Mwanaume kusaidiwa kulipa mahari ni sawa?

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,897
Reaction score
3,986
Points
113
Nawasalimu wakuu

Swala la mahari limekua kipengele sana kwa vijana siku hizi wanalalamika kuwa kiasi ni kikubwa, wengine wanaona nikama imekua biashara yaani watoto wakike wamekua mtaji kwa wazazi wao...


Ninacho taka kuuliza
  • Ni sawa mwanaume kusaidiwa kutoa mahari na mpenzi wako wa kike?
  • Je ulipwaji wa Mahari ina ulazima wowote?.
  • Je ni Agizo la kibiblia? Na kama ni hivyo Je! Adamu alitoa mahari kwa nani ili ampate Hawa?
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Mwanzo 34:12 NEN
Niambieni kiasi cha mahari na zawadi nitakayoileta, hata iwe kubwa kiasi gani, nami nitawalipa chochote mtakachodai. Nipeni tu huyu msichana awe mke wangu.”
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Ndoa ya kwanza ilifungishwa na Mungu mwenyewe…Na hakukuhusika mahari wala viapo…Hiyo yote ni kwasababu Hawa hakuwa na Baba wala Mama…

Lakini sasa wake zetu wanao wazazi wao..hatuwatoi ubavuni mwetu kama Adamu alivyompata Hawa..Hatuna budi kuwatoa kutoka kwa wazazi wao…Na wazazi wao waliwalea na kuwatunza kwa gharama zao.

Hivyo sio vyema kuwaiba kutoka kwa wazazi wao na kuwafanya wetu…Hatuna budi kufuata taratibu za kuwatoa kutoka kwao na kuwaleta kwetu…Na taratibu hizo zinahusisha ulipwaji wa mahari. Ulipwaji wa mahari hakumaanishi kumnunua huyo mwanamke…hapana! Bali kumthaminisha Yule binti kwamba hajaokotwa tu.

Laiti kama tungekuwa tunawapata wake zetu kama Adamu kwamba Mungu anatuletea usingizi na kuwatoa kutoka ubavuni mwetu..hapo kungekuwa hakuna haja ya mahari wala ndoa kanisani..hapo mahari ina ulazima wowote?..haina ulazima kwasababu wametoka kwetu(kwenye miili yetu kama Adamu)…lakini tulio nao hawajatoka kwetu wametoka kwa wengine… Hivyo ni lazima mtu upitie hatua za kuposa, na kuposa kuna taratibu zake ikiwemo mahari.

Hivyo hatua hiyo ikishavukwa kinachofuata sasa ni kwenda kanisani…Tulipowatoa! tumewatoa katika jamii..watu wote walikuwa wanajua binti Yule hajaolewa..hivyo binti kwa idhini yake sasa hana budi kwenda kukiri mbele ya umati wa jamii ya watu wake na mbele ya kanisa la Kristo na mbele ya Mungu kwamba amekubali kwa idhini yake mwenyewe kuolewa na kijana huyo..Na kijana naye vivyo hivyo anatamka kwa kukiri..kuwa ushuhuda..Na hapo ndipo Mungu anapoiridhia kuwa ni ndoa takatifu ya kikristo.
 

mshamba_mkuu

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
1,563
Reaction score
4,525
Points
0
Wewe ndio umesema mwanamke anakuwa kama bidhaa. Sio maana yake wewe ndio umeipa hiyo maana
inachochea mfumo dume kandamizi, mila potofu hizi
Njaa hizi unashundwa kulipa mahari utaweza muhudumia mwanangu? mahari kama mtu halipi yote haoi kwangu mzee
naweza nikawa na hela za kumhudumia mwanao ila nikamnyanyasa.... hela sio kipimo cha upendo
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
inachochea mfumo dume kandamizi, mila potofu hizi

naweza nikawa na hela za kumhudumia mwanao ila nikamnyanyasa.... hela sio kipimo cha upendo
Hebu Jaribu kumkuna mwanamke na elfu kumi kumi za million uone kama atakuwa anaendelea kuwashwa mgongo

Pesa sabuni ya roho wewe dogo

Kumnyanyasa inaingiliana vipi na mahari?
 

mshamba_mkuu

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
1,563
Reaction score
4,525
Points
0
Hebu Jaribu kumkuna mwanamke na elfu kumi kumi za million uone kama atakuwa anaendelea kuwashwa mgongo

Pesa sabuni ya roho wewe dogo

Kumnyanyasa inaingiliana vipi na mahari?
kwahiyo kama mtu atashindwa kukamilisha mahari basi asioe?? kwamba mwanao akiolewa na tajiri ndo atakua na furaha??

this is classism
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
kwahiyo kama mtu atashindwa kukamilisha mahari basi asioe?? kwamba mwanao akiolewa na tajiri ndo atakua na furaha??

this is classism
aliyekwambia kuolewa na tajiri nani?
kama unashindwa kulipa mahari utawezaje muhudumia?

Ukija hata kama shangazi yangu unaweka elfu 30 kwenye barua ya utambulisho nakufyeka na panga we dogo
 

Similar threads

Umri ambao mwanaume ana uzazi mkubwa zaidi ni kati ya miaka 22 na 25. Inapendekezwa kuwa na watoto kabla ya kufikia umri wa miaka 35. Baada ya umri huu, uzazi wa kiume huanza kudhoofika. Baada ya miaka 35, manii inaweza kusababisha ujauzito ambapo mabadiliko yanaweza kutokea. Zaidi ya hayo...
Replies
10
Views
281
Wakubwa shkamooni! Kiujumla inadaiwa wanawake ndio wana uo uwezo wa kutunza hela kuliko wanaume.. kwaili nakataa labda kama wanazungumzia wanawake wa zamani... Hawa wa siku hizi wanaspend sana kuliko men, wananunua kila kitu kilicho mbele yao, sijui ni ugonjwa? Kwa sisi men tuko vizuri mno...
Replies
33
Views
714
Mbali ya kuwa na ndevu hizi humfanya mwanaume avutie zaidi kwa mwanamke, hizi ni faida za kiafya za mwanaume kufuga ndevu;- 1. Ndevu hulinda uso dhidi ya kemikali hatari pamoja na hewa chafu ambazo kimsingi husababisha uharibu wa chembe chembe hai za mwanadamu. Pia husaidia ngozi ya...
Replies
37
Views
534
Wanaume !! Kila mwenye jinsia ya kiume anaweza kuwa mwanaume, lakini sio wote wenye uwezo wa kuwa wanaume wanaostahili kuitwa wanaume. Je sifa za mwanaume ni hizi? Wanaume halisi ni sugu; hawapaswi kulia? Mwanaume hatakiwi kula chips mayai? Wanaume halisi hawakubali yeyote awaongoze? Wanaume ni...
Replies
44
Views
911
Wanaume wengi waliooa hawapendezwi na urafiki kati ya wake zao na wanaume wengine. Wengine wanaenda mbali sana kukataza wake zao wasijichanganye na wanaume. Wanawake walio kwenye ndoa wengi wanajikuta marafiki zao wakubwa ni mashemeji zao na ndugu zao. Japo wanajichanganya na wanaume hukuti...
Replies
11
Views
293

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom