Nyoka na kujamiiana: Kwa nini anakonda wa kike hummeza wa kiume baada ya tendo?

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Gily

KF Founder & Dragon IGM
Staff member
Jun 4, 2023
7,019
22,617
113
Ngono ni jambo gumu. Kadiri tafiti zinavyofanywa kuhusu ngono, ndivyo mambo ya kushangaza yanavyozidi kuja.

Jesus Rivas ni mtaalamu wa nyoka anayefanya kazi katika Chuo Kikuu cha Mexico Highlands nchini Marekani. Hivi karibuni Jesus alijifunza jambo la ajabu kuhusu maisha ya ngono ya nyoka mkubwa anayepatikana Amerika Kusini, anakonda.

Anakonda mwanamke hula dume baada ya ngono. Hapo awali, wanasayansi waliamini kwamba nyoka dunme hutawala wakati ngono. Lakini habari hii kuhusu anakonda jike imewashtua. Kulingana na Jesus, hii ndiyo habari ya hivi punde ya kushtusha kuhusu kujamiiana ya nyoka.

Kwa viumbe wengine, wanaume ni wakubwa, wana nguvu zaidi, lakini katika kesi ya nyoka ni kinyume chake. Kwa nyoka aina ya anakonda, jike mara nyingi ni mkubwa mara tano kuliko dume. Kwa hivyo anaweza kummeza kwa urahisi.

Ukubwa wa nyoka wa kike humsaidia kutaga mayai zaidi na kuangua watoto. Kwa hiyo nyoka wadogo wa kiume hutafuta jike kama washirika wa ngono, lakini swali ni jinsi gani wanaweza kupata nyoka jike kwa ngono wakati nyoka hawaoni vizuri?

Utafiti umegundua kuwa hamu ya ngono inaonyeshwa kwanza na jike. Nyoka wa kike hutoa gamba lake anapotoka kwenye hali ya baridi kali au joto. Kisha hutoa homoni inayoitwa pheromone. Kutokana na hali hiyo, nyoka wa kiume huvutiwa kwa msaada wa homoni hiyo.

Kadiri jike anavyokuwa mkubwa wakati wa msimu wa kuzaliana, ndivyo homoni nyingi zaidi hutolewa kutoka kwa mwili wake. Kwa kumfuatilia, nyoka wa kiume humfikia nyoka wa kike kwa ajili kufanya ngono.


BBC SWAHILI.
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
Staff member
Jun 4, 2023
7,019
22,617
113
Kwanini nyoka jike hujamiana na madume wengi?
Ikiwa hajaridhika na uhusiano wa kimapenzi na nyoka wa kiume, mara moja atamsukuma na kutafuta mwenzi mwingine. Sasa swali kubwa ni je, nyoka jike anaamuaje nyoka dume hafai au anafaa kufanya naye mapenzi?

Wanasayansi hawajaweza kupata jibu la wazi la swali hilo hadi leo. Inaweza kutegemea uwezo na tamaa ya nyoka wa kiume. Au jike anaweza kuwa anapata hisia ya nguvu za dume kwa uwezo wake wa kugusa.

Si lazima nyoka jike afanye ngono na nyoka mmoja tu. Nyoka wa kike wameonekana mara nyingi wakifanya mapenzi na nyoka kadhaa wa kiume. Kwa upande mwingine, nyoka wa kiume huwa waaminifu kwa jike anapokubali kufanya ngono. Hata nyoka wa kike anapolala, nyoka wa kiume huendelea kumzunguka.

Labda ni kuongezeka kwa hamu ya ngono au kwa kufanya ngono na nyoka kadhaa, nyoka wa kike huamua ni dume gani atakayezaa mtoto mwenye nguvu. La muhimu kujua ni kuwa, madhumuni ya ngono kwa nyoka ni kuzaa tu.

Jike ana uwezo wa kuhifadhi manii ya nyoka wa kiume katika mwili wake kwa siku chache. Huenda hiyo ndiyo sababu ya kufanya ngono na nyoka kadhaa wa kiume, akihifadhi mbegu za kiume ambazo zinaweza kutoa mtoto mwenye afya zaidi.

Tazama maumbile ya asili; nyoka za kike hutoa aina maalum ya homoni ya pheromone baada ya ngono mara kadhaa ili kutuma ujumbe kwa nyoka wa kiume kwamba hatafanya ngono tena. Hakuna anayeweza kumlazimisha nyoka jike.

Ndani ya njia ya uzazi ya nyoka ya kike hufungwa. Yaani hata nyoka dume akitaka hawezi kuzalisha kwa kufanya mapenzi na jike maana mbegu zake haziingii ndani.


BBC SWAHILI.
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
Staff member
Jun 4, 2023
7,019
22,617
113
Anakonda jike humeza dume baada ya tendo

Si mara zote anakonda jike hula dume baada ya kujamiiana, lakini haijulikani ni wakati gani anakonda wa kike huamua kummeza dume baada ya kujamiiana.

Sababu ya jambo hilo haijajulikana, lakini kifo cha nyoka dume kinaweza kuwa sababu ya kumpa anakonda jike mlo wenye lishe, kwani anakonda jike mjamzito hali wala kunywa chochote kwa muda wa miezi saba.

Mitindo wa ngono katika nyoka ni migumu kama wanadamu, lakini nyoka wana tabia sawa na buibui. Ni wakubwa kwa umbo kuliko nyoka dume, na ushindani mkubwa hutokea miongoni mwa nyoka dume wakijaribu kuvutia nyoka jike. Nyoka jike ana udhibiti kamili wakati wa kujamiiana na mara nyingi hula dume baada ya ngono.

BBC SWAHILI
 

The great manenge

New member
Platinum Villager
Jul 8, 2023
1,320
2,995
0
Anakonda jike humeza dume baada ya tendo

Si mara zote anakonda jike hula dume baada ya kujamiiana, lakini haijulikani ni wakati gani anakonda wa kike huamua kummeza dume baada ya kujamiiana.

Sababu ya jambo hilo haijajulikana, lakini kifo cha nyoka dume kinaweza kuwa sababu ya kumpa anakonda jike mlo wenye lishe, kwani anakonda jike mjamzito hali wala kunywa chochote kwa muda wa miezi saba.

Mitindo wa ngono katika nyoka ni migumu kama wanadamu, lakini nyoka wana tabia sawa na buibui. Ni wakubwa kwa umbo kuliko nyoka dume, na ushindani mkubwa hutokea miongoni mwa nyoka dume wakijaribu kuvutia nyoka jike. Nyoka jike ana udhibiti kamili wakati wa kujamiiana na mara nyingi hula dume baada ya ngono.

BBC SWAHILI
Ngono ni tamu mpaka kwa wanyama ushawahi kumuoana nyani kwenye ule mchezo jamaa wanakatikankinomq
 

Similar threads

Habari wanakijiji Wakati niko shule ya msingi tukifundishwa kuwa ukiumwa na nyoka unatakiwa ufunge juu ulipoumwa na nyoka kuzuia damu yenye sumu kisambaa mwilini. Hivi karibuni nimeona taarifa tofauti zikitolewa kuwa si sahihi. Taarifa zinasema "Baadhi ya watu hufunga kwa nguvu sehemu iliyoumwa...
Replies
5
Views
212
Dar es Salaam. Utafiti uliofanywa na idara ya magonjwa ya mfumo wa mkojo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa umebaini mitindo ya kujamiiana inaweza kusababisha uume kuvunjika. Utafiti huo unaeleza miongoni mwa mikao hiyo ni mwanamke kukalia uume. Utafiti huo uliochapishwa leo Jumanne, Julai 4...
Replies
47
Views
1K
Kutoka 8:1 BWANA akamwambia Musa, Ingia kwa Farao, ukamwambie, BWANA asema hivi, Wape watu wangu ruhusa, ili wapate kunitumikia. Maandiko hapo juu yanasema bila kificho chochote yaani yuko direct lipi lilikua ni LENGO la kuwatoa wana Waisraeli misri. Sababu ya kuwatoa watu wake misri ni ili...
Replies
12
Views
83
Zab 10:1 Ee BWANA, kwa nini wasimama mbali? Kwani kujificha nyakati za shida? Hello! Nawasalimu wa ndugu kwa jina la Yesu, mko njema sio! Mimi ni mzima sana, twende kwenye mada; Umesha wai kupitia changamoto mpaka ukahisi kama Mungu hayupo, hakuoni wala hakusikii, yaani ukahisi amekuacha...
Replies
4
Views
379
Top Bottom