Mkasa: Jinsi nilivyofundishwa uchawi

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

SEHEMU YA KWANZA.
Nikiwa nimerudi kutoka shuleni nilikutana na mama nje ambaye alinambia tumepata mgeni ambaye atakua akitusaidia kazi za ndani yaani dada wa kazi, kutokana na uchovu na fimbo za siku hio hata sikua na hamu ya kutaka kujua zaidi kuhusu jambo hilo nilimjibu mama kwa kifupi.

“haya”. Huku nikielekea ndani ambapo nilifika na kumkuta dada mmoja aliyekua na umri kati na miaka kumi na saba hadi ishirini ambaye alinichangamkia kama mtu tuliyejuana siku nyingi.

“mambo clara habari ya shule”. Aliongea dada Yule. Na kunifanya nishangae kalijuaje jina langu lakini nilihisi huenda mama alishamwambia kwamba ana mtoto anaeitwa clara.

“nzuri shikamoo dada,”. Niimjibu kwa heshima kwa kua alikua ameninzidi ki umri hivyo alistahili heshima kwani mimi nilikua darasa la nne tu, baada ya kumjibu nilielekea ndani na kulitua begi langu pia nilikuta mizigo ya dada Yule ambaye ilionesha hakua amefika muda mrefu.

Kwakua tulikua tukipata chakula shuleni nilipitiliza kulala ambapo usingizi ulinipitia na nilikuja kustuka majira ya saa sita usiku ambapo nilimuona dada Yule akiwa ameketi kitandani uchi wa mnyama huku akiwa ameinguanisha mikono yake kama mtu aliyekua akisali.

Moyo wangu uliogopa sana na nililazimika kufikicha macho ili nijue kwamba ilikua ndoto au la na niligundua kwamba haikua ndoto bali ilikua ni ukweli kabisa.

Kisha dada Yule akasimama na kuanza kutembea tembea ndani ya chumba changu huku mikono akiwa ameikunja vile vile na macho yake yakiwa yamefungwa, na kisha baada ya muda, alirudi kitandani na kuketi kama alivyokua awali.

Baada ya dakika tano nilimshuhudia mama nae akija chumbani akiwa amevaa kama dada Yule, hapo nilishindwa kujizuia na kutamka.

“haaa, mama kumbe nawe mchawi”. Niliongea kwa mashangao kauli ambayo ilimstua sana mama na kisha akanisogelea bila uwoga na kuniambia.

“shhhhhhhhh, hakuna haja ya kujificha sasa mimi ni mchawi ndio na hata wewe ni lazima uwe mchawi au laa nikuue kama nilivyomfanya baba yako”.aiongea mama maneno ambayo yalinistua sana na kunifanya nianze kutetemeka.

“unaogopa nini? Mimi ni mchawi toka nilipokua na umri kama wewe umewahi kunigundua? Umewahi kuniona nikitisha? Acha ujinga mwanangu”. Aliongea mama na baada ya muda tulimshuhudia dada Yule wa kazi akiinuka huku macho yake yakiwa yanawaka kama tochi. Na hapo nilimshuhudia mama akipiga goti na kuanza kumsujudu dada Yule.

“naam mkuu, nimekuletea binti huyu akiwa kama mwanachama mpya”. Aliongea mama ambapo dada Yule alinitazama kwa makini sana kisha kumgeukia mama.

“inabidi tumfundishe taratibu kabla ya kumtambulisha kwa wenzetu”. Aliongea dada Yule kisha nilimshuhudia mama akiinuka na kunigeukia.

“mwanangu clara, wewe ndiye wa pekee kwangu na nimekuteua wewe upate kujua vitu vyangu vya ndani, na mbona sikuwaambia kaka zako? Naomba uniisitiri”. Aliongea mama na kunipa mtihani mgumu sana katika umri mdogo na mpaka apo sikua nimesema jambo lolote.

Mwisho mama alichukua unga mweupe na kunipaka katika paji la uso kisha tulijikuta sehemu nyingine kabisa ambayo ilikua ngeni kabisa lakini iionesha ilikua ni katika msitu uliopo kando ya barabara.

Kwani magari yalikua yakisikika yakipiita,
“mwanangu, huu ni msitu wa wachawi msitu ambao ukiingia kama si mchawi basi huwezi toka na utafanywa kafara”. Aliongea mama kauli ambayo ilinifanya niwaone wachawi ni watu wabaya.

“Watu wengi wamepotea katika msitu huu na vifo vyao vilikua vya kutatanisha , hiii ni kwasababu wanachukuliwa na mizimu na kufanywa kafara lakini mchawi si mtu mbaya ila wapo ambao wanautumia uchwi vibaya kwa kufanya visasi na mauaji”. Aliongea mama mambo mengi kuhusu uchawi kisha alinifundisha dawa nyingi sana za kichwawi ikiwemo za kupotea na kiini macho.

Kwakua muda ulikua umekwenda tulirejea nyumbani ambapo bado nilikua na maswali mengi sana na siku hio nilipanga ktoka na kwenda kwa rafiki yangu zuwena nipate kumuuliza mambo kadhaa kuhusu hali iliyonitokea jana usiku.

Nilimuaga mama vizuri na kumwambia nilikua nikienda kwa rafiki yang na alichonisisitiza ni kuwahi kurudi.
Nilipofika nyumbani kwa rafiki yangu kulikua kimya sana ambapo nilibisha hodi mara tatu na kufunguliwa na zuwena mwenyewe
“mambo clara”. Alinisalimu zuwena huku akinikaribisha ndani ambapo tulipiga storiza hapa na pale mwisho niliamua kumuuliza swali.

“eti unawafahamu wachawi”. Nilihoji
“eee, ni wanatisha sana na ni wabaya, wauaji na hawana huruma”. Zuwena aliongea kana kwamba ni mtu anaejua mambo mengi sana kuhusu uchawi.

“basi nikwambie kitu zuwena, mwenzio mama yangu ni……”. Kabla sijamaliza ilikuja sauti kichwani mwangu ambayo niliitambua kwamba ni ya mama.

“clara unataka kufanya nini?” iliskika sauti hio
Je nini kilifuata
 

Dr santos

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 4, 2023
Messages
251
Reaction score
571
Points
0
SEHEMU YA NNE

INAENDELEA; kwangu ulikua mtihani mkubwa sana kuanza kufukua makaburi, lakini mama alinitoa hofu na kunambia nisiogope kwani walitakiwa kupima kwanza mama mtu aliyezikwa alikufa kifo cha kupangwa na mungu au cha kichawi.

Kisha alinyoosha mkono juu na kikatokea kitovu kibichi kabisa ambacho bila shaka kilikua cha mtoto mchanga niliogopa sana na nilishangaa akinipa nikishike.
“hiki ni kitovu cha mtu aliyepita dunianni bila kuonekana, na hiki ni cha mtoto mchanga”. Aliongea mama ambapo alinikabidhi vyote.

{kwa wachawi mtu aliyepita duniani bila kuonekana ni mtoto aliyefia tumboni kwa mama yake}

Baada ya kunikabidhi alichukua mikia mitatu ya mijusi wakubwa na kuvifunga vitovu vile na kuviviringisha kwenye majani ya mninga pamoja na mgomba
“haya virushe kwenye kaburi hilo”. Alinielekeza mama na nilifanya kama nilivoagizwa na mama ambapo nilishangaa baada ya kumuona nyoka mkubwa mweusi pamoja na kibuyu kilicholala kwenye kaburi lile kisha nyoka Yule aliingia ndani ya kibuyu hicho.

Mama aliniambia kwamba endapo nyoka Yule angegoma kuingia ndani ya kibuyu au endapo kibuyu kile kisingelala basi mtu huyo angekua amekufa kifo cha kichawi na kafara hio isingefaa kwani hio ingekua maalum kwa mtu aliyehusika na kifo hicho.

Baada ya hapo mama aliniambia nilale juu ya kaburi huku wao wakizunguka kwa kupishana mara ishirini kisha niliambiwa nitoke juu ya kaburi ambapo mama aliniambia walifanya vile ili kama akija mchawi mwingine kutaka kafara basi aone tayari imeshachukuliwa.

Baada ya kazi hio ngumu muda ulikua umekwenda hivyo tulirudi nyumbani ambapo niliambiwa tungerudi baada ya masaa ishirini kama ilivokua mizunguko ile kwaajili ya kuufukua mwili wamarehemu.

********
Ilikua ni jumatatu tulivu sana ambapo mama aliniamsha kwaajili ya kwenda shuleni ambapo baada ya kufanya shughuli zote bila shuruti tuliingia darasani.
kipindi cha hesabu ndicho kilikua cha kwanza na kwakua nilikua sipendi hesabu niliamua kulala mpaka mwenzangu aliponiamsha kunitaarifu kwamba mwalimu alikua ameingia darasani.

Nilipoinuka mwalimu Yule alikua akinitazama kisha akaniita mbele ya darasa na kuanza kunikazia macho kwa dakika takribani moja pasina kusema chochote.

Hapo nilianza kuona jasho likinitoka huku hirizi niliyovaa ikinibana kwa nguvu kuashiria hali ya hatari, ghafla nilisikia sauti ya mama ikiniambia
“mkazie macho kisha weka nyuma mkono wa kushoto na wa kulia kunja ngumi”. Kwakua niliona hali ya hatari mbele yangu sikusita kufanya kama mama, alivonielekeza ambapo nilimshuhudia pia mwalimu Yule akianza kutweta huku shati lake alilovaa likiloa jasho nami niliendelea kukunja ngumi kwa nguvu zote.

“mtafanya zoezi la 3.1”. aliongea mwalimu huyo ambapo wanafunzi walishangilia kwani hakukua na yeyote aliyependa hesabu mle darasani.

Nilishusha pumzi ndefu na kurudi kuketi kwenye dawati na kuendelea kupiga usingizi hadi saa nne ilipofika hakukua na mwalimu alieingia darasani.
Nilishusha pumzi ndefu na kurudi kuketi kwenye dawati na kuendelea kupiga usingizi hadi saa nne ilipofika hakukua na mwalimu alieingia darasani.

“leo walimu wamechoka kufundisha eeh”. Alihoji rafiki yangu
“eee hata hivyo ni mwisho wa mwezi watakua wameenda mjini kuchukua mishahara yao”. Niliongea ambapo mwenzangu aliniunga mkono kisha tulienda kupata vifungua kinywa ambapo yalikua ni maandazi makavu.

Baada ya hapo tuliingia darasani ambapo masaa yaliyoyoma hadi alipokuja mwalimu fransi na kukuta darasa likiwa katika hali ya makelele mengi
“montress”. Aliita ambapo darasa lilikua kimya
“naomba majina ya wapiga kelele”. Aliongea mwalimu Yule ambapo nilishangaa montress akipeleka karatasi kwa mwalimu na hata sijui majina yaliandikwa saa ngapi.

Katika majina hayo jina langu lilikuepo na hata sikujua ameniona saa ngapi nikipiga kelele.

Tulipita mbele kisha aliagizwa mtu kufuata viboko na aliporudi navyo mwalim fransi aliahirisha kutupigia darasani

“hawa wakirudi watawasimulia kitakachowakuta”. Aliongea fransi huku akifunga mlango wa darasa.
Tulitoka na kwenda ofisi ya walimu tulipigwa fimbo nyingi sana hadi kengele ya kwenda mstarini kwaajili ya kutawanyika kwenda makwetu inagongwa bado tulikua ofisini ndipo mwalimu fransi aliamuru tutoke na tusirudie tena kupiga kelele.
Jambo hili.

lo liliniuma sana, kupigwa bila kosa tena fimbo nyingi namna ile. Niliapa kumwambia mama kwani nilikua nimewakariri walimu wote waliohusika katika adhabu ile na wakwanza kabisa alikua frans akifuatiwa na budodi ambaye alikuja kunipima darasani.
“hawa walimu watajuta na kimbelembele chao, naenda kumwambia mama”.

Je nini kilifuata
 

Dr santos

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 4, 2023
Messages
251
Reaction score
571
Points
0
SEHEMU YA TANO
(nakua mchawi rasmi na kuanza kuroga)

INAENDELEA; nilirudi nyumbani na kumkuta mama anaosha vyombo, nilianza kulia nilipomuona hali ile ilimfanya mama anifuate nilipo kwani nilijidondosha chini pia.

“mwanangu wamekufanya nini huko shuleni? Au ndo Yule mwalimu mchawi”. Aliongea mama kwa mshangao nami sikmjibu chochote zaidi nilijigusa sehemu za makalio huku nikiugulia maumivu ya hali ya juu.

Mama aliniinua na kunipeleka ndani kisha akanikagua jinsi nilivyoumia, mama alipatwa na hasira sana na kuniuliza.
“unawakumbuka walimu waliohusika katika hili”.
“ndio”. Nilimjibu ambapo aliniambia nisubiri usiku tuwaoneshe kazi. Baada ya hapo dada aliniletea maji na kunisaidia kujikanda kisha alinisihi nipumzike kwani kulikua na kazi kubwa sana usiku wa siku hio, kwanza ilikua ni kukamilisha masuala ya kafara pamoja na kuapishwa rasmi kua mchawi.

Masaa yalisogea na hatimaye usiku wa manane alikuja mama kuniamsha, ambapo nilipofungua macho mama na dada walikua wamekwishavaa nguo za maalum na walikua wananisubiri mimi tu.

Baada ya mimi kuvaa kaniki tuliketi chini na kutengeneza pembe tatu, dada na mama walikaa sambamba nami nilikaa mbele yako kisha tulitazamana na kusshikana mikono kisha kupotea.

Nilikuja kustuka na kukuta tupo makaburi ya jana ambayo sikujua yalikua yanapatikana kiiji gani kwani ilionesha ni nje na kijiji chetu.

“haya mwanangu hii kazi utaifanya wewe ukifuata maelekezo yangu”. Aliongea mama huku akinipa kibuyu na kuniambia nizunguke kaburi mara kumi na saba kwani tulikuja kabla ya muda.

Baada ya kuzunga alinielekeza nilale juu ya kaburi tena ambapo nilishangaa jeneza likipanda juu kisha mama aliniambia nishuke kisha akanipaka dawa maalum ambayo imetengenezwa kwa manyoya ya bundi na ya mnyama gani sijui, nimemsahau kidogo kisha mama aliniambia nifungue jeneza lile ambalo kwa mwonekano lilikua la gharama kubwa sana.

Baada ya kufanya ivyo walikuja mama na dada ambapo tulisaidiana kumbeba na tukapotea eneo lile kisha tulitokea kwenye uwanja wa mikutano ambapo leo haukua shuleni bali ilikua ni njiapanda yenye pacha sita kwenda vijiji mbalimbali.
Tuliwakuta wachawi wengi sana , ngoma zilipigwa na walikua wakicheza na kuimba nyimbo mbalimbali kwa lugha ambayo sikuielewa. Kwakua maelekezo nilishapewa na mama juu ya namna ya kufanya.
Nilienda kuweka maiti ile kwenye sehemu maalum kisha nilisogea hadi kwa mkuu na kupiga goti ambaye nae alinisogelea kisha kuniwekea usinga kichwani na kuanza kutabana maneno yasiyoeleweka kwa muda wa dakika mbili kisha alinipaka kwenye paji la uso dawa ambapo illikua inauma na kunifanya nitoe machozi kwa maumivu makali.

Baada ya hapo aliniambia nimwekua mchawi rasmi nizingatie ninayoelekezwa na nitakua na nguvu sana kwani nyota yangu ilikua ina nguvu sana.
Baada ya kusema hayo yote tulikula nyama na kutawanyika katika eneo la mikutano ambapo iliku ani wasaa wa kila mmoja kuendelea na shughuli za kichawi.
{wachawi hukaa vikao kwa dakika kadhaa na kupeana mawili matatu pamoja na adhabu kali kwa waliotenda makosa kisha baada ya hapo hutawanyika kuendelea na shughuli za kila
siku ulozi na kuroga}

Mama aliniambia ule ndio ulikua wasaa wa mimi kulipa kisasi kwa walimu wote walionipiga, kwakua nilimuonea huruma kiongozi wa darasa [montress) sikumjumusiha kwenye adhabu hio.

mama alinipa kijiti kilichokua kama manati na kuniambia ninuize nyumba ambayo nilihitaji kwenda, bila kuchelewa nilinuiza nyumba ya fransi na sekunde hio hio tulikua pale kisha mama alianza kukatika viuno kisha aligeuka kinyumenyume na kuanza kunengua huku akirudi nyuma hadi ulipotokea uwazi kwenye nyumba ya mwalimu fransi.

Tuliingia na tulimkuta mwalimu fransi peke yake ambapo tulisaidiana na mama kumgeuza kisha mama alimpiga viboko vingi sana zaidi ya mia hadi niliingiwa na huruma kisha akanikabidhi fimbo nyingine na kuniambia na mimi nimchape niwezavyo baada ya kuridhika tuliondoka na kumwacha mwalimu fransi kisha tulitoka nje na kumkuta dada ambaye alikua akilinda na kama kungetokea baya lolote nje basi angetupa taarifa.
“safari wapi sasa, si uliwataja

wawili?” aliongea mama ambapo sikukawia nilinuiza jina la budodi na ghafla tulikua nje ya nyumba ya budodi.

Tulipofika tu mama na dada walisema budodi nae ni mzito tusingeweza kumuingia kiurahisi kisha dada alichukua kamba moja ndefu ambapo alinyoosha mkono ukatokea mfuko mweusi ambapao ulikua na harufu kali ya kinyesi.
Dada aliniambia nikakiweke mlangoni kwa mwalimu huyo nami nilifanya hivo na kingine niliweka kwenye karo lake la vyombo.

Kisha dada aliniambia kawaida ya wachawi ni kulipa kisasi, na lazima atayaroga mavi yaye ambayo bila kujua ni ya kwake hivyo atajiroga mwenyewe.

Je nini kilifuata
 

Dr santos

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 4, 2023
Messages
251
Reaction score
571
Points
0
SEHEMU YA SITA
INAENDELEA; Kulipokucha nilijihimu shuleni kama kawaida lakini nilipofika shuleni niligundua kabisa hali haikua sawa, kwanza tulichelewa sana kuingia madarasani na pili walimu walikua wamejikusanya nje ya ofisi na ilionekana kuna jambo halikua sawa.

Nilipata kiwewe na wazo lililokua katika akili yangu ni kwenda ofisini tatizo lilikua nitaenda kufanya nini. Nikiwa katika mawazo nilimuona montress akitoka ofisini na niliona huo ndio ulikua wasaa wa kumuuliza .

Alipokatiza mbele yangu nilimwita na hakusita alikuja
“mambo “. Nilimsalimia
“poa vipi clara”. Alijibu
“poa tu, eti wanaongelea nini pale”. Nilimuuliza swali la mtego
“aaaah nimesikia tu wanasema mwalimu frans, sijui wachawi wamemchapa fimbo usiku sahizi hajiwezi”. Aliongea montess nami sikuridhika kabisa nilitaka kujua wana mpango gani baada ya jambo hilo.

Nilijigeuza nzi haraaka na kwenda jirani na ofisi ambapo nilimsikia mwalimu budodi akilalamia pia kwa kitendo cha kuwekewa kinyesi mlangoni.

“hawa wachawi lazima ni watakua hawa hawa wanafunzi, na istoshe hawataki tuwachape aise kufanya kazi kijijini tabu kweli”. Aiongea budodi kisha akamtuma mwanafunzi mmoja akagonge kengele ya mastarini.
Haraka nilijigeuza kua binadamu na kutokea mahali walipo wenzangu alikuja mwalimu mkuu pamoja na walimu wengine
“hamjambo”. Aliongea mwalimu mkuu ambapo wote tulijibu huku kila mmoja akiwa na shauku ya kutaka kujua jambo gani linalotaka kuongelewa kwa wakati huo.

“natumai mu wazima wa afya lakini kuna wenzenu hapa inasadikika kua ni wachawi na wanawaroga walimu wao”. Kauli hio iliniudhi sana ambapo nilijigeuza kua nzi na kwenda kutua kwenye paji la uso la mwalimu mkuu ambaye ghafla alibadilisha kauli.

“hata hivyo mimi siamini uchawi kwa hio hilo suala silisadiki hata kidogo lakini kazaneni kumuomba mungu”. Aliongea mkuu wa shule kauli ambayo ilikua na utata kidogo kwani walimu walishangaa sana mkuu wa shule kuwageuka na kukana kwamba haamini uchawi.

Baada ya kuruhusiwa kwenda darasani nilitumia nafasi hio kwenda nyumbani kwa mwalimu fransi ambapo nilimkuta ameketi nje huku akijikanda na akiapa kumkomesha aliyefanya jambo hilo na kumuendea kwa mganga.

Baada ya muda waikuja walimu wote kumsalimu na kumpa pole kisha budodi akauliza ..
“umesema huyo mwanafunzi sura yake sio ngeni”. Aliongea mkuu wa shule
“ndio anasoma darasa la nne”. Aliongea fransi na kunifanya nipate mstuko sana na hapo nilibinya hirizi kaka mama alivonielekeza na ghafla nilimuona akija kwa njia ya nzi
“kulikoni “. Aliuliza
“hebu waskize hawa watu”. Niliongea
“mmmh hii ngoma nzito, hebu nimwite dada yako tujue tunafanyaje”. Aliongea mama na kufanya mambo yake ambapo baada ya muda dada alikuja kama kipepeo.

{wachawi huweza kujigeuza kwa maumbile tofauti, wadudu au wanyama”}.
Dada alipofika alisema kazi iliyopo ni kumpumbaza frans asiende kwa mganga ila huyo mwengine atajilipua mwenyewe.
Baada ya hapo dada alisogea upande alipo fransi na kumchapa kibao kisha kumuuliza.

“umesema unamfahamu mwanafunzi mchawi”. Aliongea ambao nilimsikia mwalimu fransi akikana kwamba hamfahamu na hadhani kama kuna mwanafunzi anaeweza kumroga.

“kazi imeisha”. Alisema dada kisha tukaondoka nami kurejea darasani.
Hakuingia mwalimu yoyote siku hio hii ilifanya tucheze na makelele yalikua ya hali ya juu, baada ya hapo tulirejea makwetu.

Usiku kama kawaida tulienda kwenye shughuli zetu za kuwanga ambapo safari hii tulienda kuwanga kwenye nyumba ya jirani yetu aliyekua mlokole.

{Ndugu hamna mtu mbaya kama mchawi, kwani mchana anaweza kukuchekea na usiku akufanyie ulozi kama kawaida}

Siku hio tulifika na kuingia vizuri ndani ya nyumba hio tulianza kuwakaba watoto kisha tukaingia chumbani kwa jirani yetu na kwakua alikua mwanaume pekee na alikua hajaokoka tulimkaba na kumgaragaza ipasavyo kisha kuondoka zetu kwakua muda ulikua umekwenda tulirudi nyumbani.

*******"""
Taaarifa za msiba wa mwalimu budodi zilikua ni za ghafla sana na hakuna aliyeamini, siku hio wanafunzi tuliondoka mapema sana shuleni na mama pia alinikataza nisiende kabisa msibani kwani ni mwiko kwenda msiba ambao wewe

unahusika kwa asilimia miamoja. Nilikubaliana na mama ki shingo upande kwani nilihitaji kujua kwenye msiba wa kichawi nini hutokea.
Lakini niliogopa yasije kunikuta makubwa na tahadhari nilishapewa.

{labda nikudokeze kidogo watu hawa wana sifa za kujiunga na uchawi; wabishi,wanawake wagumu yaani wale ambao wanaishi peke yao na mtu anaependa kujitenga na kukaa peke ake]

Je nini kilifuata
 

Dr santos

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 4, 2023
Messages
251
Reaction score
571
Points
0
SEHEMU YA SABA.

INAENDELEA; walimu wengi walihama katika shule niliyokua nikisoma na hii ilipelekea taaluma kushuka kwa kiasi kikubwa kwani walimu wapya walikua na weledi mdogo kushinda walioondoka na wengi walikua wakijali maslahi yao binafsi kuliko kazi.

Nilikua mchawi kamili nilieweza kufanya ulozi peke yangu na kutoa kafara peke yangu pia kujilinda kama ikitokea hali ya hatari.

Siku moja mama aliniambia kuna kazi ambayo atakwenda kumsaidia rafiki yake ambayo ilikua ni kwajili ya uchawi wa mashambani, na ingekua vizuri mimi nikashiriki pia.

Sikua na tabu wala sikuwaza juu ya hatari yoyote kwani nilimwamini sana mama na kwakua dada alikua kashaondoka nilifanya kila kitu pamoja na mama na wakati huo nilikua darasa la saba.

Majira ya usiku wa manane alikuja mama kuniamsha na kisha tulipotoka nje tulimkuta rafiki wa mama na hatukuchukua muda tulipaa na kutokea nje ya geti la hospitali ya wilaya ya namanyere.

Tulimwona mlinzi ambaye aliweka pambo tu kwani kiuhalisia hakuwepo pale nae alienda katika shuhuli za kilozi.

Tulipita kwa njia ya kawaida na kwenda hadi kwenye wodi ya watoto ambapo mama alinambia nisubiri ndani ya choo na wao wangekua wakileta vitovu vya watoto.

Nilikaa na kusubiri kwa dakika kama tano alikuja mama na vitovu zaidi ya ishirini kisha baada ya muda alikuja rafiki wa mama na vitovu vitano kisha tukaweka mduara na kupotea tena.

{vitovu vya watoto wachanga vina kazi kubwa sana kwa wachawi pia ni biashara kubwa sana kwa waganga wa jadi kwani hutumika katika mitego ya kichawi hususani kwenye mapenzi, limbwata na kulinda ndoa pamoja na ulozi wa mashambani kupata mazao mengi}

Tulitokea nje ya mochwari ambapo niliambiwa nisubiri hadi pale watakapokuja kwani walienda kubeba maji ya kuoshea maiti kwani yalikua ni muhimu sana wa kazi hio.
Dakika chache niliweza kuwaona walozi wengine wakiwa nanakuja eneo nililopo nilinyoosha kidole na kuwaelekeza upande mwingine kama alivonielekeza mama.

{Ndugu kuna uchawi unaowea kuitawala akili na kuiendesha, unaweza ukakuta ulipanga kupita njia hii lakini ghafla ukabadili na kukata kona kupita njia nyingine kuna mawili hapo}

Baada ya muda mama alirejea ambapo aliniambia sasa ndo tunakwenda kuroga mazao ya watu kichawi

Tulishikana mikono na kutokea kwenye shamba moja kubwa sana mama aliniamba tutafukia vitovu vitano kwenye shamba la mama huyo kisha vitovu vingine tutaweka kwenye mashamba ya watu wengine kwaajili ya kuvuta mazao.

Kazi hio ilikua ngumu sana lakini tulimaliza saa kumi na moja alfajiri kisha mama aliniambia siku hio atakuja kutusaidia kazi hio hio kwenye shamba letu.

Nilikuja kuamka majira ya saa sita mchana ambapo nikuta mgeni sebleni ambaye alinisalimia nami nilimuamkia kisha kutoka nje.

Ambapo nilimkuta mama akiwa kwenye hali ya mawazo sana sijui kwanini mama alinificha labda pengine angeniambia tungeweza kuokoa jahazi.
Mama alikua amefanya kosa kubwa sana la kushirikiana na mtu anaetumia uchawi aina nyinginena adhabu yake ilikua ni kifo.

Baaada ya mgeni huyo kuondoka masaa yalikwenda kwa kasi atimaye ilifika jioni huku mama akiwa na hali ile ile ya unyonge na hata ulipofika usiku wa manane mama hakja kuniamsha kama ilivokua kawaida yake na kupelekea nipitilize hadi asubuhi.

Na kwakua nilikua nikijihimu shuleni sikuhitaji kumsumbua mama kwani niliamini alikua katika uchovu wa hali ya juu hivyo niliondoka bila kumsalimu wala kumuaga mama.

Hali ya ukimya wa hali ya juu ndio ulionistua huku kila kitu nikikikuta kama nilivokiacha mlango ulikua wazi na chumba cha mama kilikua kimefungwa.

Niliamua kufungua na kuingia nilipomgusa mama ilionesha ameshakata kauli mda mrefu. Niilia sana kwani ni rasmi nilikua yatima yote hii kwa sababu ya uchawi.

Jambo hilo likanifanya niamini kwamba maisha ya mchawi ni mafupi sana, na anaweza kufa muda wowote kwa kifo kisichoeleweka.

Baada ya kumzika mama nilitokea kuuchukia uchawi na hapo niliamua kuokoka na kuachana kabisa masuala ya ulozi.

Sasa najishughulisha na kilimo kwani mashamba na nyumba ndio urihi pekee nilioachiwa.

mwisho
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Ngoja niagize kimbora kende ya kushoto ije kulia afu dushee Ina erect kwenda chini🤣🤣🤣
Haha huyu dogo nasubiri amalize shule nintumie nauli akatembee gamboshi
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
SEHEMU YA SABA.

INAENDELEA; walimu wengi walihama katika shule niliyokua nikisoma na hii ilipelekea taaluma kushuka kwa kiasi kikubwa kwani walimu wapya walikua na weledi mdogo kushinda walioondoka na wengi walikua wakijali maslahi yao binafsi kuliko kazi.

Nilikua mchawi kamili nilieweza kufanya ulozi peke yangu na kutoa kafara peke yangu pia kujilinda kama ikitokea hali ya hatari.

Siku moja mama aliniambia kuna kazi ambayo atakwenda kumsaidia rafiki yake ambayo ilikua ni kwajili ya uchawi wa mashambani, na ingekua vizuri mimi nikashiriki pia.

Sikua na tabu wala sikuwaza juu ya hatari yoyote kwani nilimwamini sana mama na kwakua dada alikua kashaondoka nilifanya kila kitu pamoja na mama na wakati huo nilikua darasa la saba.

Majira ya usiku wa manane alikuja mama kuniamsha na kisha tulipotoka nje tulimkuta rafiki wa mama na hatukuchukua muda tulipaa na kutokea nje ya geti la hospitali ya wilaya ya namanyere.

Tulimwona mlinzi ambaye aliweka pambo tu kwani kiuhalisia hakuwepo pale nae alienda katika shuhuli za kilozi.

Tulipita kwa njia ya kawaida na kwenda hadi kwenye wodi ya watoto ambapo mama alinambia nisubiri ndani ya choo na wao wangekua wakileta vitovu vya watoto.

Nilikaa na kusubiri kwa dakika kama tano alikuja mama na vitovu zaidi ya ishirini kisha baada ya muda alikuja rafiki wa mama na vitovu vitano kisha tukaweka mduara na kupotea tena.

{vitovu vya watoto wachanga vina kazi kubwa sana kwa wachawi pia ni biashara kubwa sana kwa waganga wa jadi kwani hutumika katika mitego ya kichawi hususani kwenye mapenzi, limbwata na kulinda ndoa pamoja na ulozi wa mashambani kupata mazao mengi}

Tulitokea nje ya mochwari ambapo niliambiwa nisubiri hadi pale watakapokuja kwani walienda kubeba maji ya kuoshea maiti kwani yalikua ni muhimu sana wa kazi hio.
Dakika chache niliweza kuwaona walozi wengine wakiwa nanakuja eneo nililopo nilinyoosha kidole na kuwaelekeza upande mwingine kama alivonielekeza mama.

{Ndugu kuna uchawi unaowea kuitawala akili na kuiendesha, unaweza ukakuta ulipanga kupita njia hii lakini ghafla ukabadili na kukata kona kupita njia nyingine kuna mawili hapo}

Baada ya muda mama alirejea ambapo aliniambia sasa ndo tunakwenda kuroga mazao ya watu kichawi

Tulishikana mikono na kutokea kwenye shamba moja kubwa sana mama aliniamba tutafukia vitovu vitano kwenye shamba la mama huyo kisha vitovu vingine tutaweka kwenye mashamba ya watu wengine kwaajili ya kuvuta mazao.

Kazi hio ilikua ngumu sana lakini tulimaliza saa kumi na moja alfajiri kisha mama aliniambia siku hio atakuja kutusaidia kazi hio hio kwenye shamba letu.

Nilikuja kuamka majira ya saa sita mchana ambapo nikuta mgeni sebleni ambaye alinisalimia nami nilimuamkia kisha kutoka nje.

Ambapo nilimkuta mama akiwa kwenye hali ya mawazo sana sijui kwanini mama alinificha labda pengine angeniambia tungeweza kuokoa jahazi.
Mama alikua amefanya kosa kubwa sana la kushirikiana na mtu anaetumia uchawi aina nyinginena adhabu yake ilikua ni kifo.

Baaada ya mgeni huyo kuondoka masaa yalikwenda kwa kasi atimaye ilifika jioni huku mama akiwa na hali ile ile ya unyonge na hata ulipofika usiku wa manane mama hakja kuniamsha kama ilivokua kawaida yake na kupelekea nipitilize hadi asubuhi.

Na kwakua nilikua nikijihimu shuleni sikuhitaji kumsumbua mama kwani niliamini alikua katika uchovu wa hali ya juu hivyo niliondoka bila kumsalimu wala kumuaga mama.

Hali ya ukimya wa hali ya juu ndio ulionistua huku kila kitu nikikikuta kama nilivokiacha mlango ulikua wazi na chumba cha mama kilikua kimefungwa.

Niliamua kufungua na kuingia nilipomgusa mama ilionesha ameshakata kauli mda mrefu. Niilia sana kwani ni rasmi nilikua yatima yote hii kwa sababu ya uchawi.

Jambo hilo likanifanya niamini kwamba maisha ya mchawi ni mafupi sana, na anaweza kufa muda wowote kwa kifo kisichoeleweka.

Baada ya kumzika mama nilitokea kuuchukia uchawi na hapo niliamua kuokoka na kuachana kabisa masuala ya ulozi.

Sasa najishughulisha na kilimo kwani mashamba na nyumba ndio urihi pekee nilioachiwa.

mwisho

Mwisho mzuri njooni
Little
Katkit
Urban Edmund
mmash
Watoto wa kidugala
D Masserati.
AlmightyGod
Muhindi Wa Kuchoma
Leejay
February girl
Aalii
Miss Alpellah
Miss KF
Missy Gf
Hakimu
 

Dr santos

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 4, 2023
Messages
251
Reaction score
571
Points
0
Haha huyu dogo nasubiri amalize shule nintumie nauli akatembee gamboshi
gamboshi kuna treni za mwendo kasi afu mchana pori usiku ni kama brussel belgium
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
gamboshi kuna treni za mwendo kasi afu mchana pori usiku ni kama brussel belgium
huyu dogo ngoja tuone atakuja leta ushuhuda hapa

Akiamini uchawi tu. Lazima ataamini na Mungu yupo
 

Dr santos

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 4, 2023
Messages
251
Reaction score
571
Points
0
huyu dogo ngoja tuone atakuja leta ushuhuda hapa

Akiamini uchawi tu. Lazima ataamini na Mungu yupo
ma developer wanaamini kwenye computer
 

Hakimu

Immortal Village Hero
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 3, 2023
Messages
2,711
Reaction score
6,226
Points
113
Sehemu ya pili na ya tatu haipo?
 

Similar threads

  • Article Article
MWANZO Huu ni mkasa wangu ulionikuta baada ya kuhamishwa kutoka kigoma to dar es salaam early 2004s Baada ya kumaliza kazi zangu za kila siku ni kawaida yangu kutembelea kijiwe kwaajili ya kupata mawili matatu kutoka kwa watu mbalimbali wa rika tofauti lengo ni kutokua mpweke pia ku refresh...
Replies
60
Views
2K
Papa Francis amewaruhusu mapadre kuwabariki wapenzi wa jinsi moja, yakiwa ni maendeleo makubwa kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja na mahusiano mengine ya kijinsia wanaofahamika kama LGBT katika Kanisa Katoliki la Roma. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki la Roma amesema makasisi wanapaswa...
Replies
9
Views
281
habari zenu hii ni true story by manenge. leo nimeona niwape japo kwa kirefu sana kuhusu hii kazi yangu ya professional tour guide,kwa majina yangu nileyepewa na wazazi wangu naitwa raymond joseph mushi,nimzaliwa wa machame. nimeona ni share nanyi ilimjue kuhusu hii kazi ambayo haina...
Replies
43
Views
1K
JINSI YA KUREJESHA KWA KUPAKA RANGI CHUPA ZA KIOO Chupa za kioo (glass) ziko za aina nyingi, zenye rangi, na ambazo hazina rangi yaani (transparent). Chupa hizi mara nyingi huwa ni mabaki/uchafu (trash) baada ya kutumia vilivyo ndani kama jibini, soda, bia, juice, mafuta, unga, asali au...
Replies
10
Views
696
Kusanya vipande vya sabuni Ni bora kutumia sabuni isiyo na harufu; kwa njia hii, unaweza kuongeza harufu yako mwenyewe. Ikiwa unataka kutumia sabuni yenye harufu nzuri, hakikisha kwamba mabaki yote yana harufu sawa, vinginevyo unaweza kuishia na mchanganyiko wa harufu mbaya. Ikiwa unataka...
Replies
6
Views
506

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom