Mambo usiyo yajua kuhusu Mamba

Robot

Robot
Joined
Sep 9, 2023
Messages
42
Reaction score
15
Points
8
1704115313706.png

MAMBA ni mnyama anayekula nyama, huweza kuishi nchi kavu lakini maisha yake kwa kiasi kikubwa hupendelea kukaa majini, tofauti na fikra za watu wengi ambao hufikiri mamba anazaa ukweli ni kwamba huwa anataga, ambapo kwa wastani hutaga mayai 35 mpaka 50, najua utajiuliza sasa huyu kiumbe anaatamia vipi wakati maisha yake ni ya heka heka? Mamba hutengeneza kiota kwa kuchimba pembezoni mwa mto au ziwa na kisha kufukia mayai yake mpaka hapo ambapo mayai yatakapokuwa tayari.

Mayai yake yanapokuwa tayari kwa kutoa watoto, mamba husikia sauti na akiyatoa mayai hayo katika kiota watoto wake hujitoa wenyewe, yaani watoto hutumia nguvu binafsi na kuvunja gamba la yai, kisha hutoka katika ulimwengu mpya, kazi ya mama kwa wakati huo inakuwa ni kuhakikisha anawachukua wanawe na kuwapeleka majini na huwabeba kwa kutumia mdomo wake.

Wakati huu baadhi ya wanyama ambao huliwa na mamba nao hulipiza kisasi, mfano kenge, mijusi wakubwa pamoja na ndege, humtegea anapopeleka watoto wa awamu ya kwanza wale wanaosalia hujeruhiwa vibaya, au kubebwa kama chakula na wanyonge wa mamba. Hujisikia tabu kiasi kwamba anapoibuka katika maji huwatazama kwa jicho la shari.

Watoto wa mamba ukiwaona katika udogo wao wanashangaza, hutokaa ufikirie kwamba ndio hao wafikapo ukubwani hufikia urefu wa futi 10 na zaidi, uzito wa kilo zaidi ya 600, ni viumbe ambao huonekana wadogo unaweza kuhisi labda ni kenge.

Katika hatua za mwanzo watoto wa mamba hutumia samaki kama chakula chao, kwa kadri muda unavyokwenda watoto hao nao huanza kuwinda wanyama na zoezi hilo huwa jepesi kwa kuwa idadi kubwa ya wanyama hufuata maji katika makazi yao, mnyama mkubwa ambaye maisha yake huathiriwa na mamba ni nyumbu na hii ni kwa sababu pindi wanyama hawa wafikapo mtoni hukamatwa kwa urahisi kwa kukosa tahadhari ya kutosha.

Kwa taarifa yako, mamba ni miongoni mwa wanyama wakubwa duniani, meno yake yamejipanga kwa mfano wa msumeno, ana macho makubwa, ngozi ngumu na mkia mrefu ambao humsaidia katika kuwinda, hupendelea kukaa kwenye maji lakini jua linapochomoza na linapo karibia kuzama, ndio wakati hutoka majini na kukaa nchi kavu.

Ajabu ya mnyama huyu ni moja, pamoja kwamba wanyama wanaokula nyama tu ndio huishi muda mfupi, lakini yeye maisha yake ni marefu anaweza kufika miaka 50 na zaidi. Namna unayoweza kuwatofautisha kwa jinsia zao ni muonekano wao, dume huwa mrefu zaidi ya jike pia huwa mzito zaidi jike.



SIFA ZAKE ZA KIPEKEE
1. Ni mnyama ambaye ana uwezo mzuri na mkubwa katika kuyamudu maji hasa kuogelea.

2. Huishi katika maji baridi na makazi yake huweka sehemu zisizo na kina kirefu.

3. Mashambulizi yake ni ya kushtukiza, anaweza akawa anakuvizia na usijue kwamba yupo jirani kukukamata.

4. Ana akili na mjanja mno anapomuona mnyama ambaye hana uwezo wa kumkimbiza, hujifanya amelala usingizi ili uingie katika maji.

5. Pia anaweza kukukamata hata akiwa amelala usingizi, jicho lake moja huacha wazi anapolala na lina uwezo wa kufikisha taarifa ya kila kinachoendelea.

6. Huwa na nguvu maradufu awapo kwenye maji, ni vigumu kumshinda katika mapambano naye ndani ya maji.

7. Hapatani na simba kabisa kwa kuwa ndiye mnyama ambaye hupenda kumbughuzi awapo mapumzikoni, hivyo wawili hawa wanapokutana nchi kavu huwa kama watani.

8. Ni mwepesi wa kuzira kitu, hapendi kujitesa anapokutana na changamoto huamua kukaa pembeni.
 
Kuna watu wanakula nyama ya mamba, ikiwemo baadhi ya makabila Afrika.
 
Kuna imani kuwa nyongo ya mamba ni sumu kali sana. Ikitokea umeua mamba mnakamatwa kijiji kizima
 

Similar threads

KOMBA(BUSH BABY) Ni mnyama jamii ya kima ambaye Ni mdogo kuliko wote ambaye anatembea usiku tu mchana analala (night monkey) Bush baby Ni Aina pekee ya kima ambaye muda mwingi wa Maisha yake anatumia akiwa juu ya mti. Bush baby Ana macho makubwa yanayomsaidia kuona wadudu gizani na masikio...
Replies
2
Views
241
1)Kama ingetakiwa paka awe na kitambulisho cha NIDA Basi asingesajili kwa alama za vidole bali angesaini kwa alama ya Pua kwa sababu kwa kupitia pua zao ndio utapata upekee wa kila paka duniani 2) Paka wengi ni mashoto kwa maana miguu yao ya kushoto ndio hutawala katika shughuli zao nyingi 3)...
Replies
17
Views
628
  • Article Article
Jumatatu naamkia makao makuu ya nchi , katika wiki kadhaa nyuma . Huko nafanya kilicho nipeleka , najipanga kurudi ila nasema wacha nimpigie rafiki yangu mmoja kutoka huko kwa washua ( Wahaya) Bila ajizi anapokea simu , makutano yanapangwa tunakuwa na muda mzuri sana kwenye kumbi za starehe...
Replies
23
Views
502
Hutakiwi kumbusu mtoto sikioni: Ukimbusu mtoto sikioni. Imekuwa ni kawaida ya watu kubusu watoto masikioni, wasijue hii inaweza mletea mtoto kuwa kiziwi. Bush hili ambalo hutambulila kama 'Busu lisilo na hatia' linaweza pia mletea mtoto maumivu ya maisha inapotokea ngoma imepasuka. English: An...
Replies
1
Views
250
Mambo ambayo mwanamke anatakiwa kujua kahusu sehemu zake za siri 1. Sehemu za siri zinajisafisha zenyewe Idadi kubwa ya wanawake, wana imani kuwa wakitumia bidhaa mbalimbali za urembo, kama sabuni basi ndio watajisafisha vizuri sehemu za siri. Hakuna haja ya kutumia chochote kusafisha sehemu ya...
Replies
12
Views
250
Back
Top