Mkasa: Jinsi nilivyofundishwa uchawi

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

SEHEMU YA KWANZA.
Nikiwa nimerudi kutoka shuleni nilikutana na mama nje ambaye alinambia tumepata mgeni ambaye atakua akitusaidia kazi za ndani yaani dada wa kazi, kutokana na uchovu na fimbo za siku hio hata sikua na hamu ya kutaka kujua zaidi kuhusu jambo hilo nilimjibu mama kwa kifupi.

“haya”. Huku nikielekea ndani ambapo nilifika na kumkuta dada mmoja aliyekua na umri kati na miaka kumi na saba hadi ishirini ambaye alinichangamkia kama mtu tuliyejuana siku nyingi.

“mambo clara habari ya shule”. Aliongea dada Yule. Na kunifanya nishangae kalijuaje jina langu lakini nilihisi huenda mama alishamwambia kwamba ana mtoto anaeitwa clara.

“nzuri shikamoo dada,”. Niimjibu kwa heshima kwa kua alikua ameninzidi ki umri hivyo alistahili heshima kwani mimi nilikua darasa la nne tu, baada ya kumjibu nilielekea ndani na kulitua begi langu pia nilikuta mizigo ya dada Yule ambaye ilionesha hakua amefika muda mrefu.

Kwakua tulikua tukipata chakula shuleni nilipitiliza kulala ambapo usingizi ulinipitia na nilikuja kustuka majira ya saa sita usiku ambapo nilimuona dada Yule akiwa ameketi kitandani uchi wa mnyama huku akiwa ameinguanisha mikono yake kama mtu aliyekua akisali.

Moyo wangu uliogopa sana na nililazimika kufikicha macho ili nijue kwamba ilikua ndoto au la na niligundua kwamba haikua ndoto bali ilikua ni ukweli kabisa.

Kisha dada Yule akasimama na kuanza kutembea tembea ndani ya chumba changu huku mikono akiwa ameikunja vile vile na macho yake yakiwa yamefungwa, na kisha baada ya muda, alirudi kitandani na kuketi kama alivyokua awali.

Baada ya dakika tano nilimshuhudia mama nae akija chumbani akiwa amevaa kama dada Yule, hapo nilishindwa kujizuia na kutamka.

“haaa, mama kumbe nawe mchawi”. Niliongea kwa mashangao kauli ambayo ilimstua sana mama na kisha akanisogelea bila uwoga na kuniambia.

“shhhhhhhhh, hakuna haja ya kujificha sasa mimi ni mchawi ndio na hata wewe ni lazima uwe mchawi au laa nikuue kama nilivyomfanya baba yako”.aiongea mama maneno ambayo yalinistua sana na kunifanya nianze kutetemeka.

“unaogopa nini? Mimi ni mchawi toka nilipokua na umri kama wewe umewahi kunigundua? Umewahi kuniona nikitisha? Acha ujinga mwanangu”. Aliongea mama na baada ya muda tulimshuhudia dada Yule wa kazi akiinuka huku macho yake yakiwa yanawaka kama tochi. Na hapo nilimshuhudia mama akipiga goti na kuanza kumsujudu dada Yule.

“naam mkuu, nimekuletea binti huyu akiwa kama mwanachama mpya”. Aliongea mama ambapo dada Yule alinitazama kwa makini sana kisha kumgeukia mama.

“inabidi tumfundishe taratibu kabla ya kumtambulisha kwa wenzetu”. Aliongea dada Yule kisha nilimshuhudia mama akiinuka na kunigeukia.

“mwanangu clara, wewe ndiye wa pekee kwangu na nimekuteua wewe upate kujua vitu vyangu vya ndani, na mbona sikuwaambia kaka zako? Naomba uniisitiri”. Aliongea mama na kunipa mtihani mgumu sana katika umri mdogo na mpaka apo sikua nimesema jambo lolote.

Mwisho mama alichukua unga mweupe na kunipaka katika paji la uso kisha tulijikuta sehemu nyingine kabisa ambayo ilikua ngeni kabisa lakini iionesha ilikua ni katika msitu uliopo kando ya barabara.

Kwani magari yalikua yakisikika yakipiita,
“mwanangu, huu ni msitu wa wachawi msitu ambao ukiingia kama si mchawi basi huwezi toka na utafanywa kafara”. Aliongea mama kauli ambayo ilinifanya niwaone wachawi ni watu wabaya.

“Watu wengi wamepotea katika msitu huu na vifo vyao vilikua vya kutatanisha , hiii ni kwasababu wanachukuliwa na mizimu na kufanywa kafara lakini mchawi si mtu mbaya ila wapo ambao wanautumia uchwi vibaya kwa kufanya visasi na mauaji”. Aliongea mama mambo mengi kuhusu uchawi kisha alinifundisha dawa nyingi sana za kichwawi ikiwemo za kupotea na kiini macho.

Kwakua muda ulikua umekwenda tulirejea nyumbani ambapo bado nilikua na maswali mengi sana na siku hio nilipanga ktoka na kwenda kwa rafiki yangu zuwena nipate kumuuliza mambo kadhaa kuhusu hali iliyonitokea jana usiku.

Nilimuaga mama vizuri na kumwambia nilikua nikienda kwa rafiki yang na alichonisisitiza ni kuwahi kurudi.
Nilipofika nyumbani kwa rafiki yangu kulikua kimya sana ambapo nilibisha hodi mara tatu na kufunguliwa na zuwena mwenyewe
“mambo clara”. Alinisalimu zuwena huku akinikaribisha ndani ambapo tulipiga storiza hapa na pale mwisho niliamua kumuuliza swali.

“eti unawafahamu wachawi”. Nilihoji
“eee, ni wanatisha sana na ni wabaya, wauaji na hawana huruma”. Zuwena aliongea kana kwamba ni mtu anaejua mambo mengi sana kuhusu uchawi.

“basi nikwambie kitu zuwena, mwenzio mama yangu ni……”. Kabla sijamaliza ilikuja sauti kichwani mwangu ambayo niliitambua kwamba ni ya mama.

“clara unataka kufanya nini?” iliskika sauti hio
Je nini kilifuata
 

Dr santos

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 4, 2023
Messages
251
Reaction score
571
Points
0
SEHEMU YA PILi:
INAENDELEA: uso ulinishuka ghafla baada ya kujikuta nikitaka kutoa siri ya mama kwa rafiki yangu zuwena.
“rudi nyumbani haraka”. Iliskika sauti ya mama ambapo haukupita muda zuwena alipitiwa na usingizi nami nilitumia afasi hio kuondoka haraka huku nikiwaza jambo la kumweleza mama endapo nikirudi nyumbani.

Nilipofika nyumbani nilimkuta mama akiwa nje uso wake akiwa ameukunja hadi nilianza kutetemeka kwani sijawahi kumwona mama akiwa amefura namna ile na nilijua lazima jambo lile litakua limemuudhi sana.

“sasa na ugemwambia ungefaidika nini”. Alihoji mama ambapo nami sikua na jibu kwani ukweli ni kwamba sikua nikipata faida yoyote. Baada ya mama kunisema nilirudi nyumbani na kukutana na dada wa kazi ambaye alikua ameketi.

“naona umerudi lakini ni mwiko kutoa siri a wachawi la sivyo kifo kitakuhusu”. Aliongea dada Yule nami sikujibu chochote zaidi ya kwenda chumbani ambapo nilifika na kuanza kulia kilio cha kwikwi kwani sikuona kimbilio langu.
Kama mama alimuua baba na anataka mimi niwe mchawi basi niliona kabisa jambo la kua mchawi haliepukiki kabisa.

Akili yangu ilianza kubadilika taratibu ambapo nilianza kufikiria jinsi nitakavyowakomesha maadui zangu na wale wote wanaonikosea hasa walimu wanaochapa sana bakora, wakati nikiendelea kuwaza hayo usingizi ulinipitia.

Nikiwa katika usingizi mzito nilijiwa na njozi iliyonionesha nikiwa katika msitu wa wachawi nikiwa na mama aliyekua akinionesha mambo mengi na dawa nyingi za kichawi, ambapo alinionesha mti mmoja aliouita mti mweupe kutokana na rangi yake ambao ulikua a magamba meupe ambapo alinitajia baadhi ya kazi za mti ule na una maana gani katika uchawi.

“kuna aina mbili za uchawi mwanangu, mweupe na mweusi na uchawi wenye asili ya khali iliogunduliwa nchini uajemi pia kuna uchawi wa kutabiri nyota peke lakini unaotumika sana ni huu mweupe na mweusi kwani hauhitaji elimu ukilinganisha na aina zingine za uchawi hambazo huhitaji mtu ajue kusoma na kuandika”.

Mama alinielekeza mambo mengi jinsi uchawi mweupe na mweusi unavyofanya kazi na yeye alitumia aina ipi ya uchawi

“uchawi mweupe na mweusi vinategemena kwa kiasi kikubwa kwani uchawi mweupe hutumika kutengeneza uchawi mweusi ambao huu ndio wenye kuweka watu misukule na wenye kuhitaji kafara ya damu ili uwe na nguvu maradufu”.

Aliogeza mama na wakati huo sikua nimesema chochote alikua akiongea yeye tu mwisho aliniambia angenifundisha kutengeneza dawa za kichawi kupitia mizizi ya miti mbalimbali pia angenifundisha kutega mitego ya kichawi pamoja na kafara kwani ili nipokelewe ilihitajika kafara ya damu.

Nilistuka jioni na nilikua na jaa kali sana, siku hio mvua ilinyesha muda mrefu sana na kutokana nyumba yetu haikua na dari basi nilijikuta nikikosa usingizi baada ya kupata chakula cha usiku sikuweza kupata tena usingizi kutokana na kulala mchana hadi mama alipokuja kuiamsha majira ya saa saba usiku.

“mwanangu amka twende tukafanye kazi niliyokuelekeza mchana”. Aliogea mama ambapo nami sikua na ubishi ambapo mama alinielekeza nivue nguo zote kisha akipa vazi la kaniki yenye rangi nyeusi na kunielekeza namna ya kufunga baada ya hapo aliamka na dada ambaye hata sikumjua jina lake kisha tuliketi chini na kushikana mikono kisha tulijikuta katika eneo jingine ambalo hakika lilikua geni katika macho yangu.

“mwanangu umeuona huo mti, majani yake hutumika kuona visivyoonekana mfano misukule na pesa za chuma ulete, pia ukisaga maganda yake na kupaka unga wake wewe unakua huonekani hutumika na wachawi katika shuguli za kuwanga na ulozi”. Alongea mama kisha akaendelea kunifundisha na kunielekeza namna ya kuchimba mizizi ile kisha alinielekeza vitu vingi sana pamoja na dawa za kutega mitego ya kichawi mfano ajali za kichawi pia dawa za kutolea kafara.

Mwisho tulishikana tena tukiwa tumeketi chini na tulijikuta tumetokea mbele ya nyumba moja nzuri ambayo ni ya tajiri mmoja pale kijijini.

“hapa tunaenda kufanya nini”. Nilihoji
“tunakwenda kuifungulia misukule yake kwani wachawi hua tuna tabia ya kuumbuana, hapa tunakwenda kumkomoa kwani

hata yeye anatumia utajiri wa nguvu za giza”.
Aliongea mama kisha akanipaka unga kwenye paji la uso na sehemu ya makalio
alinambia nijipake, baada ya hapo mama na dada, waligeuka na kutembea kinyume nyume na kuusogelea ukuta wa nyumba hio ambapo nilishangaa kuona uwazi mkubwa kisha tukaingia na uwazi huo ukapotea.

Ajabu tulipofika chumbani kwa mzee Yule aliyetambulika kama mzee konzo hatukukuta mtu na hakukua na kutanda bali ni bwawa kubwa sana ambalo lilianza kujaa maji ghafla na nilijikuta nikipaliwa kuokana na maji kufikia shingoni na hatimaye kichwani, mama alinibeba mabegani na kakukua na ujanja wa kupotea kwani dawa zetu zilikua zimeshaloa.

Niliona kifo kikiwa mbele yetu.
Je nini kilifuata
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Subscribed..
Usituache njiani mzee story tamu sana
 

Dr santos

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 4, 2023
Messages
251
Reaction score
571
Points
0
SHEMU YA TATU

INAENDELEA; Niliamka asubuhi nikiwa nimechoka sana, na kwakua ilikua ni siku ja jumapili nilishukuru sana kwani niliutumia muda huo kupumzika.

nlimfuata mama akiwa katika sehemu tulivu na kutaka kumuuliza juu ya hali ya jana ambapo alinambia mzee Yule alikua na utajiri wa misukule na mbali na hapo alikua na kinga kubwa sana pia shariti lake kubwa ni kutolala kitandani, na ndio maana tulipoingia tuliona maji tu.

Nilishangaa kiukweli kwani sikutaraji kwamba uchawi unaweza kua na nguvu hiyo, nilitamani kua mchawii ili niwakomeshe maadui na yoyote atadiriki kunionea hasa shuleni.

Mama alinieleza vitu vingi sana kuhusu uchawi mweupe na mweusi kwamba uchawi mweupe ndio hugeuzwa na kua uchawi mweusi na pia kuna wanyama ambao wana uhusiano na kila aina ya uchawi.

Kwa uchawi mweupe wengi hutumia paka weupe au njiwa weupe katika ulozi lakini vile vile kwa uchawi mweusi hutumia paka weusi ambao inasadikika wana nguvu za kichawi za asili.

Baada ya kuongea na mama kwa muda mrefu alikuja dada na kutuita ili tukapate chakula cha mchana, baada ya kula mama aliniambia anataka anipeleke mahali nikajifunze namna ya kutengeneza dawa za kichawi kwa kutumia mizizi tuliyokata jana.

Tulianza safari kuelekea kwenye shamba letu kubwa la mahindi ambalo katikati lilikua na kijumba kidogo cha nyasi ambacho sikuwahi kukiona japo tulikua tukilima shamba hilo miaka yote.
Tuliingia na mama alinielekeza namna ya kutengeneza na kuzikausha papo hapo kwa kutumia uchawi.

“ukisha maliza kazi hii leo nnitaenda kukutambulisha kua mwanachama mpya”. Aliongea mama
“sawa ila mimi sitaki kuua”. Niliongea kwa woga sana.
“nani aliyekwambia wachawi wanaua? Sisi tunatumia uchawi katika kuongeza mazao mashambani”. Aliongea mama na kunifanya niwe na amani.

Masaa yalisogea hadi ilipohitimu usiku wa manane ambapo mama alikuja kuniamsha kisha tukapotea na kutua katika uwanja wa shule yetu, kwakua tuliwahi tulikuta watu wachache sana huku wengine wakiendelea kutua kila mmoja.

Nilishangaa kuwaona na baadhi ya walimu, moyo wangu ulistuka sana na nilishindwa kujizuia
“haaa, hadi mwalimu msinza”. Nilimwambia mama ambaye aliweka kidole mdomoni kuashiria ninyamaze.
Watu waiongezeka na mwisho alitua mzee mmoja wa makamo akiwa na kofia nyekundu na kaniki nyeupe na nyekundu pmoja na usinga.

Wachawi wote waliinama kwa heshima nami baada ya kuona peke ndiye nimesimama, niliinama kama wenzangu na baada ya muda wote tuliinuka.
“tumepata mgeni na tunaimani ataifanya kazi hii vizuri na kwa ushirikiano bila kutoa siri zetu”. Aliongea mzee Yule ambapo zilipigwa ngoma kisha moto mkubwa uliwashwa na nilishuhudia kina mama wawili wakija na maiti mbili za kiume na inaonesha walikua na umri usiozidi miaka 25.

Wachawi wote walishangilia na kucheza kwa furaha kisha ulifika ule wasaa wa kula nyama ambao ndio ulikua wakati mgumu kwangu katika nyakati zote nilizowahi kupitia duniani.
Kwenye foleni mimi ndiye nilikua wa kwanza, kisha alifuata mama na wa tatu alikua dada, nilipewa pande kubwa la nyama ambalo lilinifanya nitetemeke mwili mzima hadi kupelekea niidondodhe nyama ile.

Nilipogeuka niliona watu wakinikata jicho hasa mama kwani nilikua namtia aibu ambapo ilibidi niokote kipande kile kisha nilisogea walipoketi mama na dada ambao walikua washamaliza kula nyama zao mimi nikiwa bado naogopa.
Nilianza kula mpaka waliponilazimisha sana na kupelekea mimi kua wa mwisho kisha mkuu wa wachawi alipiga makofi na watu wote walinyamaza kumsikiliza.
Baada ya muda alituita mimi na mama pamoja na dada ambapo mama alipiga goti moja huku tukiwa tumesimama.
“karibu sana binti nakupa hii, hakikisha unaitunza na hailoi na maji itakuepusha na hatari, maelekezo mengine utapewa na mama yako”. Aliogea mzee Yule huku akinivisha hirizi nyekundu mkono wa kushoto kisha akamgeukia dada
“karibu na wewe katika jamii yetu ya wachawi, nina imani unajua kila kitu”. aliongea mzee Yule kisha mama aliinuka na ulikua ni muda wa kutawanyika kila mtu aendelee na shughuli zake kama kuwanga na kuroga kama kawaida.
Tulipotea na kutokea makaburini ambapo

mama aliniambia
“unatakiwa kupeleka kafara ya kukaribishwa kama mwanachama mpya, tunatakiwa kufukua kaburi”.

Je nini kilifuata
 

Similar threads

  • Article Article
MWANZO Huu ni mkasa wangu ulionikuta baada ya kuhamishwa kutoka kigoma to dar es salaam early 2004s Baada ya kumaliza kazi zangu za kila siku ni kawaida yangu kutembelea kijiwe kwaajili ya kupata mawili matatu kutoka kwa watu mbalimbali wa rika tofauti lengo ni kutokua mpweke pia ku refresh...
Replies
60
Views
2K
Papa Francis amewaruhusu mapadre kuwabariki wapenzi wa jinsi moja, yakiwa ni maendeleo makubwa kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja na mahusiano mengine ya kijinsia wanaofahamika kama LGBT katika Kanisa Katoliki la Roma. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki la Roma amesema makasisi wanapaswa...
Replies
9
Views
281
habari zenu hii ni true story by manenge. leo nimeona niwape japo kwa kirefu sana kuhusu hii kazi yangu ya professional tour guide,kwa majina yangu nileyepewa na wazazi wangu naitwa raymond joseph mushi,nimzaliwa wa machame. nimeona ni share nanyi ilimjue kuhusu hii kazi ambayo haina...
Replies
43
Views
1K
JINSI YA KUREJESHA KWA KUPAKA RANGI CHUPA ZA KIOO Chupa za kioo (glass) ziko za aina nyingi, zenye rangi, na ambazo hazina rangi yaani (transparent). Chupa hizi mara nyingi huwa ni mabaki/uchafu (trash) baada ya kutumia vilivyo ndani kama jibini, soda, bia, juice, mafuta, unga, asali au...
Replies
10
Views
696
Kusanya vipande vya sabuni Ni bora kutumia sabuni isiyo na harufu; kwa njia hii, unaweza kuongeza harufu yako mwenyewe. Ikiwa unataka kutumia sabuni yenye harufu nzuri, hakikisha kwamba mabaki yote yana harufu sawa, vinginevyo unaweza kuishia na mchanganyiko wa harufu mbaya. Ikiwa unataka...
Replies
6
Views
506

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom