- Jul 9, 2023
- 3,821
- 3,805
- 113
JINSI YA KUREJESHA KWA KUPAKA RANGI CHUPA ZA KIOO
Chupa za kioo (glass) ziko za aina nyingi, zenye rangi, na ambazo hazina rangi yaani (transparent). Chupa hizi mara nyingi huwa ni mabaki/uchafu (trash) baada ya kutumia vilivyo ndani kama jibini, soda, bia, juice, mafuta, unga, asali au chochote kilichohifadhiwa humo. Baada ya matumizi kuisha, chupa hizo hutupwa majalalani ambako huleta uchafu na ni hatari kwani zinaweza kumkata mtu au mnyama yeyote. Pia vipande vya chupa vinaweza kuliwa na watoto wakidhani ni salama na vikaleta madhara makubwa.
Lakini, chupa hizi zinaweza kufanya kuwa urembo mzuri sana kwa hatua chache na rahisi zifuatazo:
HATUA YA KWANZA
Tafuta chupa za kioo za ukubwa na maumbo tofauti na uzisafishe vizuri, ondoa lebo na talataka zingine na uache zikauke vya kutosha.
ANGALIZO: Angalia kwa makini kama chupa hazijavunjika usije ukajikata au kumkata mtu mwingine.
HATUA YA PILI
Chagua rangi unayotaka kutumia, mara nyingi rangi zinazotumika ni rangi za vioo (glass paint) ila kama itakosekana basi spray paint au rangi yoyote inaweza kufaa. Unaweza kuchagua mistari au picha tofauti unazotaka kuziweka kwenye chupa yako, mfano maua, mizunguko (round patterns).
Unaweza kutumia stencil au masking tape kutengeneza maumbo au mistari unayoitaka, vilevile unaweza kuweka stickers ili kuziba baadhi ya maeneo usiyotaka rangi iguse.
HATUA YA TATU
Paka au pulizia (spray) rangi unayo/unazotaka kutumia kwa uangalifu na umakini mkubwa. kumbuka kukaa mbali na chupa unayotaka kupuliza (kama unatumia spray) ili kuepuka michirizi ya rangi inayoweza kujitokeza. Kama unatumia brashi, paka kwa uangalifu ili usijichafue ama kuchafua chupa .
ANGALIZO: Kama una-spray unashauriwa upulizie walau umbali wa 30 cm toka chupa ilipo unayopulizia ilipo, ili kupata metokeo mazuri na kuounguza dripping.
Hapa unaweza kupaka rangi kwa mifumo ifuatavyo
Inaendelea.....

- Kupaka rangi moja
- Kupaka rangi zinazooana
Inaendelea.....