka leo,
duuh hatari sana point zako zote nimezichukua ila sasa nilitaka kukuuliza jambo inakuwaje mtu anaomba muda mrefu unaomba nin? na toba nzuri ni kuombaje na njia ipi nzuri ya kumsifu BWANA na utajuaje unaroho mtakatifu
 
duuh hatari sana point zako zote nimezichukua ila sasa nilitaka kukuuliza jambo inakuwaje mtu anaomba muda mrefu unaomba nin? na toba nzuri ni kuombaje na njia ipi nzuri ya kumsifu BWANA na utajuaje unaroho mtakatifu
Toba maana yake ni kubadili mtazamo au kubadili unavyofikiri.. kifupi ni kuachana na njia mbaya na kufuata ukweli
Kuna tofauti kati ya toba na kuomba msamaha, kwahyo ukiwa unapenda ngono na aujaoa iyo ni mtazamo/njia/mwenendo usiofaa, ukijua ukweli kua uzinzi ni dhambi, utaomba msamaha kisha utaachana na uo mwenendo/njia au mtizamo hiyo ni toba...
Kwahyo toba hapo ni kuacha uzizi maana ndio mtazamo na mwenendo wa kweli
 
duuh hatari sana point zako zote nimezichukua ila sasa nilitaka kukuuliza jambo inakuwaje mtu anaomba muda mrefu unaomba nin? na toba nzuri ni kuombaje na njia ipi nzuri ya kumsifu BWANA na utajuaje unaroho mtakatifu
Maombi ni mawasiliano yako na Mungu,kuomba haimanishi kwamba kila saa unapeleka shida zako NO... omba kwa lengo la kujenga uhusiano wako na yeye(kuomba kuna husisha, shukran, kusifu, kuabudu, meditate, kusikiliza na yeye anasema nini n.k)
Kiwango cha chini cha kuomba ni one hour kibiblia/per day
 
duuh hatari sana point zako zote nimezichukua ila sasa nilitaka kukuuliza jambo inakuwaje mtu anaomba muda mrefu unaomba nin? na toba nzuri ni kuombaje na njia ipi nzuri ya kumsifu BWANA na utajuaje unaroho mtakatifu
Kumsifu Mungu na roho mtakatifu majibu next time
 
Kondeni0112 nimekuelewa sana ila hapo kwenye muda wa kuomba naomba nifahamishwe ni kitabu gan kinasema ni atleast 1hr
 
Kondeni0112 nimekuelewa sana ila hapo kwenye muda wa kuomba naomba nifahamishwe ni kitabu gan kinasema ni atleast 1hr
Kisha akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamuuliza Petro, “Je, ninyi hamkuweza kukesha pamoja nami hata kwa saa moja?”
Mathayo 26:40
 

Similar threads

Kwema wadau wa kijiji forum Je shetani/ibilisi ni nani?? Ibilisi (Shetani)- malaika aliyeanguka ambaye Mungu alimpindua kutoka mbinguni kwa sababu yeye, akiwa na kiburi, alitaka kuchukua nafasi ya Mungu. Shetani hapo kwanza hakuwa adui wa Mungu, Yeye aliumbwa na Mungu kama walivyoumbwa...
Replies
26
Views
353
Back
Top