Lilith Mke wa kwanza wa Adam

Hakimu

Immortal Village Hero
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 3, 2023
Messages
2,714
Reaction score
6,235
Points
113
Lilith ni jina la mwanamke ambaye katika hadithi fulani za Mesopotamia ya kale anatajwa kama mungu mke ambaye anahusika na dhoruba akazaa majini.

Biblia inasimulia jinsi dunia ilivyoumbwa na mwanzo wa binadamu. Katika maandiko hayo, masimulizi ya uumbaji yana changamoto kuyafahamu sawasawa, hususani kitabu cha Mwanzo 1:26 na Mwanzo 2. Uumbaji wa mwanamke unatajwa sehemu hizo mbili, lakini kwa namna tofauti, kwa kuwa ni visasili tofauti. Katika Mwa 1:26 Mungu aliwaumba Adamu na Eva sawia kwa sura na mfano wake. Katika Mwa 2 Mungu anamuumba Hawa baada ya kuchukua ubavu wa Adamu na kumfanya mwanamke.

Katika Biblia Isa 34:14 tu inamtaja Lilith, na jina hilo linatafsiriwa pengine "Bundi", sambamba na wanyama wengine saba wanaotajwa katika mstari huohuo na ule unaofuata.

Hata hivyo kuanzia karne ya 10 BK wametokea watu wanaodai Lilith, si Hawa, ndiye mwanamke wa kwanza ulimwenguni naye aliumbwa na Mungu wakati mmoja na Adamu. Wanasema Lilith alifukuzwa na kukataliwa na Mungu baada ya kupatikana kuwa mwenye nguvu zaidi na mwenye akili zaidi ya Adamu na hakutii amri za Adamu.

Wanadai Lilith haitajwi katika kitabu cha Mwanzo kwa kuwa inakwenda kinyume na jadi ya kutaka mwanamke atii mwanamume na wanawake kuwa katika hali ya chini kuliko wanaume. Wanadai pia Biblia ya sasa imepitia vichujio vingi vya kidini ili kuhakikisha kwamba inapoteza baadhi ya sehemu muhimu. Hata hivyo, kuna sehemu ambayo imeachwa ndani yake (Mwa 1) ambayo inaonyesha kwamba Mungu hakumuumba mwanamume tu bali alimuumba mwanamke kwa wakati huohuo, badala ya simulizi la ubavu kuchukuliwa kutoka kwa Adamu kama ilivyopendekezwa kwenye sura ya 2.

Jibu la msingi la Wayahudi na Wakristo ni kwamba imani inawadai kupokea Biblia kama ilivyo sasa, si katika hatua za awali ambazo tena ni za kufikirika tu.
 
Lilith anajulikama kama mwizi wa watoto usiku

Inasemekana baada ya kumpa Adam tunda Lilith hakufaa tena kuwa ubavuni mwa Adamu kwa nia yake ya kutaka kiwa Kama Mungu.

Ni sahihi kabisa Biblia inaonyesha uumbaji kwa mwanadamu mara mbili
1. Mara ya kwanza aliumwa mwanaume na mwanamke kwa wakati mmoja
2. Mara ya pili aliumbwa mwanamke kutoka kwenye ubavu wa Adam
 

Similar threads

Wakuu ni uwakika? Mimi niko gud Mungu ni mwema. Sasa wandugu mimi nalileta kwenu jambo hili rafiki yangu alinishirikisha ili nimpe maushauri.. Jamaa yangu ana mke wake na amebahatika kupata ujauzito una miezi kama sita sasa, katika miezi yote ya ujauzito mambo yalikua sawa kabsa, ila kwanzia...
Replies
12
Views
318
Mmeamkaje Mke wa rafiki yangu anamsaliti mshikaji bila yeye kujua. Jamaa anaishi mtaa wa nne kutoka hapa nilipo. Mke wake anatoka na jamaa mmoja anaitwa Athumani. Wanajiachia hadharani bila kujali kuwa nafahamu hili Jana usiku nimekutana na mshikaji wangu wakati nazungumza nae mkewe anasema...
Replies
23
Views
699
  • Question Question
Mambo zenu wadau humu ndani Kuna mwanamke nimekua nae kwenye mahusiano mwezi wa saba sasa. Naomba mnisaidie jinsi ya kiachana nae maana nmejaribu nimeshindwa
Replies
7
Views
228
Mke Mtarajiwa huna haja ya kuhangaika na mabuzi nimetoboa sasa mimi ni raisi wa Kijiji. Mke wangu mtarajiwa, najua uko sehemu salama ni kuvuta muda na jamaa mwingine kabla hatujaoana. Lakini kabla sijakuweka ndndanninayo machache ya kukueleza.. 1. My future wife, Jiandae kuwa mother material...
Replies
13
Views
375
Mambo mchumba wangu Natafuta mchumba hapo baadae awe mke wangu. Kwanza ningependa tufahamiane kabla hatujafikia maswala ya ndoa. Sifa zangu Umri: Nina miaka 25 Elimu: Chuo (undergraduate) Dini: Mkristo (japo siendi kanisani) Urefu: 170cm Rangi: Mweupe Kazi: Natafuta kazi (nina kazi ndogo...
Replies
23
Views
300

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top