Jua mambo 25 ya ajabu kuhusu paka

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Hakimu

Immortal Village Hero
Jun 3, 2023
2,594
6,055
2,100
1712509486296.png

1)Kama ingetakiwa paka awe na kitambulisho cha NIDA Basi asingesajili kwa alama za vidole bali angesaini kwa alama ya Pua kwa sababu kwa kupitia pua zao ndio utapata upekee wa kila paka duniani

2) Paka wengi ni mashoto kwa maana miguu yao ya kushoto ndio hutawala katika shughuli zao nyingi

3) Siku zote paka ni wapole. ..hawapigani kwa ajili ya kuonyesha umwamba wao ukimuona paka anapigana ujue anapigania haki yake hasahasa kulinda himaya yake....

4) Watu wa zamani wa Misri walikuwa wakinyoa nyusi zao ilikuonyesha majonzi Iwapo paka wao wa nyumbani atafariki

5) Uwezo wa paka kunusa ni mara 14 zaidi ya uwezo wa binadamu

6) Paka anaweza kuruka hadi futi 8 kwenda juu...anaweza kuruka mara sita ya urefu wa mwili wake

7) Paka ana akili nyingi kuliko mbwa kwa sababu paka ana zaidi ya neurons million 300 wakati mbwa ana neurons million 160 huku binadamu akiwa na zaidi ya neurons bilion 80 (hizo neurons bilion 80 kwa binadamu ni asilimia Kati ya 10-20 ya akili ya binadamu)

8) Paka anaweza kuishi hadi miaka 30 ...Hadi sasa paka anayeshikilia rekodi ya dunia ya kuishi umri mrefu ni Paka Creme Puff aliyeishi miaka 38 na siku 3 ...paka huyo aliishi huko Texas nchini marekani

9) Paka anavyolia nyau (Meous) huwa anawasiliana na binadamu pekee ...wao wenyewe kwa wenyewe hawawasiliani kwa kulia nyau (meous)

10) Paka huweza kujitibu majeraha kwa kukoroma (purring) ... Paka wa nyumbani huweza kuzalisha frequency Kati ya 25 hadi 150 hertz ...Kwa kiwango hiko kinaweza kusaidia mifupa na misuli kukua vizuri na pia kujitibu yenyewe

11) Paka hawezi kuhisi ladha ya utamu

12) Mapigo ya moyo ya Paka yanapiga mara mbili zaidi ya Mapigo ya moyo ya binadamu kwa Paka ndani ya dakik 1 hupiga kati ya 110 -140 wakati kwa binadamu ndani ya dakik 1 hupiga kati ya 60 hadi 100

13) Mwaka 2004 wana akiolojia kutoka ufaransa waliweza kugundua kaburi (mifupa) ya paka inayokadiriwa kuwa ni ya zaidi ya miaka 9500 huko nchini Cyprus.... Hapo awali watu waliamini kuwa paka walianza kuishi nchini misri

14) Paka Stubb alishawahi kuwa meya wa Talkeetna kwa miaka 20... Talkeetna ni mji mdogo wa Alaska ....Kwa Miaka 20 alikuwa anakosa Mpinzani wa kugombea nae... Japo paka huyo Hakuwa anashika madaraka ya kiutawala lakini alikuwa anapendwa tu na watu wa Talkeetna

15) Paka mrefu (longest) zaidi duniani ni Stewie alikuwa na urefu wa inchi 48.5 wakati paka mrefu kwenda juu (tallest) zaidi duniani ni Arcturus alikuwa na urefu wa kwenda juu wa inchi 19.05

16) Asilimia 70 ya maisha ya paka wanayatumia kwa kulala... ( Kwa mfano kama paka ataishi miaka 10 Basi miaka 7 ataitumia kwa kulala)

17) Paka anayeshikilia rekodi ya utajiri zaidi duniani ni Paka Blackie...utajiri wa paundi million 7 ...ambazo kama tutazibadili kwa thamani ya pesa ya Tanzania ya sasa ...tunaweza kusema kuwa paka huyo alikuwa na zaidi ya utajiri wa Billion 20 na million 900

18) Kama hujawahi kumuona Twiga akitembea au kama hujawahi kumuona Ngamia akitembea Basi kamuangalie Paka akitembea... Namna paka anavyotembea ni sawa na Ngamia anavyotembea au namna Twiga anavyotembea
kwahyo badala ya kusema mtoto ana mwendo wa Twiga Unaweza kumwambia tu kuwa mtoto ana mwendo wa paka 🤣🤣

19) Mwaka 1963 ndio paka wa kwanza duniani alikwenda angani... Paka huyo aliitwa Felicette ndio alikuwa paka wa kwanza na wa pekee kwenda angani

20) Kwa asilimia 80 maumbile ya paka yanafanana na Chui... Lakini pia baadhi ya tabia za paka hufanana na chui

21) Paka Ana speed ya 30mph wakati chui ana speed ya 40 mph Binadamu ana speed ya 28mph (hapo wameangaliwa akina Usain Bolt sio wewe kibonge 🤣🤣🤣🤣🤣 )

22) Paka ana mifupa 230 wakati binadamu ana mifupa 206

23) Paka anaweza kupata mimba akiwa na umri wa miezi minne

25) Paka alianza kuishi majumbani zaidi ya miaka 3600 BC
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
Jun 4, 2023
6,736
21,113
2,100
Darasa Zuri sana. Paka ukifuga ntaani hawachelewi kukuita mchawi
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
Jun 4, 2023
6,736
21,113
2,100
Sema kuna paka flani hivi wa kizungu wazuri kweli kweli natamani niwafuge kwa ajili ya wanangu
 

Similar threads

KOMBA(BUSH BABY) Ni mnyama jamii ya kima ambaye Ni mdogo kuliko wote ambaye anatembea usiku tu mchana analala (night monkey) Bush baby Ni Aina pekee ya kima ambaye muda mwingi wa Maisha yake anatumia akiwa juu ya mti. Bush baby Ana macho makubwa yanayomsaidia kuona wadudu gizani na masikio...
Replies
2
Views
195
MAMBA ni mnyama anayekula nyama, huweza kuishi nchi kavu lakini maisha yake kwa kiasi kikubwa hupendelea kukaa majini, tofauti na fikra za watu wengi ambao hufikiri mamba anazaa ukweli ni kwamba huwa anataga, ambapo kwa wastani hutaga mayai 35 mpaka 50, najua utajiuliza sasa huyu kiumbe...
Replies
4
Views
483
  • Article
Jumatatu naamkia makao makuu ya nchi , katika wiki kadhaa nyuma . Huko nafanya kilicho nipeleka , najipanga kurudi ila nasema wacha nimpigie rafiki yangu mmoja kutoka huko kwa washua ( Wahaya) Bila ajizi anapokea simu , makutano yanapangwa tunakuwa na muda mzuri sana kwenye kumbi za starehe...
Replies
23
Views
472
Hutakiwi kumbusu mtoto sikioni: Ukimbusu mtoto sikioni. Imekuwa ni kawaida ya watu kubusu watoto masikioni, wasijue hii inaweza mletea mtoto kuwa kiziwi. Bush hili ambalo hutambulila kama 'Busu lisilo na hatia' linaweza pia mletea mtoto maumivu ya maisha inapotokea ngoma imepasuka. English: An...
Replies
1
Views
212
Mambo ambayo mwanamke anatakiwa kujua kahusu sehemu zake za siri 1. Sehemu za siri zinajisafisha zenyewe Idadi kubwa ya wanawake, wana imani kuwa wakitumia bidhaa mbalimbali za urembo, kama sabuni basi ndio watajisafisha vizuri sehemu za siri. Hakuna haja ya kutumia chochote kusafisha sehemu ya...
Replies
12
Views
195

Recommendation

See popular novels


Kijiji Q and A


Engage in smalltalk


Let's grow up


Greats moments ever

Top Bottom