Mantiki ya kutembelea waliokufa na kuwaombea

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Muhindi Wa Kuchoma

Well-known member
Platinum Villager
Joined
Jul 9, 2023
Messages
3,821
Reaction score
3,805
Points
113
Nini mantiki ya kutembelea waliotangulia mbele ya haki kuwaombea?
Kutokana na mafundisho ya dini nyingi kuwa mtu huona mbingu au pepo kunalingana na maisha yake aliyoishi hapa duniani. Kama maisha haya ni ya kumpendeza Mungu basi ataiona Pepo. Kama hayakuwa ya kumpendeza Mungu ataenda motoni
  • Wakristu baadhi huombea marehemu na wengine wanapinga kuombea marehemu.
  • Waislam wana siku ya kuombea marehemu na kusafisha makaburi.

Nini mantiki ya kwenda kaburini na kuongea na marehemu?
Kumekuwa na tamaduni baadhi ya watu kwenda kuzungumza na ndugu zao waliotangulia mbele za haki. Je kuna uwezekana unapozingumza na marehemu anasikia?

Nini mantiki ya kufanya ibada pale mtu anapofanyiwa maziko?
Tumeona safari ya mwisho ya marehemu lazima itafanyika ibada kwa ajili ya marehemu. Ibadi hii inaambatana na kumuombea Marehemu. Ukweli ni kwamba hata kama ukiombewa na wachungaji au masheikh wote duniani maisha yako ya hapo kabla ndio yatakayochangia kuona mbingu. Je ina maana kumfanyia ibada alitekufa?
 
Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Unajua Biblia inasemaje kuhusu kutembelea waliokufa?

Marko 16 1- 3
"Baada ya siku ya Sabato, Maria Magdalene, Salome na Maria mama yake Yakobo walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu. Basi, alfajiri na mapema siku ya Jumapili, walifika kaburini, jua lilipoanza kuchomoza. Nao wakawa wanaambiana, “Nani atakayetuondolea lile jiwe mlangoni mwa kaburi?”

Yohana 11:4
Lakini Yesu alipopata habari hizi alisema, “Ugonjwa huu hautaleta kifo bali umetokea ili kudhihirisha utu kufu wa Mungu. Kutokana na ugonjwa huu, mimi Mwana wa Mungu, nitatukuzwa. ”

Waislamu wanasemaje kuhusu kutembelea makaburi? Thawabu Ya Kwenda Kuzuru Makaburi Ya Ndugu Zetu Mumineen (Wenye Imani)
Siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliwaambia Masahaba: "Watuzeni maiti wenu? Wakauliza, "Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu tuwatuze nini maiti?" Akajibu Sadaka na Dua, tena akaendelea kusema, "Hakika roho za wenye imani siku ya Ijumaa kwenye mbingu ya kwanza sawa na mahala walipokuwa wakikaa majumba yao na kila mmoja wao hupiga kelele kwa sauti ya kuhunisha na kulia na husema, Enyi watu wangu, watoto wangu, baba na mama yangu na majamaa zangu, tuonee huruma na Mwenyezi Mungu Atakuoneeni huruma, kwa mali hiyo mliyo nayo ilikuwa mikononi mwetu, sasa haipo mikononi mwetu, mateso na hesabu tunafanyiwa sisi na faida yake wanafaidi wengine". Na kilamoja (roho) humpigia kelele jamaa zake.

Tuonee huruma kwa kutoa sadaka 'dirham' moja (pesa za zama zile) au kwa kutoa mkate kumpa maskini, au kwa nguo kumvisha asiekuwa na nguo, na Mwenyezi Mungu atakuvisheni nguo za "Janah" (Pepo). Baadaye Mtukufu Mtume (s.a.w) akalia na Masahaba pia wakalia, na kilio kilimshika kwa wingi hata hakuweza kusema. Baadaye akasema "Hao ni ndugu zenu katika dini (Imani) sasa wameshageuka udongo na mifupa imesagika baada ya kuishi humu duniani kwa raha na furaha, basi wanapiga kelele na kusema, "Ole juu yetu, laiti katika uhai wetu tungali toa sadaka na kutenda mazuri kwa (pesa zetu) hizo tulizokuwanazo katika njia ya Mwenyezi Mungu leo tusengelikuwa muhutaji wenu". Basi wanarudi wanyonge na huku wanpiga kelele, "Haraka toeni Sadaka kwa maiti wenu".

Inafaa kwa Mwislamu kila wiki kwa uchache hasa siku AIhamisi awakumbuke wafu wake kwa kufika kwenye makaburi yao, hii ni Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) akiwaamrisha Masahaba wake kuzuru makaburi.

Amepokea Bi Aisha (R.A.) na Abu Hurayrah (R. A.) kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.) amesema, "Amekuja Jibrili kwangu na akaniambia kwamba "Mola wako Anakuamrisha uende kwa watu wa 'AL-BAQEE' makaburini mwa watu wa Madina na uwaombee waghufuriwe". Nikasema (Aisha), "niseme nini ninapofika makaburini?" Akasema, Sema, "AS-SALAA-MU ALAA AHLID-DIYAAR, MINAL MU'MINEE-NA- WAL MUS-LIMEEN. YARHAM UL-LAA-HUL MUSTAK-DIMEE-NA-MIN-NAA, WAL MUS-TA'A-KHIREEN, WA IN-NAA IN-SHAA-AL-LAAHU Bl-KUM, LAA-HI KUUN.

Licha ya kuwepo wapokezi wa hadithi kuhusu jambo hilo kutokana na wanachuoni, wa Ki-Shia vile vile wamepokea hadith hizo wanachuoni wa Ki-Sunni nao ni: Bwana Muslim katika Saheeh yake, na Bwana Bayhaki katika 'Sunan' yake na pia Bwana Ahmad Bin Hambal, Bwana Abudaud, Bwana Tirmizi, Bwana Nasaina Bwana Baghawi.

Ni sunna unapofika kwenye kaburi uelekee Qibla, weka mkono kwenye hilo kaburi na soma mara saba (7) sura ya Innaa Anzalnahu (5:97) na pia bora usome sura ya AL-FAATlHA (S:1) na sura ya AL-FALAQ (5:113) na WAN-NASI (S:114) na sura ya QUL-HUWL-LAAHU (S:112) na Ayatul-Kursi kila moja mara tatu.

Ni sunna unapoingia makaburini usome:
"BlS-MIL-LAA-HIR-RAH-MAA-NIR RAHEEM, ASSALAA-MU ALAA AHLI LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, MIN AH-LI LAA-ILAA-HA IL-LAL LAAHI YAA AH-LA LAA-Llaa-HA, IL-LAL-LAAH, BI-HAK-KI- LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, KAY-FA WAJAD-TUM KAULA LAA-ILAA-HA-IL-LAL-LAAH MIN LAA ILAA-HA IL-LAL-LAAH, YAA LAA-ILAA-HA, IL-LAL-LAAH, BI HAK-KI LA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, IGH-FIR LIMAN KAA-LA LAA-ILAA-HA, IL-LAL-LAAH WAH-SHUR NAA, FIY ZUM-RATI MAN KAA-LA, LAA-ILAA HA IL-LAL-LAA-HU, MUHAM-MADUN RASUU-LUL-LAAH ALY-YUN WALIY-YUL-LAAH
Kwa kusoma haya Mwenyezi Mungu atambarikia msomaji thawabu ya kutenda mema ya miaka hamsini na kumsamehe madhambi yake na ya wazazi wake ya miaka hamsini.

Tunaomba kwa Mola Atupe tawfiki ya kuwakumbuka wafu wetu hasa wazazi kwa kuwatendea mambo ya heri kwa thawabu yao na kuwazuru makaburini kwa kuwa somea Fatha Amin. Na kwa kuzuru makaburi tutakumbuka kuwa kuna kufa (mauti), hao walikuwa kama sisi sasa hawajiwezi kujisaidia.
 
Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
dini zote ni chai,

achana na huu upotoshaji
Je kusafisha makaburi ni dhambi? Au Je usafi wa makaburini ni machukizo mbele za BWANA?
Awali ya yote,hatuna budi kujua kwamba makaburini ni eneo la ardhi lililotengwa kuzikia miili ya watu waliokufa.( Kumbuka;mwili hutokana na udogo,bali roho hutokana na Mungu,yaani mavumbi kuirudia ardhi na roho kumrudia Mungu – Mhubiri 12:7)

Hivyo kama mwili utairudia ardhi/udongo, hii ina maana- mtu afapo,basi atazikwa ili kukamilisha mchakato wa mwili kuurudia ardhi,na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa. Sasa,kama kuna “kuzika” basi ni lazima kuwepo na eneo la ardhi la kuzikia liitwalo “makaburini”.

Na kwa kuwa eneo hilo ni eneo maalumu pa kulazia miili ya wafu,basi ni haki mbele za Mungu lisafishwe na kutunzwa vizuri. Na ndio maana serikali imeweka mamlaka zake za kupatunza mahali pa kuzikia kwa mujibu wa sheria. Ikiwa kama kumejaa,serikali inatoa tangazo kupitia halimashauri ya Manispaa husika.

Kibiblia suala la makaburi limeelezwa vizuri,kuonesha ni suala la kawaida na ni muhimu sana. Ibrahimu alipokufa,naye alizikwa kwenye shamba/makaburini lililokuwa likitunzwa,(Naye Sara mkewe alizikwa hapo hapo kabla ya Ibrahimu).

Na tangu kipindi hicho tunaona utaratibu wa kutunza maeneo ya kuzikia ukiendelea mpaka leo. Kwa bahati mbaya leo kumezuka zana ya kupaona makaburini ni kama eneo la majini na mapepo,hivyo walokole wengine huogopa hata kukatisha huko,

au kwenda kufanya usafi hali wakidhani kufanya usafi katika eneo hilo ni sawa na kujiungamanisha na wafu!!!! kitu ambacho si kweli. Usafi kama usafi wa makaburini haukuungamanishi na wafu,isipokuwa ibada ya wafu huko makaburini ndio imekatazwa na ni mbaya mbele za Mungu.
 
mshamba_mkuu

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
1,563
Reaction score
4,525
Points
0

upuuzi mtupu, ndio maana africa hakuna maendeleo
 
Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Kitu ulichowahi kukifikiri kikakuletea impact kwa jamii ni kipi
Unanichosha kuandika nimefanya makubwa mengi tu
1. Nishawahi jenga msingi wa hospital Pwani huko kwa hela zangu mwenyewe. Wao wamalizie
2. Nimechangia sana CCM hata mtaani napoishi barua ya kwanza mchango huanzia kwangu
3. Nimechangia tofali ujenzi wa serikali za mitaa napoisho kama mdau mkereketwa
5 Nimeshawahi kuguswa tu nikachangia msikiti, nilipiga wiring msikiti nzima.

Mengine sitaki kuandika inatosha. Je wewe umefanya nini kuacha alama katika jamii? pamoja na mshamba_mkuu na Muhindi Wa Kuchoma
 
Muhindi Wa Kuchoma

Well-known member
Platinum Villager
Joined
Jul 9, 2023
Messages
3,821
Reaction score
3,805
Points
113
Unanichosha kuandika nimefanya makubwa mengi tu
1. Nishawahi jenga msingi wa hospital Pwani huko kwa hela zangu mwenyewe. Wao wamalizie
2. Nimechangia sana CCM hata mtaani napoishi barua ya kwanza mchango huanzia kwangu
3. Nimechangia tofali ujenzi wa serikali za mitaa napoisho kama mdau mkereketwa
5 Nimeshawahi kuguswa tu nikachangia msikiti, nilipiga wiring msikiti nzima.

Mengine sitaki kuandika inatosha. Je wewe umefanya nini kuacha alama katika jamii? pamoja na mshamba_mkuu na Muhindi Wa Kuchoma
Nimefanya kazi ofisi za kata mawazo yangu mengi yalisaidia sana jamii. Ikiwemo
1 kuwasaidia akina mama kuanzisha vyama vya vikoba

2 kupiga dawa mazingira ya kata yetu. Nilisimamia sana hili kwa kuwashawishi watu wachangie kidogo ndio maana hakukuwahi kuwa na magonjwa ya mlipuko wakati niko kata

3 Kusimamia stahiki za wazee kupitia TASAF na mipango mingine ya kiserikali

4 Magari ya taka ni machache nikaongea na jamaa mmoja kumshawishi nanikaetuma barua halmashauri kuwaomba tuongeze gari ya ziada
 
mshamba_mkuu

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
1,563
Reaction score
4,525
Points
0
Unanichosha kuandika nimefanya makubwa mengi tu
1. Nishawahi jenga msingi wa hospital Pwani huko kwa hela zangu mwenyewe. Wao wamalizie
2. Nimechangia sana CCM hata mtaani napoishi barua ya kwanza mchango huanzia kwangu
3. Nimechangia tofali ujenzi wa serikali za mitaa napoisho kama mdau mkereketwa
5 Nimeshawahi kuguswa tu nikachangia msikiti, nilipiga wiring msikiti nzima.

Mengine sitaki kuandika inatosha. Je wewe umefanya nini kuacha alama katika jamii? pamoja na mshamba_mkuu na Muhindi Wa Kuchoma
nimekataa dini.
 
The great manenge

New member
Platinum Villager
Joined
Jul 8, 2023
Messages
1,320
Reaction score
2,995
Points
0
Unanichosha kuandika nimefanya makubwa mengi tu
1. Nishawahi jenga msingi wa hospital Pwani huko kwa hela zangu mwenyewe. Wao wamalizie
2. Nimechangia sana CCM hata mtaani napoishi barua ya kwanza mchango huanzia kwangu
3. Nimechangia tofali ujenzi wa serikali za mitaa napoisho kama mdau mkereketwa
5 Nimeshawahi kuguswa tu nikachangia msikiti, nilipiga wiring msikiti nzima.

Mengine sitaki kuandika inatosha. Je wewe umefanya nini kuacha alama katika jamii? pamoja na mshamba_mkuu na Muhindi Wa Kuchoma
1.Nilitoa eneo kwa ajili ya kuweka takataka za kijiji
2.nilichangia matofali 100 ya kanisa
3.nilimchangia mchungaji pikipiki ya kutembea
4.nilitoa mchango ijengwe ofisi ya kijiji
5.nilishauri polisi jamii kuanzishwa
Kuna mengi sana
 
Similar threads

Ushawahi pata hisia za kutaka kutembelea sehemu au nyumba ambayo uliishi utotoni? Una kumbukumbu za kutosha kuhusu nyumba nyumba hii au sehemu ambayo umekulia? Karibu tukumbushane maisha ya utotoni na makuzi tuliyokulia hapa. Binafsi: Nimekulia Kinondoni B. Nilikuwa naona sifa sana kujiita...
Replies
29
Views
540
Licha ya mtandao wa Twitter kuzuiliwa nchini China, Billionea ambaye ndiye mmiliki wa mtandao huo anatarajiwa kuanza ziara yake nchini humo wiki hii. Hii inakuwa ni mara ya pili baada ya miaka mitatu kupita, Elon Musk kwenda nchini China, kwani mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2020 alipokwenda...
Replies
7
Views
195

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom